Habari za Punde

Breaking Newssssss: Abiria 3 Waokolewa na Maiti 5 zapatikana Ajali ya Boti ya Kilimanjaro ikitokea Pemba.

Boti ya Kampuni ya Azam Marine ya Kilimanjaro  ikitokea Pemba asubuhi ya leo ikiwa na abiria karibu 320 imepata misukosuko ya hali ya upepo na mawimbi na kusababisha baadhi ya abiria waliokuwa wamekaa sehemu ya abiria ya mbele ya boti hiyo na kutumbukia baharini, kutoka na upepo huo.

Ajali hiyo imetokea katika mkondo wa Nungwi na baadhi ya abiria wa boti hiyo kuingia baharini kutokana na mawimbi na upepo uliokuwa ukivuma katika majira ya asubuhi ya leo na hali ya bahari kuchafuka ikiwa katika safari zake za kawaida ikitokea Pemba na kuelekea Unguja ilipata dosari kutokana na upepo na mawimbi katika maeneo ya Nungwi.

Juhudi za Wananchi na Vyombo husika kuchukua juhudi za uokoaji wa abiria hao na kufanikiwa kuwapata Wananchi watatu wakiwa hai na miili ya watu watano kupatikana mpaka sasa na zoezi la uokowaji linaendele kufanyika katika eneo la tukio  la bahari ya Nungwi. 

Maiti zilizopatikana katika zoezi hili ni 5, na mbili ni za Wanawake na tatu za Wanaume.

Zoezi hilo limesitishwa hadi keshoasubuhi.
 

12 comments:

  1. Innalillahi wainna ilayhi rajiuun. Hawa viongozi wa serikali ya Zanzibar wote vichwa maji, baada ya kututafitia meli ya kujulikana wanatujengea mnara wa kuadhimisha miaka 50 ya mapinduzi. Huu ni ujinga wa hali ya juu yaani serikali isioyojali wananchi wake, ni sawa na mama kutomjali mwanawe!!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. sasa kwani serikali ndio imeleta upepo.... usimkufuru mungu ukisema innalillahi basi imetosha kwani hata ingekua meli la chuma kama mungu ameandika ajali itokee ingetokea tu

      Delete
    2. Inallilahi waina ilayhi rajiuun..tusiilaumu sana serikali kwani mbele ya Mwenyezi Mungu haina upinzani kwani kama ajali yaeza tokea mda wowote na pahala popote...

      Delete
    3. hii ni dalili ya upumbavu kusingizia serikali kila kitu. Wewe siasa imeharibu ubongo wako. MKUMBUKE MUNGU WAKO.

      Delete
  2. Nahoza wa boat ni mzembe pamoja na mabaharia wake, haiwezekani abiria wadondoke baharini huku wakijua kwamba hali ya upepo isingeweza kuruhusu abiria hao kukaa sehemu ya wazi, halafu la kusikitisha zaidi serikali ilipojaribu kuwasiliana na nahoza wa chombo ili kama kuna watu waliopata madhara yeyote ufanyike utaratibu wa kupelekwa boat za uokozi, nahoza alijibu abiria wote wako salama, hivi tunajiuliza nahoza huyo alikuwa hajui kwamba sehemu ya juu ya wazi iliokuwepo sehemu ya mbele huwa wanakaa abiria? hata hao mabaharia (wafanyakazi) wanaohudumia abiria wao pia hawakulijua hili? ule utaratibu wa kuwapitia abiria na kuwasikiliza matatizo yao tuseme ndio haufanyiki siku hizi mpaka inatokezea ajali na nahoza anasema hakujua kama kulikuwa na abiria sehemu hiyo, ajali zote hizo zilizotokea hivi karibuni bado tu hakuna funzo lolote lililopatikana? bila kubana meno ni lazima vyombo vya sheria vifanye kazi na wamilki wa boat za usafiri ni lazima waangalie uwezo wa wafanyakazi wao, jamani kifo ni lazima lakin uzembe wa baadhi ya watu isiwe sababu ya vifo vyetu.

    ReplyDelete
  3. innalillah wainna ilaih rajuun

    ReplyDelete
  4. Hilo ni kweli kazi ya mungu haingiliwi. huo ni uwezo wake 2

    ReplyDelete
  5. Allah awasameh madhambi yao na inshallah awalaze mahali pema peponi amin.

    ReplyDelete
  6. @ Anonymous wa 4..Nakuunga mkono 100% Uzembe unaotokea katika Vyombo vya Baharini, angani na Barabarani visiwe Visingizio Vya Vifo vya Wananchi wanyonge... Muliobakia nyote Ni wajinga wakubwa..Mungu mungu..Ndio Mungu yupo lakini huu ni Uzembe uliopita na Wacheni Uyakheee Wenu huo..

    Ndiomaana nyinyio Walipokuja Watanganyika pale Unguja kwasababu tu wamevaa Nguo za Kijani muliwakumbatia na mukawaona ni Nduguzenu..hivi Sasa kutoka Matemwe hadi Nungwi ni watanganyika tu ndio waliohamia nakueneza ukimwi kila kona..baadae mukamlilia samia Suluhu ati Kisiwa Cheni kimevamiwa hamuna pakuzikana...Sio Nyinyi Ni Mayakheee fedha munaziona bola kuliko Pahala pakusitilika... ..Maeneo yote ya Unguja mumewauzia Wataliano halafu wanawaletea Cocain na kuwaharibu wototo wenu... Nani anafaidika na utalii hapo unguja.. Ni bora hata hao wapemba alivokataa kuharibiwa visiwa vyao..Sasa unawauwa mmoja mmoja kwakisingizio cha Mungu... Aithee Kweli Nyinyi ni Mabwege.. hio Selikali ya Mkataba ndio mutaiweza kweri..? Boshirt.. Wasenge nyinyi...

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ndugu yangu ustaarabu haununuliwi. Mimi ni mbara lakini sijafurahishwa la lugha ulizo tumia hapa. Maneno ya uchochezi na matusi yanakusaidia nini? Wewe una uhakika gani kama huna ukimwi au una dhani kuwanyanyapaa walio athirika ndio kutakufanya wewe uwe salama? Jaribu kushirikisha ubongo wako unapo toa maoni yako.

      Delete
  7. Jamaini matusi hayafai, kunyamaza ni zahabu kama hunalakusema, sisi wadau tumepata tabu kuutangaza humtandao, na sikunyingi huyumdau, hazitawi, comment, zetu kwa sababu ya hawa wzembe wanao shindwa hoja na kuibka na matusi, tukosoeni kwa hoja, sio jaziba

    ReplyDelete
  8. wambieni wajinga hao wasiojua kusema ilimradi tu mtu aandike, acheni kutukana ovyo si ustaarabu wala si kujua kusema

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.