Habari za Punde

Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ.

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR
 

HOTUBA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ
 UTEKELEZAJI WA SERIKALI ZA MITAA
MHE. HAJI OMAR KHERI
KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA WA FEDHA 2014/2015
KATIKA BARAZA LA WAWAKILISHI LA ZANZIBAR


YALIYOMO
Serikali za Mitaa ndio mhimili mkubwa wa utekelezaji wa majukumu ya Serikali katika lengo zima la kuhakikisha kunakuwepo maendeleo endelevu katika nchi yetu. Katika kufanisha azma hiyo, Serikali kupitia Mpango wa Mageuzi ya Serikali za Mitaa imedhamiria kuziwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa kutoa huduma bora kwa wananchi. Hata hivyo, jukumu hilo haliwezi kutekelezeka kama Halmashauri zetu hazitokuwa na wataalamu pia hazitaweza kuongeza mapato na kuwa na nidhamu katika matumizi.
Lengo ni kuwa na Serikali za Mitaa zenye Wataalamu wake wenyewe zenye kubuni mipango yake ya maendeleo na kuweza kuitekeleza kwa rasilimali zao wenyewe. Ushirikishwaji wa wananchi na kuweza kutoa maamuzi yao yenyewe ni mambo ya msingi yatakayozingatiwa katika mpango huo mzima.
Kutokana na hali hiyo, Serikali itaimarisha usimamizi wa mapato na matumizi katika Serikali za Mitaa. Hivyo, Taasisi hizo zinawajibu wa kuhakikisha kuwa Sheria, Kanuni na Taratibu za Fedha zinazingatiwa. Aidha, Ofisi yangu itahakikisha Serikali za Mitaa zinaongeza uwazi katika mapato na matumizi ili kuwawezesha wananchi kushiriki katika kupanga, kufuatilia na kutathmini Mipango na utekelezaji kulingana na vipaumbele vyao.
Kwa mwaka wa fedha 2013/2014 Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa ujumla wake zimefanikiwa kutekeleza malengo yake kama yalivyopangwa. Majadweli ya hapo chini (Namba 1 hadi 13) yanaonesha uchambuzi wa kina wa malengo, shughuli zilizopangwa kutekelezwa na utekelezaji wake. Aidha, kwa mwaka wa fedha 2014/2015 Mamlaka za Serikali za Mitaa zimepanga kutekeleza malengo ambayo pia yameoneshwa kwa ufasaha.
Kwa mwaka wa fedha 2013/2014, Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa ujumla wake zilikadiriwa kukusanya jumla ya TZS 4,783,343,580/=. Hadi Machi 2014, Mamlaka hizo zimefanikiwa kukusanya 2,934,237,898 milioni sawa na asilimia 61  Aidha, kwa mwaka wa fedha 2014/2015 Serikali za Mitaa zimekadiria kukusanya jumla ya 5,162,581,500/= kutoka katika vyanzo vyake mbali mbali (Angalia Kiambatanisho Nambari. 1).

Kiambatanisho Nambari 1: Makadirio ya Makusanyo, Makusanyo Halisi kwa mwaka 2013/2014 na Makadirio ya Makusanyo kwa Mwaka 2014/2015
Namba
Taasisi za Serikali za Mitaa
Malengo ya Makusanyo ya Mapato 2013/2014
Fedha Zilizokusanywa hadi Machi 2014
Asilimia ya Fedha Zilizopatikana hadi Machi 2014
Makadirio ya Makusanyo Mwaka 2014/2015
1
Baraza la Manispaa
2,743,140,580
1,317,063,132
48
2,555,324,500
2
Baraza la Mji Mkoani
40,000,000
52,965,700
132
70,000,000
3
Baraza la Mji Chake Chake
100,000,000
107,391,300
107.3
150,000,000
4
Baraza la Mji Wete
65,000,000
40,229,282
61.89
110,000,000
5
Halmashauri ya Wilaya ya Magharibi
800,000,000
540,146,634
67.51
950,000,000
6
Halmashauri ya Wilaya ya Kati
200,000,000
137,871,502
68.95
204,100,000
7
Halmashauri ya Wilaya ya Kusini
129,900,000
93,280,750
71.81
131,296,000
8
Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini "A"
177,500,000
139,045,124
78.3
295,125,000
9
Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini "B"
281,000,000
220,766,000
78.56
309,700,000
10
Halmashauri ya Wilaya ya Mkoani
51,265,000
74,869,822
146
85,000,000
11
Halmashauri ya Wilaya ya Chake Chake
48,728,000
47,711,510
98
82,306,000
12
Halmashauri ya Wilaya ya Wete
66,424,000
67,419,600
101.4
100,000,000
13
Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni
80,400,000
99,236,650
123
120,000,000

JUMLA
4,783,343,580
2,934,237,898
61
5,162,581,500

2.     BARAZA LA MANISPAA

Jadweli Namba 1: Utekelezaji wa Baraza la Manispaa kwa Mwaka 2013/2014.

