Habari za Punde

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Amefungua Maadhimisho ya Wiki ya Vijana

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akiwasalimia Wananchi Mkoani Mbeya alipowasili katika viwanja vya Uhindini kwa ajili ya Maadhimisho ya Wiki ya Vijana. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana  na Wenye Ulemavu,  Ridhiwani Kikwete  (wa pili kulia) wakimsikiliza , Mwamtoro Abdallah Khamis  (kushoto) walipotembelea banda la maonesho la  Wajasiriamali kutoka Zanzibar  katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Vijana kwenye viwanja vya Uhindini jijini Mbeya.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu,  Ridhiwani Kikwete wakimsikiliza , Jumbe Lameck alipotoa ushuhuda wa jinsi alivyonufaika baada ya kujiunga kuwa mwanachama wa NSSF walipotembelea banda la maonesho la NSSF katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Vijana kwenye viwanja vya Uhindini jijini Mbeya Oktoba 10, 2025. Kushoto ni Meneja uhusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF, Lulu Mengele.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Ajira, Vijana  na Wenye Ulemavu,  Ridhiwani Kikwete wakimsikiliza , Meneja uhusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF, Lulu Mengele (kushoto) walipotembelea banda la maonesho la NSSF katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kwenye biwanja vya Uhindini jijini Mbeya.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Gonsawa Lungu walipotembelea banda la maonesho la VETA katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Vijana kwenye viwanja vya Uhindini jijini Mbeya.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kasism Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete  alipowasili katika viwanja viwanja vya  Uhindini Jijini Mbeya kwa ajili ya Maadhimisho ya Wiki ya Vijana yaliyofanyika katika viwanja hivyo .
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Isongwe  ya Mbeya ambao walitembelea  uwanja huo kujifunza . Mheshimiwa Majaliwa alifungua Maadhimisho ya Wiki ya Vijana kwenye viwanja vya Uhindini jijini Mbeya.

Waziri Mkuu, Kasssim Majliwa akimkabidhi Laurensia Nathani wa Shule ya Sekondari Mwanzoli Kompyuta Mpakato na  1, 000,000/= baada ya kuwa mshindi wa shindano la uandishi wa insha lililoandaliwa na Shirika la Utangazaji Tanzania TBC Oktoba 10, 2025. Waziri Mkuu alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya vijana Kwenye viwanja vya Uhindini jijini Mbeya, Oktoba 10, 2025. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.