KATIBU mkuu wa Chama Cha wananchi CUF, ambaye pia ni makamo wa kwanza wa rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe Maliim Seif Sharif Hamad, akiwahutubia wananchi wa mikoa miwili ya Pemba, katika mkutano wa hadhara wa chama hicho, uliofanyika katika kiwanja cha Tibirinzi Chake Chake.
WAJUMBE wa kamati ya maridhiano Zanzibar, wakibadilishana mawazo, huko katika kiwanja cha Tibirinzi Chake Chake Pemba, katika mkutano wa chama cha CUF, kutoka kulia.Ndg. Edi Riyam,Ndg.Mansour Yussuf Himid,Mhe:Ismail Jussa,Mhe:Aboubaka Khamis Bakari na Mzee Nassor Moyo.
AKINAMAMA wa kikundi Cha ngoma ya msewe kutoka kambini kichokochwe, wakionesha umahiri wao wa kucheza ngoma hiyo ya asili kisiwani Pemba, huko katika kiwanja cha Tibirinzi chake Chake katika mkutano wa hadhara wa CUF. (Picha na Abdi Suleiman, Pemba.)
Nyie CUF kubwa kwenu ni kuangalia akina mama wazazi wetu wakikata viuno tu yaani hata maadili hamna.Zanzibar ni nchi ya Kislamu na haya mambo yamekatazwa katika dini au ndio siasa haina dini?Kumbuka waandaaji na watazamaji wore wana dhambi kwa hiyo Maallim nawe umo ktk hao
ReplyDeleteUmefilisika kimawazo.
ReplyDelete