Habari za Punde

Mchezo wa Kujipima Nguvu Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes




 Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Salum Bausi, akitowa maelekezo kwa wacheaji wake wakati wa mapumziko ya kipindi cha kwanza kumalizika, timu hiyoilikuwa ikiongoza kwa bao moja lililofungwa katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo.  
 Kocha wa timu ya Kijichi Seif Bausi akitowa maelekezo kwa wachezaji wake. wakati wa mapumziko ya kipindi chwa kwanza, timu yake ikiwa imeshalala kwa bao moja lililofungwa katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo wa kirafiki uliofanyika uwanja wa Mao.  



 Waandishi wa habari wakifuatilia mchezo wa kujipima nguvu kwa timu ya Taifa ya Zanzibar, ikicheza mchezo wa kirafiki na timu ya Kijichi, mchezo uliofanyika uwanja wa Mao. 
 Mchezaji wa timu ya Kijiji Saleh Mohammed akijiandaa kuzuiya mpira na huku beki wa timu ya Zanzibar Heroes, akijiandaa kumzuia. 
 MCHEZAJI wa timu ya Kijiji Khamis Kitwana (kushoto) akimpita beki wa timu ya Zanzibar Heroes Is-haka Othman wakati wa mchezo wa kujipima nguvu kwa timu ya taifa ya Zanzibar inayojiandaa kushiriki michuano ya Kombe la Chalenji inayotarajiwa kufanyika nchini Kenya , mchezo huo wa kirafiki umefanyika uwanja wa Mao,timu hiyo imeifunga Kijiji bao 1—0
Mshambuliaji wa timu ya Kijiji Mohammed Nassor, akijaribu kumpita beki wa timu ya Zanzibar Heroes katika mchezo wa kujipima nguvu kwa timu ya Taifa wa Zanzibar ikijiandaa kushiriki michuano ya Chalenji nchini Kenya mwezi huu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.