Habari za Punde

KINANA AZINDUA MRADI WAUJENZI NYUMBA 60 INYONGA KATIKA WILAYA MPYA YA MLELE UNAOFANYWA NA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba 60 za makazi ya watu zinazojengwa na Shirika la Nyumba ya Taifa katika Wilaya ya Mlele mkoani Katavi.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana  akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Shirika la Nyumba Mkoa wa Katavi, Nehemia Msigwa juu ya miradi ya ujenzi wa nyumba itakayofanyika ndani ya mkoa wa Katavi.
Michoro ya nyumba zitakazojengwa mkoani Katavi na Shirika la Nyumba ya Taifa,ambapo wilaya ya Mlele ,Shirika la Nyumba linajenga nyumba 60 na zitachukua  miezi nane kukamilika.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr. Rajab Rutengwe  akizungumza mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la uzinduzi wa nyumba 60 zitakazojengwa na Shirika la Nyumba  la Taifa  katika wilaya ya Mlele.
Meneja wa Huduma za Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa Ndugu Muungano Saguya akizungumzia namna Shirika la Nyumba lilivyojipanga katika kuboresha makazi ya watu katika mkoa wa Katavi. Picha na Adam Mzee(Bashir Nkoromo)

2 comments:

  1. Hii sio kazi ya Katibu Mkuu wa CCM mbambo haya yanatakiwa kufanywa na Waziri anaeshughulika na mambo ya Ujenzi.Siasa za namna hii ndio mwanzo wa matatizo.Imarisha chama mzee Kinana usiingilie mambo ya Serikali.

    ReplyDelete
  2. Anonymous1
    Hongera sana mdogo wangu wee... Unayosema ni kweli kabisa imekua ni kawaida ya CCM kuchukua pesa za walipa kodi, za mikopo na za Misaada ya Nje na kuimarisha shughuili za Kichama.. Na hili Ndilo wanalolilia vyama vya Upinzani... Kwamba kuwe na Serikali 3 ambazo zitakua na account moja ya Muungano ambayo mapato ya matumizi ya Serikali yatakua yanajulikana... Hivi tunavyoona ni Propaganda za CCM kujifanya kwamba CCM ndio inayofadhili hela hiyo .. Nakuonekana Wapinzani hawafanyi kitu cha maana.... Kazi ipo kweli kweli hata kuelimisha Watangnayika wote wa Vijijini wakaelewa nini CCM inavyoharibu Hela ya walipa KOdi na Mikopo..... halafu wazanzibari nao wakidai Nchi yao nakusema Kwamba Muungano umevaa Joho la Tanganyika Munawaona wabaya...

    Aiseeee CUF na Chadema kazi wanayo kweli huku kwetu Tanganyika......Hizi nyumba wamesema kwamba ni kuwasaidia Watanzania wote.. Mbona kule Visiwani hawajapeleka mradi kama huu?

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.