Malengo ya Mwaka 2013/2014
Shughuli Zilizopangwa Kutekelezwa
Utekelezaji Halisi
1. Kuimarisha na kusimamia ukusanyaji wa Mapato ya TZS 2,743,140,580   na matumizi bora ya Baraza. 
1.Kukusanya mapato ya TZS 2,743,140,580   kupitia vianzio vyake vya ndani vya mapato (maegesho , matangazo, leseni za biashara na ada za usafi)
Jumla ya Tshs 1,317,063,132.  sawa na asilimia 48% ya lengo zimekusanywa kupitia vianzio vya ndani vya Baraza la Manispaa. Changamoto kubwa iliyojitokeza ni baadhi ya wafanyabiashara kukataa kubadilishiwa ada za leseni lakini watendaji waliwaelimisha na kuwanasihi na hatimae kukubali.
2. Uchapishaji wa Stakabadhi mbalimbali za ukusanyaji wa Mapato
Stakabadhi za ukusanyaji wa mapato zinachapishwa na kutumika katika shughuli mbali mbali za utoaji wa huduma za Baraza la Manispaa.
3. Kuimarisha takwimu za vianzio vyote vya Mapato ya Baraza la Manispaa kwa kuvishirikisha vikundi vya Polisi jamii
Takwimu za vianzio vya mapato zimekusanywa na uchambuzi wake umeanza. Shughuli hii inaendelea kutekelezwa kupitia Mradi wa ZUSP.
4.Kuendelea na utaratibu wa kupunguza madeni pamoja na kuwapatia Waheshimiwa Madiwani fedha za “ Political vote”
Madeni ya jumla ya TZS 50,877,575 yamelipwa, Madeni hayo yaliyolipwa ni malipo ya stakabadhi, vipuri vya magari na ada za uanachama (TACINE, AMICAAL na World Haritage) na TZS 29,000,000 (political vote) wamelipwa Waheshimiwa Madiwani,
2. Kutoa huduma endelevu za usafishaji wa mji kwa kushirikisha jamii na wakaazi wote wa Manispaa ya Zanzibar ili kuweka mazingira bora kiuchumi na kijamii.
1. Kuelimisha jamii juu ya masuala ya afya na usafi wa mazingira kwa kutumia vyombo vya habari, mikutano na Siku ya Manispaa
Vipindi vya redio na TV vilitayarishwa kupitia ZBC, Coconut FM na Zenji FM na kurushwa hewani.  Mikutano mitano ya wazi na mikutano baina ya waandishi wa habari kwa lengo la kuhamasisha jamii ilifanyika

2.Kuboresha huduma za ukusanyaji na uondoaji wa taka kwa maeneo yote ya Manispaa ya Zanzibar kwa kushirikiana na vikundi jamii
Baraza limebinafsisha huduma ya usafishaji wa barabara kuu kwa kuingia mikataba na vikundi vya kijamii na Jumla ya tani 72,000 za taka zimeondolewa katika vizimba vilivyopo katika maeneo mbali mbali ya Manispaa.

3. Kusimamia na kuendeleza maeneo ya wazi na bustani za mji ziwe na hadhi na haiba ya kupendeza kwa jamii, wageni na wapita njia.
 Kazi za ufyekaji wa bustani katika maeneo ya njia  kuu ya Michenzani, bustani ya Donge na barabara ya Kariakoo, ukataji wa matawi ya miti na ukataji wa miti mibovu katika maeneo ya Mwanakwerekwe, Malindi, Darajani na Ng'ambu zimefanyika
3.Kuimarisha ufanisi wa utendaji kazi
1. Kulinda afya za wafanyakazi kwa kuwapima na kuwapatia madawa pamoja na kufanya ufukizaji katika majaa na masoko.
Jumla ya wafanya kazi 100 wa kuzoa  taka ngumu, kusafisha makaro na michirizi ya maji machafu na ya maji ya mvua wameshapimwa afya zao Hospital ya Mnazi Mmoja. Baraza linasubiri ripoti kamili ya vipimo hivyo kutoka wizara husika.


