MAADHIMISHO
YA MIAKA 50 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR
MRADI WA KUTOA MIKOPO KWA WAJASIRIAMALI
WADOGO (SELF) NA MKAKATI WA KUPUNGUZA
UMASIKINI WA KIPATO:
Ø SELF ni Mradi wa kutoa mikopo kwa wajasiriamali
wadogo kupitia asasi ndogo na za kati za fedha.
Ø SELF yatimiza miaka 13 ya huduma ya
kutokomeza umasikini nchini.
Ø SELF yaeleza mikakati yake, mafanikio na
changamoto
Tangu mwaka 1961 Serikali
ya Tanzania
imekuwa inapambana dhidi ya maadui watatu wa maendeleo yaani; ujinga, maradhi
na umasikini. Aidha, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, Malengo ya Maendeleo ya
Milenia na MKUKUTA na MKUZA; inaainishwa changamoto za kuyapata maendeleo na
haja ya kuweka vipaumbele. Wakati tukiadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar,12 January 2014, changamoto
kubwa inayoikabili Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kama ilivyo kwa serikali
nyingine katika nchi zinazoendelea, ni jinsi ya kutekeleza mipango ya
kuwawezesha wananchi wengi zaidi kushiriki kikamilifu katika shughuli kukuza
uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na hatimaye nchi nzima; ili waweze kuwa na
maisha ya viwango vya kuridhisha na kustahimilika kama vilivyoanishwa katika Malengo ya Milenia.
Mpango wa Kukuza Uchumi na
Kupunguza Umasikini Zanzibar
(MKUZA),umeandaliwa katika nguzo kuu tatu.
Nguzo ya kwanza ni ‘’Ukuaji wa Uchumi na Kupunguza Umaskini wa Kipato.’’ Nguzo
hii inaunganishwa kwa karibu na nguzo ya pili ya ‘’Kuimarisha Ubora wa Maisha
na Ustawi wa Jamii’’, na nguzo ya tatu ni ‘’Utawala Bora na Uwajibikaji’’
ambayo ni msingi muhimu wa nguzo mbili zilizotangulia.
Serikali inatambua kwamba
umasikini wa kipato ni chanzo na/au kichocheo cha maradhi na ujinga katika
jamii, ndiyo maana juhudi za dhati zinahitajika ili kuhakikisha kuwa, sambamba
na kupatikana kwa mahitaji ya msingi; chakula, mavazi na makazi, suala la
kuwawezesha wananchi kijikwamua wao wenyewe kiuchumi, ni la msingi kabisa; hasa
ikizingatiwa kwamba uwezo wa Serikali pia una ukomo kutokana na upungufu wa
rasilimali. Hivyo Serikali inatakiwa iandae mazingira mazuri ya kutekeleza
MKUKUTA na MKUZA; yanayoshirikisha jamii kubwa katika masuala ya kiuchumi.
Ndani ya MKUKUTA na MKUZA, imeainishwa miradi na programu mbalimbali kusaidia
Watanzania na hasa wale wa kipato cha chini mijini na vijijini waweze kujiajiri
na kuongeza vipato. Mradi wa SELF ni miongoni mwa miradi iliyoanzishwa, kwa
lengo hili.
Mradi
wa kutoa Mikopo kwa wajasiriamali wadogo (SELF ), ni Mradi wa kutoa mikopo kwa
Asasi ndogo za kifedha ili hatimaye asasi hizo ziweze kutoa mikopo hiyo kwa wananchi wajasiriamali wenye kipato kidogo waliopo mijini
na vijijini.
Lengo
kuu la Mradi ni kukuza na kuboresha upatikanaji wa huduma za kifedha, hivyo
kuwapa fursa ya kushiriki katika shughuli za uzalishaji mali kwa lengo la kujiongezea
kipato ili kuondokana na umaskini. Ili kufikia
lengo hili, Mradi wa SELF unatekeleza shughuli zifuatazo:
1.
