Na Zainab
Atupae, PEMBA
TIMU ya
‘Combine’ ya mkoa wa kaskazini Pemba, imeendelea kuwa ugea kwa timu kama hiyo
ya mkoa wa kusini Pemba, baada ya jana tena kukubali kichapo cha magoli 4-2,
kwenye mchezo maalumu wa kusaka wachezaji watakaounda timu ya taifa ya Tanzania
itakayoshiriki michuano ya mataifa ya Afrika 2015.
Katika mchezo wa awali timu ya hiyo
ya mkoa wa kaskazini Pemba, ilikubali kichapo cha magoli 3-2, ambapo na mchezo
mwengine wa pili pia uliofanyika uwanja wa Gombani timu hiyo iliendelea kuwa
mtija.
Magoli ya timu ya Combine ya kusini
Pemba yaliwekwa wavuni na na mchezaji
Omar Juma, mnamo dakika ya 61, huku goli mengine matatu ypte yaliwekwa
wavuni na mshambuliaji Mussa Ali dakika za
69,81 na 84.
Magoli mawili ya kufutia machozi ya
timu ya Combine ya kaskazini Pemba, yaliwekwa wavuni na Hassan Rashid dakika ya
44 na goli lapili lilingizwa na
mchezaji Suleiman Saidi dakika ya 60.
Kumalizika kwa michezo hiyo miwili ya
kusaka wachezaji wa watakaounda timu ya taifa ya Tanzania, ambayo mwakani itashiriki
michuoni ya mataifa ya Afrika, kambi ya timu ya kusini Pemba imevunjwa rasmi.
No comments:
Post a Comment