Habari za Punde

Balozi Seif Akutana na IGP na Mkuu wa Uhamiaji Zanzibar.

 Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Ernest Mangu akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyefika Ofisini kwake Baraza la Wawakilishi Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar kujitambulisha rasmi baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo.Kati kati yao kutoka kushoto ni Naibu IGP Kamanda Abdulrahman Omar Juma na Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdan Omar Makame.
  IGP Ernest Mangu akimuelezea Balozi Seif Mikakati ya Jeshi la polisi katika ulinzi wa raia na mali zao walipokutana katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar iliyopo Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif ali Iddi akiwa katika picha ya pamoja na kulia yake Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Ernest Mangu, kushoto ni Naibu wa IGP Kamanda Abdulrahman Omar Juma pamoja na Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdan Omar Makame.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Mkurugenzi mpya wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar Nd. Johari Masoud Sururu aliyefika Ofisini kwake Mbweni kujitambulisha rasmi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  Balozi Seif Ali Iddi akiagana na Mkurugenzi mpya wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar Nd. Johari Masoud Sururu baada ya kujitambulisha rasmi huko  Ofisini kwake Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.(Picha na Hassan Issa wa – OMPR)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.