Utoaji wa mikopo kwa Asasi za kifedha kwa
lengo la kuwakopesha walengwa wa mradi wa SELF:
Ukiwa ni mradi
uliojizatiti kikamilifu kuwapa watu masikini fursa ya kuwa na uchaguzi katika
kujipangia maendeleo yao, kupambana na umasikini, na kujenga msingi bora na
imara ya vyanzo vya mapato kwa ajili ya mahitaji yao ya kila siku; SELF –
inatoa mikopo kwa Asasi za kifedha (Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGOs),
Vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS), Kampuni zinazotoa mikopo (Microfinance
Companies), Jumuia za kijamii (CBOs), Benki za wananchi za maendeleo (Community
Banks) ambazo nazo hutoa mikopo kwa walengwa ambao ni Wanawake,Vijana,Walemavu
wake kwa waume, Wakulima na Wajasiriamali wadogo wadogo. Mikopo hii inatolewa
katika kiwango cha riba nafuu; kiwango ambacho kitaziwezesha Asasi za kifedha
kutoa mikopo kwa walengwa wanaofanya shughuli za uzalishaji mali katika sekta rasmi na isiyo
rasmi huku wakimudu gharama zao za uendeshaji. Mikopo hii inatolewa tu kwa zile
Asasi za kifedha zenye uwezo na sifa nzuri katika kusimamia utoaji wa mikopo
kwa kufuata taratibu bora na sahihi za usimamizi wa fedha.
2.
Kujenga Uwezo: Katika kuhakikisha kuwa yanakuwepo
mazingira mazuri yanayo shajiisha kuwepo kwa huduma endelevu za kuweka na
kukopa, SELF imetenga fedha kwa shughuli zifuatazo:
Ø
Kuendeleza
Kada ya Wafanyakazi: SELF imejizatiti katika kutoa mafunzo kwa mujibu wa
tathmini ya mahitaji ya mafunzo kwa wafanyakazi na viongozi wa asasi wabia wa
mradi kwa Kada zifuatazo:
·
Wajumbe
wa bodi, kamati za mikopo na usimamizi wa fedha, maafisa mikopo pamoja na
makarani.
·
Wajasiriamali
wadogo walengwa wa mradi ambao ni wabia wa asasi za fedha zinazoshirikiana na Mradi.
·
Maafisa ushirika.
Ø
Kuandaa
kada ya Wakufunzi na utayarishaji wa mitaala inayotumika kufundishia.
Ø
Kusaidia
ukarabati wa majengo ya ofisi na vitendea kazi pamoja na samani za ofisini kwa
asasi wabia wa mradi
3.
Uhamasishaji na Ufuataliaji: Ukiwa
kama kielelezo cha jitihada za mwanadamu na matarajio yake katika mapambano
dhidi ya umaskini uliokithiri, mradi wa SELF umeandaa kampeni mbalimbali kwa
lengo la kuuelimisha umma kuhusu shughuli za mradi na kutoa hamasa kwa wananchi
ili waweze kuelewa umuhimu wa kujiajiri, kujipatia mikopo na kuirejesha mikopo
kwa wakati na kwa faida ya wote. Aidha ufuatiliaji na tathmini ya mara kwa mara
ya shughuli za mradi ni nguzo kuu katika kujua maendeleo yake kwa ajili ya
ufanisi.
Mradi
huu ulianza kutekelezwa mwaka 1999/2000, ni Mradi uliobuniwa na Serikali na
kufadhiliwa na Serikali ya Tanzania
na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), ili kutoa huduma zilizo endelevu za
kifedha kwa jamii ambayo ilikuwa haijafikiwa na huduma rasmi za kifedha
hususani jamii za vijijini.
Serikali
ilikusudia kutumia fedha hizi, kuanzisha mfuko ambao utatoa mikopo yenye
masharti nafuu kwa wananchi kupitia Asasi za Kifedha. Eneo la mwanzo la
shughuli za Mradi wa SELF ilikuwa kwenye mikoa 6 yaTanzania bara, ambayo wakati
huo ilibainika kuwa nyuma kimaendeleo na kwenye mikoa 5 ya Tanzania visiwani. Mikoa hiyo
ilikuwa ni Mtwara, Lindi, Pwani, Dodoma , Singida na Dodoma .
Mnamo mwaka 2004/05, Serikali iliongeza eneo la Mradi wa SELF kufikia mikoa 14
ya Tanzania Bara. Mikoa mipya iliyoongezwa ilikuwa Mwanza, Mara, Ruvuma , Mbeya, Iringa, Tanga, Kilimanjaro na Arusha.
