Habari za Punde

ZANLINK Yamwaga Vifaa vya Michezo kwa Timu ya Shangani FC Zenj.

Afisa Masoko wa Kampuni ya Mtandao ya ZANLINK Zanzibar Nasib Amour, akimkabidhi seti mbili za Jezi Makamo Mwenyekiti wa timu ya Shangani FC, Halfan Ali Halfan, makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi za Zanlink Majestik.
Afisa Masoko wa Kampuni ya Mtandao ya ZANLINK Zanzibar Nasib Amour, akimkabidhi seti mbili za Jezi Makamo Mwenyekiti wa timu ya Shangani FC, Halfan Ali Halfan, makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi za Zanlink Majestik.
Maofisa wa Zanlink wakiwa  baadhi ya Jezi hizo na Kocha wa timu ya Shangani FC,baada ya kuwakabidhi seti hizo timu ya Shangani ambayo inashiriki Ligi Daraja la Pili Wilaya ya Mjini Unguja. wakiwa na nyuso za furaha
Mambo safi ndivyo inavyoonekana wakimwambia Afisa wa Zanlink mwenye jezi nyekundu akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa timu ya Shangani FC,baada ya kukabidhiwa kwa ajili ya matumizi ya kushiriki ligi daraja la Pili Wilaya ya Mjini Unguja 

Afisa Masoko wa Zanlink Nasib Amour, akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu ya Shangani FC , ikiwa ni msaada uliotolewa na Kampuni hiyokuiunga mkono ili kuweza kushiriki vizuri katika michuano wanayoshiri kuweza kufanya vizuri na kuibuka Bingwa na kurejesha heshima ya timu hiyo miaka ya nyuma.Timu hii iliweza kutowa Ubingwa .
Kocha Mkuu wa timu ya Shangani FC Nadiri Nyuni, akitowa shukrani kwa Kampuni ya Zanlink kwa msaada wao kwa timu yao na kuwafikia wakati ndio wakiwa katikamichuano ya Ligi Daraja la Pili Wilaya yaMjini na kuweza kunanikiwa kupanda daraja,ilikuweza kurejesha heshima kwa timu za Mji Mkongwe kurudi Daraja la Kwanza Taifa.
Na kuitafa kampuni ya Zanlink,isiwe ni mwisho kwa msaada huu uwe ni endelevu kwatimu yao ikizingatiwa Zanlink iko katika mtaa wa shangani. 



1 comment:

  1. Hivi ndivyo inayotakiwa muwe mnasaidia jamii. Endeleeni hivyohivyo kwani mpo juu sana Zanlink hasa kwa jinsi mnavyotuwekea mtandao wenu bure maeneo ya Jamhuri Garden, Forodhani, Bandarini, Airport na Zanlink. Mnatusaidia sana hasa sisi wanafunzi.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.