Msanii Khamis Fakhi akiwa na Tunzo yake ya Ubunifu baada ya kukabidhiwa na Afisi ya Msajili wa Hakimiliki Zanzibar kwa kuona Ubunifu wake wa Kazi mbalimbili, zilizoiletea sifa Zanzibar
Wasifu wa Msanii wa Uchoraji na Ubunifu wa Nembo mbalimbali ambazo amebuni Msanii Bwana Khamisi Fakhi Mohammed, ambaye amatunukiwa Tunzo ya Ubunifu na Afisi ya Mrajisi wa Hakimiliki Zanzibar katika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani Zanzibar.
Msanii Khamis Fakhi amechora Nembo mbalimbli na michoro, Alama, Herufi na hata rangi na aina za utambulisho wa kibiashara ama uendeshaji wa shughuli rasmin na hutofautisha baina ya shughuli moja ama taasisi moja na nyengine, Nembo ni alama inayotoa ujumbe juu ya shughuli za taasisi husika.
Taasisi nyingi za Umma ua hata za binafsi hapa Zanzibar tayari zina nembo zilizojipatia umaarufu kutokana na mvuto wa nembo hizo na hatimae kujenga uhusiano kati ya biashara au huduma na mteja.
Kwa maana hii Uchoraji wa nembo ni kazi ya ubunifu na usanifu wa hali ya juu, huhitaji kipaji na umakini wa kuwasilisha ujumbe kwa ana ufadsaha na michoro michache.
Nembo maarufu kwa hapa Zanzibar ni ile ya Serkali ya Mapinduzi Zanzibar. Wengi tunaweza kujiuliza ni nani aliyeibuni hii ya Kitaifa.
Mbunifu na Msanii wa michoro (Graphic Designer) atakayekumbukwa kwa kazi hiyo na nyengini zenye sifa hapa Zanzibar si Mwengine ila ni Bwana Khamis Fakhi Mohammed, ambaye ni mfanyakazi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) Yeye atakumbukwa katika historia ya Zanzibar si kwa kazi hii kuu ya Kitaifa bali pia kwa kazi nyingi nyengine zinazotoa taswira ya taasisi muhimu hapa nchini kwetu Zanzibar.
Katika majengo kadhaa na karatasi za barua au bahasha, nembo zinazotumika zinadhihirisha umuhiri wa Bwana Khamis Fakhi katika ubunifu na usanifu wake.
Baadhi ya kazi zake ni kama nembo zifuatazo.
Nembo ya Baraza la Wawakilishi, Nembo ya Serekali za Mitaa, Nembo ya Baraza la Sanaa, Nembo ya Baraza la Kiswahili, Nembo ya Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar (BMZ) na ya Baraza la Utafiti wa Afya.
Zaidi ya Mabaraza hayo Bw, Khamis Fakhi amesanifu kwa makini nembo za vyombo vyengine vya Serekali katika sekta ya Habari kama vile Sauti ya Tanzania Zanzibar (STZ),Tume ya Utangazaji na Chuo cha Uandishi wa Habari Zanzibar.
Kazi za Bwana Khamis Fakhi ni nyingi sana ambazo amebuni na kutumika kama alama ya Taasisi au Idara. amabuni pia Nembo ya Jitegemee Viwanda Vidogovidogo, Crown ya Kikosi cha KMKM, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, Huduma za Maktaba, Umoja wa Wauguzi na Wakunga Zanzibar, Kampuni ya Sigara ya Zanzibar, na Kalabu ya Muziki ya Culture.
Aidha amebuni, kusanifu na kuchora kanga za miaka arubaini ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye mchoro wa jengo la Chuo Kikuu cha SUZA Zanzibar na pia amechora mchoro wa kanga za millennia mwaka 2000 kuingia karne ya 21.
Umahiri wa Bwana Khamis Fakhi katika ubunifu huu nin kipaji alichobarikiwa na rabuka lakini pia na utaalamu aliopata katika kazi zake.Yeye alizaliwa mwaka 1959 huko Mkoani Pemba, alipata elimu yake ya msingi mwaka 1965 hadi 1971 hukohukomkoani Pemba.
.
Aliaza elimu ya sekondari katika mwaka 1972 hadi 1974 katika skuli ya Ngombeni mkoani Pemba na baadae kujiendeleza katika mafunzo ya Uchoraji kutoka kwa walimu wa Kijapani wakati akiwa kazini, katika mwaka 1988. Alijiendeleza na fani hiyo ya mafunzo ya kujiendeleza katika Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kigeni na kupata Cheti.
Pia Bwana Khamis Fakhi ni mwajiriwa wa Serekali ya Mapinduzi Zanzibar katika Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC , hadi sasa alikuwa ni mtangazaji katika vipindi mbalimbali na kusoma taarifa ya habari kupitia Redio Zanzibar na TV.
No comments:
Post a Comment