Awamu
ya kwanza ya utekelezaji wa Mradi wa SELF ilikwisha mwaka 2007. Hata hivyo
kutokana na mahitaji makubwa ya huduma za kifedha yaliyoibuliwa na Mradi,
Serikali bila ufadhili wa nje iliendelea kugharamia shughuli za Mradi, husasani
uendeshaji. Mchango huu toka Serkalini pamoja na mapato ya ndani ya Mradi
yaliwezesha SELF kuendelea kutekeleza shughuli zake kwa ufanisi mkubwa na mwaka
2009 mikoa 7 iliyokuwa imebaki kwa upande wa Tanzania Bara iliongezwa kwenye
eneo la Mradi. Mikoa iliyoongezwa ilikuwa ni Manyara, Shinyanga, Tabora,
Kagera, Kigoma, Rukwa na Dar es Salaam .
Hivyo Mradi wa SELF ukawa unatekelezwa, mikoa yote ya Tanzania Bara na
Visiwani.
Mradi wa SELF umekuwa makini kutekeleza kwa vitendo majukumu
yake kwa ufanisi mkubwa ili kutimiza malengo
ya kuanzishwa kwake. Hali hii imechangiwa na jitihada za makusudi za
SELF zilizofanywa katika kuutangaza Mradi, kuzihamasisha Asasi ndogo na za Kati
za Fedha kuchukua mikopo yenye masharti nafuuu na kuzifanya ziwe na fikira ya
kutoa huduma iliyo endelevu kwa kujenga uwezo wa kiutendaji kupitia mafunzo
yanayotolewa na wataalamu waliobobea katika masuala ya uendeshaji na usimamizi
wa fedha. Aidha vitendea kazi vinavyotolewa na Mradi vimekuwa ni motisha kwao ya kutoa huduma vizuri na
kuboresha utendaji.
Leo hii SELF sio tu kwamba
imekuwa ya kupigiwa mfano kutokana na sera zake zinazolenga kuleta maendeleo
kwa watu maskini, bali pia kwa mafanikio iliyoyapata ambayo yanaifanya iwe
mfano wa kuigwa miongoni mwa miradi inayosimamiwa na Serikali
inayojishughulisha na utoaji wa huduma za Kifedha, pale ambapo taasisi rasmi,
yaani Benki za biashara zimeshindwa kukidhi mahitaji kutokana na sera, sheria
na taratibu za kibenki. Kimataifa SELF imejijengea umaarufu kutokana na kushika
nafasi ya juu miongoni mwa miradi ya aina hii, inayofadhiliwa na Benki ya
Maendeleo ya Afrika (AfDB).
Uzoefu na mafanikio yaliyopatikana katika awamu ya kwanza ya mradi
yameiwezesha SELF kuingia katika awamu ya pili ya utekelezaji iliyoanza Julai
2010 na itamalizika Juni 2015. Katika awamu hii ya pili ya utekelezaji,
Serikali inakusudia kuibadilisha SELF kutoka kuwa Mradi na kuwa taasisi
inayojitegemea.
Katika
kipindi cha miaka kumi na mitatu iliyopita, utoaji mikopo unaofanywa na SELF
kwa Asasi za Fedha umepanda kwa kasi na kuweza kuwafikia wananchi wengi wa
kipato cha chini waliopo mjini na vijijini kama inavyoonyeshwa kwenye jedwali
hapo chini.
Kupanuka
kwa Huduma za Kifedha Vijijini na Mjini
Mwaka
|
02/03
|
03/04
|
04/05
|
05/06
|
06/07
|
07/08
|
08/09
|
09/10
|
10/11
|
11/12
|
12/13
|
1.Idadi
ya Asasi za Kifedha
|
21
|
39
|
70
|
71
|
56
|
186
|
155
|
203
|
301
|
323
|
364
|
2.
Thamani ya mikopo kwa Asasi ‘’Tshs 000’’)
|
665,450
|
1,513
|
3,465
|
2,733
|
3,769
|
3,283
|
5,752
|
6,859
|
9,014
|
10,248
|
9,843
|
3.
Idadi ya wananchi waliokopeshwa
|
7,083
|
12,325
|
20,526
|
37,364
|
54,058
|
60,016
|
65,809
|
73,025
|
80,454
|
88,083
|
93,364
|
4.
