Habari za Punde

Hatimaye Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Apitikana Mwenyekiti wake leo Jioni Dodoma.

               Mhe. Samuel Sitta achaguliwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba.kwa Kura nyiingi.

Mhe. SamuelSitta aibuka kidedea katika uchaguzi wa kuwania nafasi ya Mwenyekiti waBunge Maalum la Katiba Tanzania kwa kura nyingi na kumpita mpizani wake Hashim Rungwe Spunda, Katika uchaguzi uliofanyika jioni hii. katika ukumbi wa Bunge la Katiba Mjini Dodomas.

Mhei Samuel Siita katika uchaguzi huo ameibuka kidedea kwa ushindi mkubwa wa kupata kura 487, dhidi yampizani wake Mhe Hashim Rungwe aliyepata kura 69 katika uchaguzi huo.

Wajumbe waliopiga kura katika ukumbi huo ni  563  na kura 7 zimeharibika.

Matokeo hayo yametangazwa na msimamizi wa uchaguzi huo Katibu wa Bunge,ametowa matokea hayo na ukumbi mzima uliibuka na nderemo na vifiji vya kumshangilia mshindi Mwenyekiti Mpya ewa Bunge la Katiba Mhe, Samuel Sitta na ukumbi wate ukishangilia Sitta sitta..........................

Mkutano huo umeharishwa hadi kesho saa kumi jioni kwa kumchagua Makamo Mwenyekiti wa Bunge la Katiba  ambae atatoka Zanzibar kwa mujibu wa Sheria ikiwa Mwenyekiti atatoka Tanzania Bara basi Makamo wake atatoka Zanzibar.

5 comments:

  1. @ Sasa Mogorila wamepata Gorila Mwenzao, Labda Bunge litakua na Heshima na kumuheshimu Mwenyekiti Wao ... Kwasababu ni:

    1 Mtanganyika Mwenzao.
    2. CCM Mwenzao anaeikandia Katiba ya Warioba kuwa na muundo wa serikali 3.
    3. Ni Mu-umini wakuwaona Wazanziobari Wanapoteza Identity zao kwakutawaliwa na Watanganyika.

    4. Ni Muumini wa muungano wa serikali 1 tu...

    ReplyDelete
  2. tunataka ismail jussa awe kwenye hio nafasi mojawapo wengine hatuwaamini , ismail jussa kumbuka kuwa upo hapo kwa ajili ya znz , usikubaliane na mtu kitu chochote kile kwa manufaa ya nafsi yako , wajumbe wengine tunawajua ni vivuli tu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Makamu atatoka Zanziba na ni lazima awe mwanamke. Kwa hivyo Jussa hana nafasi hiyo. Tunataka serikali moja.

      Delete
  3. serikali moja unataka wewe peke yako bwana mkubwa , waznz wengi hawataki , kujua mbichi na mbivu tufanye kura ya maoni tuone , hawawezi kuwa wenye maarifa na wasio kuwa sawa......

    ReplyDelete
  4. Bora serikali ziwe nne. Moja ya muungano,nyengine ni ya Tanganyika.Iwepo ya Unguja na ya nne ni ya Pemba ili kukata kiromoromo

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.