Habari za Punde

Nyota Njema Champion wakiwa katika shughuli za usafi wa mazingira Kundemba

Vijana wa Nyota njema wakiendelea na usafi

Hatari ya kujidunga na kutupa ovyo sindano za wateja
 


Kama unawakumbuka Vijana wadogo mtaa wa Kundemba uliopo Wilaya ya Mjini Unguja ambao ni miongoni mwa mitaa iliyoathirika sana na matumizi ya madawa ya kulevya waliamua kujikusanya pamoja na kujaribu kujiepusha na mazingira hatarishi yanayowakabili kwa kujibidiisha katika elimu na michezo.
 
Hapa wanaonekana wanajifunza pia umuhimu wa kujitolea katika kazi za kijamii pia (Community Services) kwa kufanya usafi wa mazingira wa sehemu ya mtaa wa Kundemba.
 
Kama umeguswa na jitihada za vijana hawa na uko tayari kuwasaidia utakachojaaliwa kufanikisha azma na jitihada zao hizi wasiliana na Mlezi wao Ummu Ahmad 0773 925313 au kupitia blog hii.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.