Jamii iliyonufaika
|
28,332
|
49,300
|
82,104
|
149,456
|
216,232
|
240,064
|
263,236
|
292,100
|
321,816
|
352,332
|
374,560
|
Hadi
kufikia Juni 2013 tayari SELF ilikuwa imeshatoa mikopo yenye thamani ya bilioni
52.3 kwa asasi za kifedha zipatazo 364 (asilimia 60 kati ya hizo ni za
vijijini). Mikopo hii imesaidia kukuza shughuli ndogo
za kiuchumi na kunufaisha zaidi ya wateja wapatao 93,372 ambao kati ya
hao 58% ni wanawake. Aidha, watu wapatao 374,560 kwa njia moja au nyingine
wamenufaika na mikopo hii.
Mafunzo
yanayotolewa na Mradi wa SELF kwa viongozi na watendaji wa asasi ndogo na za
kati za fedha yanalenga kuwajengea uwezo juu ya utawala bora,usimamizi wa
shughli za fedha na mikopo. Wajasiriamali wadogo wanaokopa toka asasi wabia wa
SELF nao pia hupatiwa mafunzo ya ujasiriamali na stadi za biashara. Mafunzo
haya yanalenga kuwaongezea ujasiri wa kuthubutu na kuongeza ubunifu katika
biashara zao ili waweze kuwekeza vizuri kwenye mikopo wanayoipata kwa kuifanyia
biashara kwa njia za kitaalamu zitakazo waongezea tija kwenye biashara zao.
Jedwali
lifuatalo linaonyesha idadi ya wabia wa mradi walionufaika na mafunzo toka
Mradi mradi ulipoanza hadi kufikia Juni 2013.
Idadi
ya Viongozi, Watendaji wa Asasi za kifedha, Wajasiriamali wadogo na Watoa
Huduma walionufaika na Mafunzo toka SELF.
Kundi
|
2000
- 2009
|
2010
- 2013
|
Jumla
|
Viongozi
na Watendaji wa Asasi za kifedha
|
2,486
|
1,042
|
2,551
|
Wajasiriamali
wadogo
|
3,175
|
4,558
|
5,649
|
Watoa
huduma (Maafisa Ushirika ngazi ya wilaya)
|
208
|
180
|
240
|
Mradi
wa SELF umekuwa ukihakikisha huduma za fedha zinazotolewa zinakuwa endelevu kwa
wabia wake, ili wananchi wengi zaidi hasa maeneo ya vijijini waweze kunufaika
na huduma za kifedha. Mradi wa SELF umekuwa ukihamasisha wabia wake kutoa
huduma katika mazingira yaliyo bora, salama na yenye mvuto, ili wananchi wengi waweze
kuhamasika na kujiunga kwenye huduma za kifedha.
Hadi
kufikia mwezi June 2013, Mradi wa SELF tayari ulikuwa umetoa jumla ya T.sh. 75,374
milioni kwa asasi za fedha 68 inazoshirikiana nazo katika kuhakikisha huduma
za kifedha zinawafikia wananchi kwa wingi zaidi, katika mazingira yaliyo salama
na kisasa zaidi. Kiasi hicho kimeziwezesha asasi hizo kununua samani za ofisi, vitendea
kazi kama vile kompyuta, mashine za kudurufu na kusikani karatasi, pikipiki,
kasiki, baiskeli, kukarabati majengo pamoja na kuandaa mikutanao kwa ajili ya wanachama
wao.
Mikopo inayotolewa kwa wabia wake pamoja na vitendea
kazi vya ofisi wanavyopewa wabia wa SELF, umezifanya asasi hizi kuongeza ufanisi
na kuimarisha utoaji huduma kawa katika viwango bora kabisa, na kuzifanya asasi
hizo ziweze kukua toka kwenye kiwango cha chini cha utoaji huduma hadi kwenye kiwango
cha kati, na zile asasi za fedha zilizo kuwa kwenye kiwango cha kati kukua na kufikia
kiwango cha juu cha utoaji huduma.
Hadi kufikia mwezi June 2013, asilimia 12 ya
wadau wanaoshirikiana na Mradi, wameweza kukua toka kiwango cha chini kabisa
cha utoaji huduma hadi kiwango cha kati, wakati asilimia 3.4 ya asasi za fedha
zilizo kwenye kiwango cha kati zimeweza kufikia kiwango cha juu kabisa cha
utoaji huduma za mikopo. Asilimia 31 ya wadau wa kiwango cha chini, waliweza
kuimarisha huduma zao ndani ya kiwango hicho na kuanza kutoa huduma bora zaidi
kwa wanachama wake. Kukua huku ni muhimu, ili kuibua Asasi za kifedha
endelelevu ambazo zitaendelea kutoa huduma bora za kifedha kwa jamii na hivyo
kukuza uchumi na kuboresha maendeleo ya jamii nzima.
