Habari za Punde

Tafrija ya Kuwakaribisha Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Katiba Dodoma.

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Alio Iddi akitoa salamu katika Tafrija Maalum ya kukaribishwa kwa wabunge wa Bunge Maalum la Katiba wa CCM Mjini Dodoma.
Waziri Mkuu wa SMT Mh. Mizengo Pinda akitoa Hotuba kwenye Tafrija Maalum ya kukaribishwa kwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wa Chama cha Mapinduzi iliyofanyika ndani ya ukumbi wa Mlimani Grand Mark Mjini Dodoma.
Waziri Mkuu wa SMT Mh. Mizengo Pinda akiwaongoza Wabunge,Wawakilishi  na Wabunge wa Bunge la Katiba kutoka Chama cha Mapinduzi kwenye Tafrija Maalum ya kukaribishwa Wabunge hao Mjini Dodoma.Nyuma yake ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Nd. Vuai Ali Vuai, Mbunge wa Jimbo la Mpendae Mh. Salum Turky na Mwakilishi wa Jimbo la Mwanakwerekwe Mh. Shamsi Vuai Nahodha wakijichukuliwa mlo kwenye tafrija maalum ya kukaribishwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mh. Dr. Sira Ubwa Mwamboya pamoja na Mwakilishi wa Viti Maalum Mh. Salma Bilal wakijumuika na waheshima wenzao wakijipatia mlo kwenye Tafrija maalum ndani ya Ukumbi wa Mlimani Grand Mark Mjini Dodoma.

Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akiwa sambamba na Waziri wa Nchio Ofisi ya Waziri Mkuu Mh.William Lukuvi wakivaa koti saizi ya miili yao kwenye       Tafrija la Kukaribishwa kwa Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba wa Chama cha Mapinduzi Mjini Dodoma.

 Mke wa Mbunge wa Mpendae Mama Tamima Turky, Mbunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Zakia Maghji pamoja na Waziri wa Uwezeshaji Wananchi, Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto Mh. Zaibab Omar akipata Maakuli kwenye tafija ya kukaribishwa wabunge wa Bunge Maalum la Katiba Mjini Dodoma.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa pamoja na Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda wakijumuika pamoja katika kulisakata rumba kwenye tafrija ya kukaribishwa kwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mjini Dodoma.
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiwa na Mke wa Mbunge wa Mpendae Mama Tamima Turky wakionyesha manjonjo yao katika mduara wa tafrija ya kuwakaribisha wabunge wa Bunge Maalum la Katiba wa CCM. 
 Raha iliyoje kwa Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda Kushoto, Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi na Mbunge wa Viti Maalum Chekechake Pemba Mh. Faida Mohd Bakari wakati wakiliskata rumba kwenye tafrija ya kukaribishwa wabunge wa Bunge Maalum la Katiba wa Chama cha Mapinduzi.(Picha na Hassan Issa OMPR)

1 comment:

  1. Ovyo kabisa kwa eeti wanaoitwa viongozi kutuonesha uhuni, sasa ndio wanatupa picha gani, au wanatoa ujumbe gani. Vijana wakiharibika kwa kufuata wanayoyaona eti tunatafuta nani mchawi? Sijui tukoje, na hawa ndugu zangu waislam wao kufuata mkumbo tuu, Mibaba na mimama mizima kazi kutoa ujumbe wa kupotosha kwa jamii.Badilikeni jamani kwa matendo kama haya munapotosha jamii kwani nyinyi ni kioo cha jamii, jamii inakutizameni nyinyi, leo mnafanya hivyo kesho vijana nao wataiga hivyo hivyo kwa kisingizio cha kwamba hata viongozi wa juu wanafanya hiyvohivyo na kwa kuona kuwa sio tatizo, kumbe ndio mwanzo wa mmomonyoko wa maadili.

    Hebu fikiria leo mke wa mtu anacheza na mume wa mtu, kwa kisiongizio burudani, huo ndio mwanzo wa kukaribisha masuala ya zinaaa na mengineyo.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.