1.      Kuwajengea uwezo wafanyakazi kwa kuwapatia mafunzo ya muda mfupi na mrefu katika utunzaji ghala, takwimu, sheria na afya ya mazingira pamoja na inhouse training.
Jumla ya wafanyakazi 2 wamesaidiwa gharama za masomo yao ya muda mrefu. Mfanyakazi mmoja anasoma Shahada ya kwanza ya Utawala wa Umma na mmoja Stashahada ya Usimamizi wa bustani

3. Kuweka mazingira mazuri ya kazi kwa kununua vitendea kazi ili kutoa huduma bora na kwa ufanisi.
Nyenzo na vitendea kazi kwa wafanyakazi vimenunuliwa.  Vifaa vilivyo nunuliwa ni glavu,,viatu, 'over roll', makoti ya mvua, bero, magamba ya leseni, pauro, mabwela,  pamoja na suti kwa waheshimiwa madiwani
4. Kufanya mapitio na marekebisho ya sheria pamoja na kuandaa sheria ndogo ndogo.
 Kanuni za udhibiti wa wanyama, ukodishwaji wa mabango na maegesho zimeweza kufanyiwa mapitio na marekebisho kwa kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na kutayarisha kanuni mpya ya matangazo

5.Kuwapatia wafanyakazi sare maalum za utambulisho katika maeneo ya kazi.
Wafanya kazi wa kuzoa taka ngumu, kusafisha michirizi, mafundi gereji, askari wa Baraza la Manispaa na baadhi ya madereva wamepatiwa sare.
4. Kuimarisha ufanisi wa baraza kwa kuendesha vikao vya kamati, baraza la madiwani na ziara za kimafunzo kwa kila kamati
1. Kuendesha vikao vya kamati vya kila mwezi na vile vya Baraza la Madiwani kila baada ya miezi mitatu.
Kamati tano za kudumu zimefanya vikao vyake kwa wakati.  Mikutano mitatu ya Baraza  la Madiwani imefanyika. Vikao vilipokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa Baraza.

2. Kudumisha na kuendeleza urafiki na kushiriki mikutano, semina na shughuli za ufuatiliaji kazi ndani na nje ya Tanzania
Watendaji wa Baraza wameshiriki mikutano na semina za ndani ( mikutano ya TACINE, UDCA) na kushiriki mikutano na ziara za nje ya nchi ( China, Korea, Afrika ya Kusini, Swaziland)
5. Kuimarisha na kuifanyia ukarabati michirizi ya maji machafu na ya mvua pamoja na kuimarisha huduma za vyoo vya umma ndani ya maeneo ya Manispaa ya Zanzibar
1. Kuisafisha na kuifanyia matengenezo madogo madogo michirizi ya maji machafu na ya mvua ndani ya Manispaa ya mji wa Zanzibar kwa kuifanyia ukarabati.
Kazi za uzibuaji wa makaro na usafishaji  katika maeneo ya Mji Mkongwe,  Ziwani, Jitini, U.U.B, Makadara, Jang'ombe Kwachimbeni, Kiswandui, Kariakoo na Migombani zimefanyika pamoja na kufanyiwa ukarabati mdogo
6. Kutengeneza na kuendeleza njia za wapitao kwa miguu, maeneo ya maegesho pamoja na kutunza  na kuyafanyia ukarabati wa majengo ya ofisi na masoko ndani ya Manispaa ya Zanzibar
1. Kutengeneza na kuendeleza ukarabati wa njia za wapitao kwa miguu na maeneo ya maegesho na ukarabati wa majengo ya ofisi na masoko ndani ya Manispaa ya Zanzibar.
Jumla urefu wa mita 489 zenye upana wa mita 1.5 za njia ya wapitao kwa miguu katika maeneo ya Michenzani Jumba namba 8 zimekamilika.


