Habari za Punde

Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Italia Cesare Prandelli kuwasili Zenj.

Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Said Ali Mbarouk, akizungumza na Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Italia, Cesare Prandelli, alipowasili Zanzibar, Akizungumzia juu ya kuazisha kwa Ushirikiano wa masuala ya michezo na Utalii, wakiwa katika chumba cha VIP Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, wakifuatilia mazungumzohayoKocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Salum Bausi na Rais wa ZFA Ravia Idarous Faina.    
Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Italia, Cesare Prandelli, akizungumza na Waziri wa Habari Utamaduni Utaliina Michezo Zanzibar Said AliMbarouk, alipowasili Zanzibar, wakiwa katika ukumbi wa VIP, akielezea jinsi ya kuisaidia Zanzibar katika nyanja ya Michezo  

Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar BMZ Shery Khamis akizungumza katika mkutano huo na kocha Mkuu wa timu ya Italia Cesare, katika ukumbi wa VIP Zanzibar alipowaili.




Kocha Bausi akibadilisha mawazo na Kocha wa Italia Cesare kuhusiana na timu ya Taifa ya Zanzibar maendeleo yake ikiwa na maandalizi ya kushiriki michuano ya Chalenji mwishoni mwa mwezi huu nchini Kenya.a


Kocha Bausi akisalimia na Kocha mwezake wa Timu ya Taifa ya Italia Cesare, alipowasili Zanzibar.


Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Italia Cesare, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar ZFA, alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, kutoka kushoto Kocha Mkuu ya Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes Salum Bausi, Kocha wa Italia Cesare, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Timu ya Taifa Hashim Salum, Mdau wa Michezo Zanzibar na Rais wa ZFA Ravia Idarous Faina.







No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.