Na Rose Chapewa, MBEYA
POLISI Mkoani Mbeya, wamefyatua risasi kuwatawanya
wananchi wenye hasira, waliokuwa wakijaribu kuwachoma moto wanawake wawili,
waliowatuhumu kuwa wezi.
Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya,Ahmed Msangi alisema tukio hilo limetokea juzi saa 17.50. jioni
eneo la la Mwanjelwa kata ya
Manga, baada ya wanawake hao kuzingirwa na wananchi wakiwa kwenye duka la mfanyabiashara
mmoja.
Aliwataja wanawake
hao walionusurika kuuawa kuwa
ni Rukia Rashind (24) Jamila Abdalah
(38),wakazi wa
Tunduma wilaya ya Momba na kwamba
wanashikiliwa na polisi kwa mahojiano
zaidi.
Alisema watuhumiwa hao waliingia katika duka la mfanyabiashara aitwaye
Janeth Sivanus (28) wakiwa wamevalia
nguo zinazoficha nyuosa zao na kuiba vitambaa vya vyenye thamani ya shilingi 2,400,000.
Alisema kabla ya kufanya wizi huo, wanawake hao waliuliza vitambaa hivyo na kisha mtuhumiwa
mmoja alikwendelea kumsemesha muuzaji wa duka ambaye alikuwa akiendelea kuhudumia
wateja wengine huku mtuhumiwa wa pili akiiba.
Alisema baada ya
kuiba vitambaa hivyo na kuondoka pasipo mwenye duka kujua, majirani walimjulisha mwenye duka juu ya tukio hilo na
ndipo jitihada zilianza za kuwafuatilia watuhumiwa hao na kufanikiwa kuwakamata karibu na nyumba ya kulala wageni
ya Mfikemo iliyopo mtaa Jua Kali wakiwa
na vitambaa hivyo.
Alisema baada ya kukamatwa lilijitokeza kundi la
wananchi likiwa na silaha lililotaka kuwashambulia huku wakiwa na adumu ya
petrol, lakini wakati wakijiandaa kutekeleza unyama huo polisi walifika na
kufyatua risasi hewani kuwatawanya na kuwaokoa wanawake hao.
Kamanda Msangi alitoa wito kwa jamii kuacha tabia
ya kujichukulia sheria mkononi kwani sio
tabia nzuri na ni kinyume cha sheria.
No comments:
Post a Comment