1. Kuimarisha ukusanyaji wa mapato, usimamizi bora wa fedha na Manunuzi na kuzifanyia mapitio na kuunda sheria ndogo ndogo mpya za Baraza la Manispaa.
2. Kutoa huduma endelevu za usafishaji wa mji kwa ufanisi kwa kushirikiana na vikundi vya kijamii katika usafishaji na usafirishaji taka.
3. Kusimamia na kuendeleza maeneo ya wazi, bustani na njia za wapitao kwa miguu.
4. Kuweka mazingira bora ya kazi kwa kulipa stahiki za wafanyakazi, upatikanaji wa nyenzo na kugharamia shughuli za uendeshaji.
5. Kuwajengea uwezo wafanyakazi kwa kuwapatia mafunzo ya muda mrefu na mfupi, semina na kushiriki mikutano ya mashirikiano.
6. Kuimarisha ufanisi wa Baraza kwa kuendesha vikao vya kamati, Baraza la Madiwani na ziara za kimafunzo kwa kila kamati na kuchangia miradi ya maendeleo.
7. Kuimarisha na kuendeleza ukarabati wa maeneo ya maegesho, michirizi na kuyafanyia ukarabati majengo ya ofisi na masoko ndani ya Mji wa Zanzibar.


Jadweli Namba 14: Utekelezaji wa Mradi wa ZUSP
Malengo ya Mwaka 2013/2014
Shughuli Zilizopangwa Kutekelezwa
Utekelezaji Halisi
1. Kuuimarisha  uwezo wa Baraza la Manispaa katika kubuni na kusimamia utekelezaji wa ukarabati , ujenzi wa miundo mbinu ya huduma za miji kwa ajili ya    kutoa huduma endelevu Mjini.

1. Kutafuta Mshauri Elekezi katika kuimarisha uwezo wa utekelezaji wa Manispaa kwa miaka mitatu
Mshauri elekezi wa kukuza uwezo wa kiutendaji wa Baraza la Manispaa  ameanza kazi

2. Kufanya ukarabati wa Afisi kuu Darajani na Karakana ya Saateni Manispaa

Ukarabati wa Afisi Kuu Darajani umeanza kwa kuezeka paa, kutia plasta  kurekebisha kuta, ujenzi wa mitaro, na ujenzi wa jengo dogo sambamba namatengenezo ya Karakana ya Manispaa Saateni.   

3. Kutafuta Mshauri Elekezi kwa kusimamia kazi za ukarabati na ujenzi wa mitaro ya maji ya mvua na uwekaji wa taa za barabarani.
Utekelezaji wa shughuli ya  umeanza baada ya Kampuni ya Techniplan kutoka Israel kufunga Mkataba. Ukarabati na Ujenzi wa mitaro ya maji ya mvua unatarajiwa kuanza Mwezi wa Julai, 2014. Maeneo yatakayonufaika na mradi huu  ni Ziwa la Sebleni,  Ziwa la kwa Binti Amrani - Mpendae, Kwamtipura, Kilima hewa, Karakana, Sogea, Mpendae, Jang’ombe (Botanical garden), Uwanja wa Demokrasia na Shauri moyo.Uwekaji wa taa barabarani  mjini tunatarajia kuanza Mwezi wa Julai 2014. Maeneo yatakayo kunufaika na ujenzi huo ni baadhi ya  maeneo ya Mji Mkongwe kama Shangani,  Mkunazini na Kiponda  na maeneo ya Ngambo ni barabara za Amani hadi kwa Biziredi, Amani hadi Mzunguko wa Mwanakwerekwe, Mzunguko wa Mwanakwerekwe hadi Magomeni na Vuga hadi Baraza la Wawakilishi la zamani.


4. Kujenga vizimba 80 vya kuhifadhia taka.
Jumla ya vizimba 50 vimejengwa katika maeneo ya Halmashauri ya Wilaya ya Magharibi  chini ya Usimamizi wa wataalamu wa Manispaa

5. Kununuzi wa vifaa vya Ofisi
Kompyuta 14, laptop 8, printa 5, Projekta 2 na Scanner 2 kwa ajili ya matumizi ya shughuli mbali mbali za  Manispaa zimenunuliwa.

6. Kununua gari la kunyonya uchafu wa vyoo na makaro
Gari moja imenunuliwa.

7. Ununuzi wa  gari la kusafishia mchanga 
Taratibu za ununuzi zimekamilika, gari bado haijawasili.

8. Ununuzi wa gari moja ya kutengenezea taa za barabarani
Gari imenunuliwa na tayari imeshafika Zanzibar.
9. Ununuzi wa gari tano za Wakuu wa Idara tano za Manispaa 
Gari zimenunuliwa
10. Ununuzi wa Vespa kumi  za kufuatilia kazi za Manispaa 
Vespa zimenunuliwa
11. Ununuzi wa vifaa vya kazi na thamani kwa ajili ya Idara ya Mipango Miji.
 Vifaa vimenunuliwa
12. Ununuzi wa gari moja ya Idara ya Mipango Miji.
Gari imenunuliwa

13. Ununuzi wa mikokoteni ya taka na vikapu vya taka 193
Mikokoteni imeshanunuliliwa 
14. Kusambaza Mapipa ya kuhifadhia taka 
Mapipa yamesambazwa katika maeneo ya Mji Mkongwe

15.Ununuzi wa Magari ya taka ya vikapu
Gari zimenunuliwa na zinatarajiwa kuwasili mwishoni mwa mwezi wa Julai.

