Habari za Punde

Taarifa kwa Vyombo vya Habari Zanzibar.

STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
    Zanzibar                                                                     27 Januari, 2014
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amemtumia salamu za pongezi Rais wa India Mheshimiwa Shri Pranab Mukherjee kwa kuadhimisha miaka 65 ya Uhuru wa nchi hiyo.

Katika salamu zake hizo, Dk. Shein amesema wananchi wa Zanzibar wanaungana na ndugu zao wa India kusherehekea mafanikio makubwa waliyoyapata katika kipindi hicho cha miaka 65 ya uhuru.

“Tunaupongeza na kuthamini uhusiano uliopo kati ya nchi zetu ambao unazidi kuimarika siku hadi siku na tunaeleza dhamira yetu ya dhati ya kupanua ushirikiano huo katika maeneo ya uchumi, biashara, utamaduni na masuala ya ufundi na uhusiano wa kimaitaifa” Dk. Shein ameeleza katika salamu hizo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ameitumia fursa hiyo kumtakia Rais Mukherjee afya njema na maisha yenye furaha.


Postal Address: 2422 Tel.+255 776 613 015, Fax: 024 2231822 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.