Akizungumza
katika moja ya mafunzo ya kuwajengea uwezo Warajisi Wasaidizi na Maafisa
Ushirika wa Mikoa ya Tanzania bara na visiwani, Katibu tawala wa Mkoa wa Pwani
Ms. Beatha Swai, aliwataka Maafisa ushirika wa mikoa yote waongeze bidii katika
kuwaelimisha viongozi wa SACCOS ili waweze kuzifahamu sheria za ushirika vizuri,
hivyo kuweza kuimarisha utendaji na usimamizi wao wa kazi. “ Mnatakiwa msimamie vizuri Sheria ya Ushirika kwa viongozi wa SACCOS kwa
kufuata misingi na kanuni za ushirika, ili kuongeza uelewa kwa viongozi wa SACCOs ili waweze kusimamia shughuli zao vizuri”
Bw. Abdulhaman
Mohamed Hassani, ambaye ni Katibu Mkuu wa taasisi ya kutoa mikopo ya Jumuiya ya
Changamoto ya Unguja (Changamoto Life Preservation Fund), iliyoanzishwa kwa
lengo la kutoa huduma mbalimbali kwa jamii ya Saateni na maeneo yanayozunguka;
anasema kwamba; awali taasisi ilisajiliwa kama chama cha kuweka akiba na kukopa
(SACCOS). Lakini kufuatia utendaji mzuri na uhitaji mkubwa wa huduma za kifedha
uliokuwepo , uongozi uliamua kuongeza wigo wa kutoa huduma na kuamua kubadilisha
usajili wa SACCOS, na kuwa chama cha kijamii mwaka 2007. Anasema Mradi wa SELF
umeweza kukidhi mahitaji ya asasi yao kwa kuongeza mtaji kupitia mikopo wanayoichukua
SELF. Anaendelea “…..kutokana na
kuongozeka kwa mtaji tumekuwa tukitoa mikopo kwa wakati kwa wanachama wengi zaidi
tofauti na hapo awali, hivyo kuwafanya wanachama wetu kufanya biashara kwa
uhakika zaidi kwa kujiamini. Ajira 2,700 zimeweza kupatikana baada ya wajasiriamali
kuweza kupanua biashara zao”
Bw. Abdulhaman
Mohamed Hassani anaelezea jinsi mafunzo yaliyotolewa na Mradi wa SELF kwa viongozi,
na wajasiriamali wa asasi yao, yalivyoboresha na kuongeza ufanisi wa utendaji
kwa viongozi na kuwafanya kuongeza nidhamu ya fedha, kitu kilichokuwa kikwazo kikubwa katika usimamizi wa asasi yao
hapo awali, “……kwa upande wa wajasiriamali,
mafunzo ya ujasiriamali
kuhusu stadi za biashara, usimamizi wa biashara na elimu ya ujasiriamali, yamewaongezea
ujasiri mkubwa wa kuthubutu na kuwa wabunifu katika biashara, hali inayowafanya
waweze kusimamia biashara zao kwa kujiamini”
“Vile vile
SELF imetusaidia kukarabati ofisi yetu, imekuwa ya kisasa na kuvutia zaidi; hali
inayotufanya tuaminike na kutambulika kwa wadau wengi zaidi. Nawashauri wananchi
wajiunge kwa wingi kwenye taasisi za kifedha, ili waweze kunufaika na mikopo ya
masharti nafuu, ni vigumu kufikiwa na huduma
za kifedha kwa mtu mmoja mmoja’’, anasema Bw. Abdulhaman Mohamed Hassani.
Bw. Ally Adam
Ally ni Mwenyekiti wa Serena SACCOS, ambayo imekuwa miongoni mwa wanufaikaji wa
huduma za fedha toka Mradi wa SELF. Yeye anasema, katika maeneo yote ambako SELF
imewafikia wananchi, imekuwa mkombozi mkubwa kwao hasa kutokana na kutoa mikopo
yenye masharti na riba nafuu inayowawezesha watu wa kipato cha chini kuimudu.
Anasema tofauti na asasi
nyingine za kifedha kama benki na kampuni binafsi ambazo huweka masharti magumu
yanayohitaji dhamana, SELF imejidhirisha kuwa tofauti kabisa na asasi hizo.