16. Kununua magari mawili ya tipa
Magari yamenunuliwa na tayari yameshafika Zanzibar.


1.     Kuimarishaji  uwezo wa Baraza la Manispaa katika kukuza mapato,   utumishi bora na kuhamasisha ushirikishwaji wa jamiii katika kuchangia  utekelezaji wa  huduma endelevu Mjini.

2.     Kuimarisha huduma za usafi wa mji kwa kujenga  misingi ya maji ya mvua ,

3.     Kuimarisha mandhari bora ya mji wa Zanzibar kwa kuweka taa za Barabarani

4.     Kuinua uwezo wa ufanisi kwa watendaji wa  Manispaa kwa kufanya kazi katika mazingira mazuri kwa kujenga afisi bora

5.     Kukarabati Karakana ya Manispaa iliopo Saateni

Jadweli Namba 2: Utekelezaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Magharibi kwa Mwaka 2013/2014

Malengo ya Mwaka 2013/2014
Shughuli Zilizopangwa Kutekelezwa
Utekelezaji Halisi
1. Kuimarisha ukusanyaji wa mapato wa Halmashauri kwa asilimia17 kutoka  681 milioni mwaka 2012/2013 mpaka 800 milioni mwaka 2013/2014
1.Kufuatilia ukusanyaji wa mapato ya TZS 800  milioni.
Ufuatiliaji umefanyika kwa njia ya ukaguzi wa leseni, michirizi ya maji machaf, (kutoza faini), mabango ya matangazo, majenzi na matumizi ya rasilimali za misitu na kufanikiwa kukusanya  jumla ya TZS. 537.4 milioni sawa na asilimia 67.2
2. kuendeleza mfumo wa takwimu za wafanya biashara
2. Ofisi imekamilisha hatua ya uchukuwaji wa taarifa za wafanya biashara katika Wilaya ya Magharibi na kuanza kuziingiza katika Mfumo wa Takwimu "Data Base” ya Halmashauri.              

3. Kutayarisha Mpango Mkakati wa Halmashauri.
Rasimu ya awali ya Mpango Mkakati wa Halmashauri imeshatayarishwa na iko tayari kwa kuwasilishwa kwa wadau ili waweze kutoa maoni yao kwa kuiboresha.
4. Kuendesha vikao vya Baraza la Madiwani.
Vikao vitatu   vya Baraza la Madiwani vimefanyika na kujadili utekelezaji wa shughuli za Halmashauri pamoja na kupokea mapendekezo ya Bajeti ya  mwaka 2014/2015
2.Kutunga/ kufanya mapitio ya Sheria ndogo ndogo katika kuendeleza shughuli za Halmashauri.
1. Kutoa elimu juu ya Sheria ndogo ndogo za Halmashauri
Semina moja juu ya kujenga   uelewa wa sheria ndogo ndogo za Halmashauri imefanyika kwa Madiwani na watendaji   
2. Kuendesha vikao vya Kamati ya Sheria na maendeleo ya wafanyakazi.
Vikao vitatu vimefanyika na kujadili Usimamizi wa Sheria katika utekelezaji wa shughuli za Halmashauri pamoja na Maendeleo ya wafanyakazi kwa kuzingatia upatikanaji wa stahiki zao na mikataba.
3. Kutekeleza miradi mbalimbali kwa lengo la kukuza ustawi
1. Kuendeleza ujenzi wa Ofisi ghorofa ya pili.
Ujenzi wa ghorofa ya pili ya Ofisi umekamilika.
2. Kujenga maegesho ya magri mbele ya soko la Mwanakwerekwe
Ujenzi wa maegesho  umefanyika na wastani wa gari 36 zinaweza kuegesha kwa wakati mmoja.
3. Kusaidia miradi ya Wanachi katika Wadi tano.
Halmashauri imesaidia usamabazaji wa umeme katika kijiji cha Bumbwisudi, kuchimba visima viwili katika Wadi ya Mwanyanya na Bububu, kuezeka Madrasa katika Wadi ya Magogoni, ujenzi wa Skuli ya Chekechea Nyamanzi, ujenzi wa Ofisi ya SACCOS Mwera pamoja na kusaidia vifaa vya Ujenzi wa Skuli ya Kihinani
4. Kuendesha vikao vya Kamati ya Fedha na Mipango Miji.
Vikao tisa vilivyojadili mapato na matumizi ya kila mwezi, utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2014-2015 na kutayarisha rasimu ya bajeti 2014-2015  vimefanyika.
4. Kujenga uwezo kwa Waheshimiwa Madiwani na Watendaji wa Halmashauri
1. Kufanya safari za kikazi ndani na nje ya nchi.
Safari mbili za kikazi zimefanyika Dar es salaam na Pemba kwa lengo la ufuatiliaji wa mapato na shughuli nyengine za kikazi.  Katika ziara hizo Halmashauri imefanikiwa kulipwa deni la siku nyingi kutoka kwa Kampuni ya TIGO.  

