Habari za Punde

Kijana Oscar John Atafuta Jiko. Ona picha yake na sifa za mchumba huyo anayemtaka

Master Oscar John

Mimi ni kijana wa kitanzania ambaye nimekulia katika maadili ya kidini na malezi mazuri ya kifamia, napenda nichukue fursa hii nitangaze nafasi ya mchumba ambaye kama ata kidhi vigezo vyangu atakuwa ndio mke wangu wa ndoa. Kifupi mi ni mtaalam wa IT naishi Dar es salaam. 
Mchumba ninaye mtaka ni vema awe amekulia malezi ya kidini kwa sababu mimi ni mcha Mungu na napenda kusali kwa hiyo napenda na yeye awe hivyo, malezi yangu ni ya dini ya kikristo ni vema na yeye akawa huko ila itakapobidi anaweza akatoka dini tofauti na mimi, ila itamlazimu aamie kwenye dini yangu, napenda pia asiwe zaidi ya miaka 24, kwa upande wa elimu asiwe chini ya kidato cha nne. 
Namtanguliza Mungu mbele kwa yeyote ambaye anaona anafaa katika vigezo vyangu ili ambariki kabla hajafanya mawasiliano na mimi. 
Kwa mawasiliano na mimi: 
Simu: +255 658 044751 +255 658 044751 FREE  end_of_the_skype_highlighting
Mungu akutangulie wewe utakayeona unafaa kuishi na mimi kama mke na mume. 

Asanteni na karibu

9 comments:

  1. mke anatafutwa hivo subiri uoe jini

    ReplyDelete
  2. Umekosea step ya kwanza ya maisha ya ndoa:COMPROMISE!.
    Wewe unataka mwanamke awe tayari kubadili dini kama atakuwa dini nyengine, kwanini na wewe usiseme kuwa uko tayari kubadili dini ikibidi. Ndoa sio kukamata mpini. Usianze kuonesha kuwa unalotaka wewe tu ndio liwe.Huwezi kuishi na mke kama utajiona wewe ndio muamuzi.

    ReplyDelete
  3. Kama mke awe tayri kubadili dini wewe jee uko tayari kubadili dini Oscar?????

    ReplyDelete
  4. Ha ha haaaa! Oscar ona mambo hayo hapo juu. Yaelekea umejichanganya na kujichanganyua. Umeeleweka ni mtu wa aina gani. Usikate tamaa,jitakase kama utaweza,bado una nafasi kubwa la si hivyo jiunge na face book wamejaa wasio na masharti magumu.

    ReplyDelete
  5. Mpendwa OSCAR maisha bora na upendo hayategemei wanandoa kusali dhehebu moja.Jambo lingine muhimu ni vema ukajua tofauti ya Dini na Dhehebu.

    ReplyDelete
  6. mke mwema anatoka kwa Mungu

    ReplyDelete
  7. Uliposema unasali nilidhani unasali Sala tano

    ReplyDelete
  8. oscar wewe si unasali na ni mcha Mungu omba Mungu akupe mke wa madhabahuni, wako wadada wakristo safi makanisani.

    ReplyDelete
  9. Nadhani kwa maelezo yako tu osacr kuwa umelelewa vizuri na dini...!! Ingekuwa umelelewa vizuri na wokovu ingekuwa Rahisi kwako wala usingeangaika mitandaoni kutafuta mke humu.... Ungesaidia watu wengine kutok katika hili dimbwi la matatizo..... Mungu ni zaidi ya Blog ukisimama nae vizuri anakupa mke had utashangaa mwenyewe

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.