Habari za Punde

Rais Kikwete ameteua Nd Johari Masoud Sururu kuwa Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar

Picture: Johari Masoud Sururu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Johari Masoud Sururu kuwa Kamishna mpya wa Uhamiaji Zanzibar.


Kabla ya uteuzi huu ambao unaanzia tarehe 24 Novemba, 2013 Bwana Sururu alikuwa Mwambata wa Uhamiaji katika Ubalozi wa Tanzania jijini Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E).

Kufuatana na uteuzi huu, aliyekuwa Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar Bwana Mwinchumu Hassan Salim sasa atapangiwa kazi nyingine.

Imetolewa na:Isaac J. NantangaMSEMAJIWIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.