2. Kutoa mafunzo ya muda mrefu na mfupi kwa wafanyakazi.
Jumla ya wafanyakazi wanne, ambapo wawili wanawake wamepata mafunzo ya muda mrefu katika ngazi za  Stashahada ya utunzaji wa kumbukumbu na rasilimali watu na wafanyakazi wawili wanaume wamepatiwa mafunzo ya muda mfupi katika fani ya udereva.

3.Kufanya semina za kuongeza uelewa na uwezo wa Waheshimiwa Madiwani
Semina zilizohusu (i) Mwelekeo wa Sera ya Serikali za Mitaa (ii) Mpango wa Matumizi ya ardhi (iii) Uwekezaji katika Maeneo Huru, (iv) Mfumo mpya wa Bajeti za Serikali na (v) Uratibu wa Mipango ya Serikali zimefanyika
5. Kuongeza ufanisi kazini na kuwapatia wanyakazi stahili zao
1. Kulipa posho na mishahara kwa wafanyakazi wa muda pamoja na stahiki zao
Wafanyakazi wote 38 wamelipwa mishahara yao ya kila mwezi na stahiki zao zote

2. Kulipa posho la kila mwezi kwa Waheshimiwa Madiwani pamoja na stahiki zao
 Jumla ya Madiwani 20 wamelipwa posho la kila mwezi pamoja na stahiki zao.

3. Kuimarisha shughuli za uendeshaji wa kazi za ofisi
Malipo yote ya mafuta, matengenezo ya magari, ulinzi, vifaa vya kuandikia, umeme na kodi ya jengo la kitengo cha usafi wa mazingira yamefanyika

4. Kushiriki katika sherehe za maadhimisho ya sherehe za kitaifa.
Maandalizi ya  ufunguzi wa jengo la Ofisi pamoja na kufanya operesheni maalumu  za usafi katika kuelekea sherehe za  miaka 50 ya Mapinduzi  ya Zanzibar

5. Kutoa misaada kwa wafanyakazi wanaopatwa na matatizo kazini.
Misaada imetolewa kwa wafanyakazi waliopatwa na matatizo mbalimbali pamoja na ubani wa ufiwa na wafanyakazi 30 wamepimwa  afya zao


Malengo ya Halmashauri ya Wilaya ya Magharibi kwa Mwaka  2014/2015

·         Kukusanya mapato kwa ongezeko la asilimia 18.kutoka 800 milioni mwaka 2013/2014 mpaka 950 milioni mwaka 2014/2015.

·         Kuimarisha huduma za usafi wa mazingira katika maeneo ya Halmashauri.

·         Kukuza ustawi wa Jamii na kupunguza umasikini kwa kutekeleza Miradi ya Maendeleo.

·         Kuimarisha mazingira ya utendaji na maslahi ya watendaji.

