Habari za Punde

Makamu wa pili wa rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akikagua ujenzi wa barabara ya Kidutani hadi mtambile iliyopita katika maeneo ya makaazi ya watu 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na wananchi wa shehia hio mara baada ya kukagua ujenzi wa barabara ya kidutani hadi mtambile iliyopita katika maeneo ya makaazi ya kijiji hicho.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amewataka wananchi wa shehia ya Kidutani Jimbo la Kiwani kuendelea kuunga mkono ujenzi wa miradi mbali mbali ya maendeleo inayojengwa na Serikali ya Awamu ya Nane na kuwapuuza wanasiasa wasioitakia mema Zanzibar.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa shehia hio mara baada ya kukagua ujenzi wa barabara ya kidutani hadi mtambile iliyopita katika maeneo ya makaazi ya kijiji hicho.

Amesema kuwa serikali imeamua kuzijenga barabara zote za mijini na vijijini kwa lengo la kuwaondoshea changamoto za usafiri na usafirishaji wananchi wote wa Zanzibar wakiwemo wananchi wa shehia ya kidutani.

Mhe Hemed amesema serikali itahakikisha inagharamia na kuwalipa fidia wananchi wote  watakaopata athari ya kuharibiwa vipando vyao au sehemu zao za makaazi katika ujenzi wa mradi wa barabara ya kidutani mtambile na sehemu zote ambazo zinapita miradi ya maendeleo kulingana na makubaliano yao.

Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar amefahamisha kuwa Serikali imejipanga kuzijenga barabara zote kwa kiwango cha lami ama kwa zege kulingana na ushauri utakaotolewa na wakandarasi  watakaojenga baranara hizo katika maeneo mbali mbali ya Zanzibar

Mhe. Hemed amewakakikishia wanachi ambao tayari wameshafanyiwa tathmini ya vipando vyao na sehemu zao za makaazi kuwa fedha zao za malipo zipo tayari na wakati wowote zitaingizwa katika akaunt zao.

Wakati huo huo Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar ambae pia ni Mgombea wa Uwakilishi wa jimbo la Kiwani ametumia fursa hio kuwaomba wanachi wa shehia ya kidutani na Kiwani kwa ujumla kumchagua kwa kura nyingi za ndoo ili aweze kuwa muwakilishi wa jimbo hilo ili aendelea kuwatumikia.

Amesema pindi akipata ridhaa ya kuwa muwakilishi wa jimbo hilo atahakikisha yeye na viongozi wenzake  wanajenga wodi ya kisasa ya kujifungulia katika hospitali ya Kendwa ili kuwarahisishia akinamama kujifungulia huko huko kiwani na kuondasha usumbufu wa kufuta huduma hio maeneo ya mbali.

Kwa upande wa sekta ya elimu mgombe uwakilishi jimbo la kiwani ameaahidi kwa kushirikiana na viongozi wenzake watajenga skuli kubwa ya kisasa karibu na makaazi yao ambayo itawaondolea usumbufu wanafunzi wa kufuata skuli masafa ya mbali.

Aidha, Mhe. Hemed amesema kwa kutambua mchango mkubwa wa vijana katika Taifa amesema atakapopata ridhaa ya kuwa mwakilishi wa Jimbo la kiwani atasimamia upatikanaji wa ajira kwa vijana iwe kuajiriwa serikalini ama kuwapa nyenzo za kuweza kujiajiri wenyewe.

Sambamba na hayo amesema ataendelea kusimamia suala la ulinzi na usalama ndani ya Jimbo la Kiwani na kuwataka waanchi kujitokeza kwa wingi kwa kwenda kupiga kura kwa viongozi ambao watawaletea maendeleo mijini na vijijini kikiwemi kijiji cha kidutani.

Imetolewa na kitengo cha Habari ( OMPR )

Leo tarehe 10 / 10 /2025

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.