“Tumeweza kuboresha maisha
yetu tofauti na awali, kupitia mikopo ya SACCOS yetu, tumeweza kuboresha maisha
yetu, tumenunua vyombo vya moto kama pikipiki, magari na kuboresha makazi yetu
kwa kupitia mikopo, vilevile ada za watoto na zetu sisi wenyewe zimekuwa zinapatika
kwa urahisi sana tofauti na awali”, anasema Mwenyekiti Ally Adam Ally.
Akizungumza na Majira
katika mahojiano maalum, Meneja wa Mradi wa SELF Bw. Abiah Kaaya, anasema
pamoja na mafanikio ambayo SELF imeyapata katika kipindi cha takribani miaka
kumi na tatu tangu kuanza huduma zake, bado kumekuwa na changamoto mbalimbali
ambazo zimekuwa kikwazo katika kutekeleza na kutimiza malengo ya Mradi wa SELF.
‘’Utoaji
wa huduma za Kifedha kwa wananchi wa kipato cha chini ni dhana iliyoshamiri miaka
ya karibuni hapa Tanzania; Asasi zinazofanya shughuli hii zimejikita zaidi
mijini na kwenye maeneo yenye shughuli kubwa za kipato. Aidha upatikanaji wa
huduma hizi katika maeneo ya vijijini umekuwa bado uko katika kiwango cha chini,
ambapo huwa ukifanyika kwa utaratibu ambao si rasmi kutokana na kutokuwepo kwa Asasi
zinazotambulika kisheria.
Aidha,
kwenye maeneo ambayo kuna Asasi za kifedha
zinazotoa huduma, kutokana na udhaifu wa kiutendaji, hususan upungufu wa
wafanyakazi wenye ujuzi utoaji wa huduma ni duni na hazikidhi matakwa ya
walengwa. Wafanyakazi wenye ujuzi mdogo wamelazimika kuwa na majukumu mengi kwa
wakati mmoja tofauti kabisa na uwezo wao, utawakuta wakati mwingine wakifanya kazi kama Mameneja, Maafisa
Mikopo na Wahasibu. Katika utendaji kazi wa aina hii, udhibiti na utunzaji wa
fedha umekuwa tatizo kubwa; ni dhahiri kabisa kwa asasi za aina hii kukabiliwa
na hatari kubwa ya kushindwa kutoa huduma zilizo endelevu kwa sababu ya zisizoridhisha
zitolewazo na wafanyakazi wasio na uzoefu, hali hii inapelekea kupoteza pesa’’, anaeleza Meneja wa Mradi.
Anaeleza kuwa changamoto nyingine
inayozikabili Asasi za kifedha ni wananchi kuwa na uelewa mdogo juu ya masuala
kifedha, yahusuyo mikopo, akiba, riba n.k.; hivyo kushindwa kutoa maamuzi
sahihi kuhusu dhana nzima ya matumizi ya akiba na mikopo, ili kuongezea kipato
na hivyo kujikwamua kiuchumi. Aidha, mapungufu ya elimu hii, inafanya wananchi
kushindwa kufanya tathmini ya fursa zilizopo ili kuzitumia vizuri kwa manufaa
yao. Kuondokana na changomoto hii, Meneja wa Mradi wa SELF anashauri asasi za
fedha ziwe zinatoa elimu kwa wateja, wanachama na wananchi, ili waweze kuwa na uelewa
mkubwa wa namna ya kutumia mikopo hiyo vizuri na kuwafanya wafanye shughuli kwa
malengo na mitizamo iliyo endelevu. Kwa upande wa viongozi wa asasi za fedha,
baadhi yao wamekuwa na uelewa mdogo wa masula ya kifedha, hali inayowafanya washindwe
kubuni vyanzo vingine vya mapato vilivyo imara na kutegemea zaidi vyanzo
vilivyopo tu. Viongozi na watendaji hawana budi kuelewa kuwa kuendelea kuwepo kwa
asasi zao kutategemea zaidi uwezo wao wa kubuni mikakati itakayoziwezesha Asasi
za fedha kuwa endelevu. Mikakati hiyo ni pamoja na kupanua wigo wa eneo na
huduma wanazotoa, kubuni vyanzo vipya vya mapato, kudhibiti gharama za
uendeshaji, kuboresha urejeshwaji wa mikopo na kudumisha uongozi bora.