Jadweli Namba 3: Utekelezaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini "A" kwa Mwaka 2013/2014

Malengo ya Mwaka 2013/14
Shughuli Zilizopangwa Kutekelezwa
Utekelezaji Halisi
1.  Kukusanya mapato ya jumla ya TZS. 177.5 milioni kutokana na vyanzo vyake mbali mbali vya mapato;

1. Kukusanya mapato kutoka vianzio vya Halmashauri
Mapato yamekusanya kutokana na ada za leseni, mabango ya matangazo, majenzi na matumizi ya rasilimali za misitu na kufanikiwa kukusanya  jumla ya TZS 139,045,144/= sawa na asilimia 78

2. Kuwashajihisha na kuelimisha  wafanyabiashara 30 juu ya umuhimu wa kulipa kodi kwa hiari na kuendesha mafunzo kwa watendaji 20 juu ya kumjali mteja
Wafanyabiashara 30 na watendaji 20 wameelimishwa  juu ya umuhimu wa kulipa kodi kwa hiari na kumjali mteja.

3. Kuendeleza na kusimamia mpango wa takwimu ( Database) za Halmashauri
 Mpango wa takwimu (Database)  za Halmashauri hasa vyanzo vya mapato umeendelezwa kwa kuandaa ''template'' za kuingizia taarifa za wafanyabiashara.
2. Ukarabati wa Ofisi ya Halmashauri Mkokotoni;

1.     Kufanya ukarabati kwa kujenga ukumbi wa, kupiga plasta, kujenga sakafu na kuezeka.
2.     Kukamilisha ukumbi kwa kutia feni, viyoyozi na samani za ofisi. 
Shughuli zote zimefanyika 
3.     Ujenzi wa Ofisi ndogo na nyumba ya Halmashauri, maduka ya Halmashauri Pwani Mchangani, soko la Mkwajuni, kiwanda cha kukoboa na kusaga nafaka na maegosho ya gari;

1.     Ujenzi wa Ofisi ndogo na nyumba ya Halmashauri.

2.      Ujenzi wa maduka ya Halmashauri Pwani Mchangani na Kiwanda cha kusaga nafaka.

3.     Soko la Mkwajuni na
maegosho ya gari
Fedha za shughuli hizi zimehaulisha na kuingizwa kwenye mradi wa ujenzi wa ukumbi kupitia kikao cha Baraza la Madiwani.

Ukarabati wa Soko la Mkwajuni na maegesho ya gari yamefanyika.
4.     Ukarabati wa njia ndogo za Tumbatu na Shindoni/Chutama;

1.     Kufanya ukarabati wa njia ndogo za Tumbatu
2.     Kufanya ukarabati njia ndogo Shindoni/Chutama;

Ukarabati wa njia ndogo za Tumbatu na Shindoni/Chutama umefanyika na kukamilika

5.     Kununua pikipiki/vespa mbili, samani na mashine za Ofisi
1.     Ununuzi vespa mbili.
2.     Ununuzi samani na mashine za Ofisi
Vespa moja pamoja na mashine za Ofisi zikiwemo mashine ya fotokopi 1, komputa 1 na printa mbili zimenunuwa
6.     Kuendesha mafunzo ya muda mrefu na mfupi kwa watumishi wa Halmashauri, kufanya ziara za kimasomo kwa Madiwani na kuendesha programu maalum ya usafi.

1.     Kuendesha mafunzo ya muda mrefu na mfupi kwa watumishi na madiwani wa Halmashauri
2.     Kufanya ziara za kimasomo kwa Madiwani na kuendesha programu maalum ya usafi.
Mafunzo ya muda mrefu na mfupi kwa watumishi wawili (Katibu muhtasi na usimamizi wa fedha) wa Halmashauri na programu maalum ya usafi zimefanyika

Malengo ya Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini "A"kwa mwaka wa fedha wa 2014/2015


1.       Kuimarisha ukusanyaji wa mapato kutoka TZS.177,500,000/= kwa mwaka 2013/2014 hadi kufikia TZS.295,125,000/= kwa mwaka 2014/2015
2.       Kuimarisha vyanzo vya mapato katika mamlaka ya Hamashauri
3.       Kuimarisha usafi wa mazingira katika mamlaka ya Halmashauri
4.       Kusaidia miradi ya maendeleo na ya wananchi katika kujiletea maendeleo
5.       Kuwajengea uwezo watendaji na madiwani katika mamlaka ya Halmashauri
6.       Kuimarisha uendeshaji wa shughuli za Ofisi
      
4.  HALMASHAURI YA WILAYA YA KASKAZINI "B"

Jadweli Namba 4: Utekelezaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini "B"kwa Mwaka 2013/2014

