Dar es Salaam, Tanzania, 18-02-2014: Kampuni ya simu
za mikononi ya Zantel leo imezindua zoezi la kuhamasisha wateja kusajili laini
zao za Zantel kwa mujibu wa sheria ya serikali inayozitaka kampuni za simu
kufanya usajili wa wateja wao.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo, kampeni hiyo
inalenga kutambua wateja wote wanaohudumiwa na Zantel, lakini pia kusaidia
kupunguza matumizi
mabaya ya huduma za mawasiliano, na kuwapa wateja usalama
katika shughuli kama simu benki, usafirishaji wa fedha kwa njia ya simu na
malipo kwa njia ya elektroniki kwa ajili ya huduma kama maji, umeme na kulipia
huduma za luninga.
‘Lengo kubwa la kampeni ni kuhakikisha watumiaji na
wateja wanao jiunga na Zantel wana tambulika na kupewa huduma bora na kampuni
yetu’ alisema Pratap Ghose, Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel.
Usajili wa laini za simu ni wa lazima kutokana na
sheria ya mawasiliano ya 2010 ‘Electronics and Postal Communication Act’
(EPOCA), na chini ya sheria hii ni kosa la jinai kuuza au kusambaza laini ya
simu ambazo hazijasajiliwa. Kutumia laini za simu zisizosajiliwa na kushindwa
kurekodi mauzo ya laini za simu na kutoa taarifa za uongo wakati wakufanya
usajili wa laini za simu.
Kulingana na kipengele 130 m (1) cha EPOCA 2010, mtu
yeyote anaeuza au kwa njia yeyote anatoa simu za mkononi au laini za simu kwa
mtu mwingine yeyote kwa njia sahihi ya sheria bila kurekodi taarifa za mtu huyo
ana fanya kosa la jinai, na mtu huyo akitiwa hatiani ata takiwa kulipa faini ya
shilingi milioni tatu au kwenda jela.
Sheria hiyo pia inamtaka mteja au promota wa laini za
simu ambae kwakujua anatumia au ana sababisha matumizi ya laini za simu zisizo
sajiliwa ana fanya kosa la jinai na akitiwa hatiani ata takiwa kulipa faini isiozidi
500,000/- au kifungo cha jela kisicho zidi miezi mitatu.
‘Tunawaomba watumiaji wote ambao hawaja sajili laini
zao za sim kufanya hivyo haraka na kwa wale wanaotaka kujua hali yao ya usajili
wapige *106#, ili waweze kuendelea kufurahia huduma mbalimbali za Zantel’’ alisisitiza
Pratap.
Kwa kuongezea Pratap alisema ‘Sasa Zantel imerahisisha
kwa wateja wake kusajili kwa kuongeza vituo vya mawakala wa Ezypesa, na maduka
na ofisi za Zantel nchi nzima’
Ili waweze kusajili laini za simu, watumiaji wanatakiwa
kutoa majina yao kamili, namba ya kitambulisho (cha aina yoyote), anuani ya
posta, jinsia, tarehe ya kuzaliwa na namba za simu.
No comments:
Post a Comment