( حق المسلم على المسلم ست : إذا لقيته فسلم عليه ، و إذا دعاك
فأجبه ، و إذا استنصحك فانصح له ، و إذا عطس فحمد الله فشمته ، و إذا مرض فعُده ،
و إذا مات فاتبعه ) .
Kutoka kwa Abu Hurayrah, Allaah Amuwie radhi
amesema. Mtume Swalla Alaahu ‘alayhi Wasallam amesema:
Haki za muislamu
kwa muislamu mwenzake ni sita: Utakapokutana nae umsalimie, atakapokuita
umuitike, atakapokunasihi umsikilize nasiha zake, atakapoenda chafya umuombee
rehma ( yarhamuka Allaah – Allaah Akurehemu), atakapougua ukamkague (kwa kumtembelea
na kumjuulia hali) na atakapofariki umsindikize (kwa kwenda maziko yake).
Muslim
No comments:
Post a Comment