Na
Kauthar Abdalla
MTU
mmoja amefariki dunia baada ya kupigwa rungu la kichwa kutokana na ugomvi wa
familia.
Marehemu
alipigwa rungu wakati alipokwenda kumpeleka rafiki yake nyumbani kwa dada yake
kusuluhisha ugomvi ambao ulikuwepo uliohusisha mambo ya familia.
Tukio
hilo lilitokea
Nyarugusu wilaya ya magharibi Unguja.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo MKuu wa Operesheni ya Polisi Mkoa Kusini Unguja, Hamad
Said Masoud, alisema kifo cha marehemu kilitokea Februari 22 mwaka wakati
akipatiwa matibabu hospitali ya Mnazimmoja.
Alimtaja
marehemu kuwa ni Mussa Haji Suleiman (20) mkaazi wa Mtopepo.
Alimtaja
mtuhumiwa aliyesababisha mauaji hayo kuwa ni Malik Mohammed Ali (30) mkaazi wa
Tomondo mjini Unguja ambae anashikiliwa na polisi na atafikishwa mahakamani
kujibu shitaka la mauaji.
Katika
tukio jengine, mtu mmoja ameokotwa akiwa amefariki dunia karibu na kisima
katika kijiji cha Cheju .
Alisema
marehemu alifariki baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali.
Alisema
marehemu aliyetambuliwa kwa jina la Kombo Khamis Makame mkaazi wa Muembemakumbi,
alikutwa akiwa na majeraha mikononi na mguu wa kulia.
No comments:
Post a Comment