Na Masanja Mabula, PEMBA
JESHI la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba,
limashikilia mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina la Mwanaisha Kiyaka
Ayoub (30) mkaazi wa Pande Tanga na Chake Chake kwa tuhuma za kupatikana
na mafurushi ya bangi.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi
kwa niaba ya kamanda wa Polisi Mkoa huo, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi,
Mlenge Mohammed Mlenge, alisema mtuhumiwa alikamatwa jana majira ya saa 11:50
alfajiri baada ya kushuka kwenye mashua katika bandari ya Wete akitokea Tanga.
Alisema kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo
kumetokana na ushirikiano uliopo kati ya wananchi na jeshi la polisi.
"Taarifa za kwamba kuna mtu anakuja
na bangi tulizipokea mapema na kuweka mtego hapa bandarini Wete, kwa kweli
haikuwa shida kumkata,” alisema.
Aidha alisema baada ya kufanya upekuzi
kwenye begi lake walimkuta
na mafurushi 22 ya bangi.
Aliwataka wananchi kuendelea kuunga mkono
falsafa ya polisi jamii ambayo imekuwa msaada mkubwa katika kukabiliana na
matendo ya uhalifu.
Alisema polisi wanaendelea kukamilisha
uchunguzi kabla ya kumfikisha mahakamani.
No comments:
Post a Comment