Anaendelea
kueleza kuwa, tabia na mawazo potovu yatokanayo na mila na desturi kuhusu mikopo,
hasa ile itolewayo na Serikali imekuwa changamoto kubwa inayofanya viwango vilichokusudiwa
na Serikali, vya kuifikishia mikopo jamii pale ilipo hasa sehemu za vijijini,
visifikiwe. Vilevile kuna desturi kwa baadhi ya jamii kuona mikopo kama chombo
kinachodhalilisha au chombo kinachotumika kuwakandamiza na kuwarudisha nyuma
kimaendeleo, pindi wanaposhindwa kulipa mikopo kwa wakati.
Utawala
mbovu wa baadhi ya viongozi wa Asasi za kifedha, ambao umekuwa hauzingatii misingi
ya utawala bora, usiofuata utaratibu uliowekwa wakati wa uchaguzi na usio
zingatia huru na haki kwa viongozi wengine umekuwa changamoto kubwa ya
kuhakikisha huduma za kifedha zinatolewa katika mzingira huru na ya haki. Viongozi
wamekuwa wakiingilia kazi za meneja na kuwafanya wafanye kazi katika mazingira magumu,
yasio huru hivyo kushindwa kusimamia majukumu yao vizuri, hiyo ni mojawapo ya
changomoto zinazoelezwa na Meneja, kwa asasi za fedha.
Anataja changamoto nyingine inayozikabili Asasi
za kifedha kuwa ni kutumiwa vibaya fursa ya kuwepo kwa taasisi mbalimbali
zinazotoa mikopo. ‘Lipo tatizo kwa baadhi ya Asasi za fedha kutumia vibaya
fursa ya kuwepo kwa taasisi nyingi zinazotoa mikopo kwa kuchukua mikopo mingi kwa wakati mmoja toka
kwa wakopeshaji tofauti kuliko uwezo wake wa kuitumia na kuisimamia, hivyo kuwa
na mikopo mingi isiyolipika hali ambayo inapunguza ufanisi na uendelevu wa
asasi hizo’’. Anasema juhudi za Serikali za kuhakikisha kuwa kila mwananchi
anapewa kitambulisho cha utaifa, ambazo zinaendelea sasa, pamoja na kuanzishwa chombo
kitakachokusanya taarifa za wakopaji (credit bureau), vitatoa ufumbuzi wa tatizo
hili; kwa sehemu kubwa.
Meneja
wa Mradi wa SELF, anawashauri wananchi waache kuwa na mawazo potofu, na wajiunge
kwa wingi kwenye asisi za fedha zinazotoa mikopo yenye riba nafuu, ili waweze
kunufaike na mikopo hiyo kuwafanya washiriki kikamilifu katika shughuli za
uzalishajimali, na kuongeza vipato miongoni mwao na kutengeneza ajira nyingi
zaidi kwa wananchi.
Habari Mpenzi wangu,
ReplyDeletei am David Cruz ya Los Angeles katika Marekani kwa ajili ya kushuhudia kampuni hiyo ni hisia za binadamu na Mungu kuogopa watu, ambao nilikutana katika yahoo majibu katika si chini ya masaa 48, nilikuwa kutafuta kampuni zilizokopwa binafsi ambapo i wanaweza kupata usawa mkopo 590,000us inakadiriwa dola .so i aliona mtu kushuhudia kwa makampuni ambayo kutoa wake mkopo wa dola takriban 590,000us katika masaa 24 benki 'Kisha i kuwasiliana na kampuni kwa sababu i hawaamini ushahidi, hivyo i tu alisema basi mimi kujaribu kama kampuni inaweza kusaidia nje ya matatizo ya kifedha ni, Mheshimiwa Smith Alexanda mail yangu na yeye i na kujaza fomu ya kutuma mimi kwamba zitawawezesha kuendelea kwa mkopo mara moja na i hawana na i kufuata yote mchakato na wao alinipa, hivyo kushangazwa mkuu wa mkopo wangu alikuwa uhamisho wa akaunti ya benki si chini ya masaa 24. Sijui ni aina gani ya matatizo ya kifedha kwamba una au una ndoto ya kuwa na nyumbani yako mwenyewe. Makampuni haya ni uwezo wa kufanya ndoto yako ya kweli ya barua pepe ni sasa (smithloanfirm2016@gmail.com) na utakuwa na furaha kama sisi sasa i
Asante
Njia gani yakujiunga
ReplyDeleteTunaomba mawasiliano ya simu za mkononi
ReplyDelete