Na Mwandishi wetu
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete
amemjulia hali Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Haroun Ali Suleiman, anaepatiwa
matibabu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Rais Kikwete alifanya ziara hiyo juzi akiambatana na mkewe, mama Salma
Kikwete.
Aidha Rais Kikwete alimtembelea na kumkagua Waziri Mkuu Mstaafu, mzee
Cleopa David Msuya aliyelazwa hospitali hiyo akiendelea na matibabu.
Ziara kama hiyo imefanywa na
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib
Bilal.
Awali Dk. Bilal akiambatana na mkewe mama Zakia Bilal alimtembela mzee
Msuya, aliyelazwa hospitalini hapo na baadae alimjulia hali Waziri Haroun.
Januari 13, Rais Kikwete alimtembela kumjulia hali
Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Salmin Amour nyumbani kwake Migombani
No comments:
Post a Comment