Januari 28, 2013: Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dkt. Edmund Mvungi (katikati) akibadilishana mawazo na Makamishina wa Tume ya Pamoja ya Fedha (JFC), Dkt. Juma Ngasongwa (kulia) na Mhe. Othman Masoud, ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) mara baada ya JFC kuwasilisha maoni yao kuhusu Katiba Mpya wakati wa mkutano wao uliofanyika katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam.
Jumatano Januari 9, 2013: Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk. Edmund Mvungi (katikati) akizungumza na Viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA) waliofika katika Ofisi za Makao Makuu ya Tume Jijini Dar es Salaam leo kuwasilisha maoni yao kuhusu Katiba Mpya.
Na Mwandishi Wetu
Mjumbe
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba aliyekuwa akipatiwa matibabu nchini Afrika
Kusini amefariki dunia.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw.
Assaa Rashid leo jioni (Jumanne, Novemba 12, 2013), Dkt. Sendongo Mvungi majira
ya saa 8:30 mchana kwa saa za Afrika ya Kusini akiwa katika Hospitali ya
Milpark.
“Kwa
masikitiko makubwa, Tume inawafahamisha wananchi kuwa Mjumbe wake, Dkt.
Sengondo Mvungi aliyekuwa akipata matibabu katika Hospital ya Milpark iliyopo
jijini Johannesburg nchini Afrika
Kusini amefariki dunia leo (Jumanne, Novemba 12, 2013) saa 8:30 mchana kwa saa
za Afrika ya Kusini,” amesema Bw. Rashid katika taarifa yake fupi ya awali na
kuongeza:
“Taratibu
za kuusafirisha mwili wa marehemu kutoka nchini Afrika Kusini kuja nchini kwa
mazishi zinaendelea na taarifa zaidi zitatolewa kesho (Jumatano, Novemba 13,
2013),” ameongeza.
Marehemu
Dkt. Mvungi alisafirishwa siku ya Alhamisi, Novemba 7, 2013 kwenda nchini
Afrika Kusini kwa uchunguzi na matibabu zaidi akitokea Kitengo cha Mifupa
Muhimbili (MOI) aliokuwa amelazwa baada ya kuvamiwa nyumbani kwake Kibamba,
wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na watu waliomjeruhi vibaya kichwani
usiku wa kuamkia siku ya Jumapili, Novemba 3, 2013.
Katika
taarifa yake, Tume pia imewaomba watanzania wote kuungana na familia, ndugu,
jamaa na marafiki wa marehemu Dkt. Mvungi katika kuomboleza msiba huo.
No comments:
Post a Comment