Na Abdi Shamnah
SERIKALI ya Oman
imeombwa kuangalia uwezekano wa kuyafanyia matengenezo maeneo ya kihistoria,
ikiwa ni hatua za kuendeleza ushirikiano uliopo kati yake na Zanzibar .
Ombi hilo
limetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Mhe. Said Ali Mbarouk, wakati alipofanya mazungumzo na
ujumbe wa Taasisi ya Sayansi na Utamaduni ya Mfalme Qaboos wa Oman , ulioongozwa na Katibu Mkuu
wake, Habib Al Riyami.
Alisema mbali na uhusiano wa muda mrefu uliopo kati ya
wananchi wa nchi hizo, lakini pia kuna maingiliano ya karibu katika tamaduni
zao.
Alisema majengo kadhaa yanayohusisha tamaduni kati ya watu
wa mataifa hayo, yamechakaa na mengine kubaki magofu, hivyo aliuomba ujumbe huo
kuangalia uwezekano wa kuyafanyia matengenezo, ili kuuenzi utamaduni.
Alisema majengo hayo yana umuhimu mkubwa kwa Zanzibar , kwani mbali na
kuenzi hisitoria ya tamaduni ya watu wa nchi mbili hizo, lakini pia hutoa
mchango mkubwa katika nyanja ya utalii.
Aliyataja baadhi ya majengo hayo kuwa ni pamoja na Beit el
Ajaibu, Kasri la Mfalme, mahamuni ya Mtoni, Kizimbani na Msikiti chooko ulioko
Chwaka Tumbe.
Nae Katibu Mkuu wa taasisi hiyo, Habib Al Riyami, aliahidi
kuendeleza ushirikiano wa muda mrefu uliopo katika nchi hizo, kwa faida na
maslahi ya watu wake.
Alisema Oman
itaendelea na juhudi za kuimarisha uhusiano uliopo kupitia nyanja mbali mbali
za kiutamaduni na kijamii.
No comments:
Post a Comment