Habari za Punde

Khitma ya Kidishi kesho Msikiti wa Miembenni


Viongozi, wachezaji wa zamani na wanachama wa Black Fighters unawatangazia khitma ya mchezaji wao wa zamani na mwanachama wao Maulid Hamid Abdullah (Kidishi) itakayosomwa kesho baada ya sala ya Laasir msikiti wa Miembeni Zanzibar.

Nyote tunakaribishwa ili kumuombea dua mwenzetu, ALLAH amsamehe makosa yake na amkubalie dua na ibada zake pamoja na zile zetu tutakazoomba kwa niaba yake na awemo kwenye waja watakaopewa malazi mema peponi AAMEEN.

Ahsanteni wote

5 comments:

  1. Allahumma firlahu warhamhu fil janah

    ReplyDelete
  2. Allahumma ighfir lahu warham huu, yaa rabbil aalamyn.
    Ila naomba kuuliza tu, huyu kidishi ni yupi kidigi kumbukumbu zimenitoka, mimi ninavyokumbuka Kidishi alikuwa akichezea Small Simba ndile huyo aliefariki (ingawa yule akiitwa JUma Bakari Kidishi) au kulikuwa na Kidishi mwengine??
    Naomba tujulisheni. Alla amsamehe kwa kila aliloteleza, na ampokee kwa wema amiin.

    ReplyDelete
  3. MOla amlaze peponi amiin. Naomba kuuliza, huyu ni yule kidishi aliyewahi kucheza Small simba au vipi, ingawa yule nakumbuka akiitwa Juma Bakari Kidishi???

    ReplyDelete
  4. Bin Shaaban et al.
    Aliefariki anaitwa Maulid Hamid Abdullah alikuwa anachezea Black Fighters na alikuwa akiishi Miembeni kabla mpira wake haujaexpire na akakimbilia ughaibuni ambako ndiko alikofia. Kidishi huyu ndio mwenye jina hasa la Kidishi na hawa wengine wote wanafananizwa nae kiuchezaji. Kidishi huyu miaka hiyo alicheza na akina Bausi, Maya, Wahid, Bwanga na Kocha wao alikuwa Malick. Samahani sana kuwa tulisahau kushare picha yake on the blog

    ReplyDelete
  5. Thankx mdau kwa taarifa na ufafanuzi, kungekuwa na picha ingesaidia kidogo, hata hivyi shukran

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.