Habari za Punde

Baraza la mawaziri la kwanza baada ya mapinduzi 1964


Pichani ni Baraza la Mawaziri la mwanzo la Jamhuri ya Watu wa Zanzibar likiwa pamoja katika jumba la Beit el-Ajaib tarehe 13 Januari, 1964, siku chache baada ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Kutoka kushoto kwenda kulia ni Abdulaziz Twala (Msaidizi Waziri katika Ofisi ya Rais), Aboud Jumbe (Waziri wa Siha na Majumba), Hasnu Makame (Waziri wa Fedha na Maendeleo), Othman Shariff (Waziri wa Elimu na Mila), Abdulrahman Babu (Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara), Abeid Karume (Rais wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar), Abdallah Kassim Hanga (Makamu wa Rais), Saleh Saadalla (Waziri wa Kilimo), Idris Abdul Wakil (Waziri wa Kazi, Njia na Nguvu za Umeme) na Hassan Nassor Moyo (Msaidizi Waziri wa Kazi, Njia na Nguvu za Umeme).

Picha na Maelezo haya ni kwa hisani kubwa ya Mdau Ismail Jussa, Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe, Unguja, Zanzibar

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.