Malengo ya Mwaka 2013/2014
Shughuli Zilizopangwa Kutekelezwa
Utekelezaji Halisi
1.Kuimarisha ukusanyaji wa mapato yanayotokana na vianzio vya Halmashauri
1. Kukusanya mapato ya TZS 281 milioni kutoka katika vianzio vya Halmashauri
Mapato ya TZS 220,766,000/=  yamekusanywa sawa na asilimia 79 hadi kufikia Machi 2014. Mapato hayo yametokana na ada za leseni, mabango ya matangazo, majenzi na utumizi wa rasilimali za mchanga, mawe na kifusi.
2. Kushajihisha na kuelimisha jamii na wafanya biashara juu ya umuhimu wa kulipa kodi na kufuata taratibu za Halmashauri katika uendeshaji wa biashara
 Jumla ya mikutano 8  imefanywa kwa wanajamii na wafanyabiashara iliyolenga kuongeza uelewa na kuwahamasisha kulipia ada mbali mbali za biashara zinazokusanywa na Halmashuri.
3. Kutoa mafunzo kwa Makarani na watendaji wa Halmashauri wanaohusika na ukusanyaji wa kodi na ada za Halmashauri.
 Jumla ya watendaji 34 wamepatiwa mafunzo juu ya ukusanyaji wa Kodi na ada kwa Halmashauri kwa lengo la kuongeza ufanisi
4. Kutengeneza Mpango wa Takwimu (Data base) ya vianzio vya mapato.
Takwimu za wafanya biashara zenye uchambuzi wa wamiliki wa biashara na aina za biashara katika kila Shehia zimekusanywa na zitasaidia katika uwekaji wa makisio ya makusanyo na kurahisisha ufuatiliaji. Takwimu zinaonesha Halmashauri ina maduka  560 na Hoteli 11.
 2. Kuimarisha vyanzo vya mapato katika Mamlaka ya Halmashauri
1. Kufanya uendelezaji wa ujenzi wa masoko 3 (Bumbwini Mtendeni, Mahonda na Muwanda).
Ununuzi wa vifaa vya  ujenzi wa masoko mawili (Mtendeni na Muwanda) umefanyika 
 3. Kufanya mapitio na kuimarisha uelewa wa Sheria za Uendeshaji wa Halmashauri.
1. Kuelimisha jamii juu ya Sheria ndogo ndogo za Halmashauri, mazingira na usafi.
Vikao vya kutoa elimu juu ya sheria ndogo ndogo za Halmashauri, usafi wa mazingira na usafi wa wafanyabiashara vimefanyika katika Wadi zote kumi za  Wilaya ya Kaskazini B

3.      Kuendesha vikao vya Baraza na Kamati za kudumu za Halmashauri (Sheria na ustawi wa wafanyakazi , kamati ya mazingira na Kamati ya Fedha na Mipango Miji).
Vikao  vimefanyika na kujadili masuala mbali mbali ya uendeshaji wa Halmashauri na utekelezaji wa miradi ya wananchi
4. Kutekeleza miradi mbali mbali ya jamii na kusaidia vikundi katika kupunguza umaskini.
1. Kuweka kifusi njia 2 za ndani.
Njia mbili za ndani zimewekewa kifusi (Skuli ya Kinduni na Donge Njia Mtoni) ili ziweze kupitika na kuwaondolea wananchi usumbufu hasa katika kipindi cha mvua.
2. Kuweka miundo mbinu ya maji katika vijiji 9 vya Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini “B”.
Miundombinu ya maji imewekwa katika Vijiji vyote tisa (9)  vya Njia ya Mtoni, Mto Mchanga, Mswalani, Kipandoni, Mahonda Ushehani, Mahonda kwa Omar Panya, Omar Mawenge Mahonda, Mkataleni, Mbaleni na Makoba na tayari wananchi wanapata huduma ya Maji  safi na salama. Miundombinu ya umeme imewekwa katika Shehia ya Mgambo kwa kununua nguzo na waya
3. Kuvisaidia vikundi 7 pembejeo na vifaa vya kilimo.
 Vikundi saba (7) vya kilimo vimepatiwa pembejeo na vifaa vya kilimo ili kuongeza nguvu ya uzalishaji na ubora wa mazao. Vikundi vilivyopatiwa pembejeo ni Yakwao Donge, Mwerevu Hatufai, Subira Huvuta Kheri, Tusikosane, Mwenda pole, Kwa chao na Jumusama
4. Kuendeleza ujenzi wa madarasa ya skuli 3 za msingi na matengenezo ya nyumba moja ya walimu.
 Vifaa vya ujenzi vimenunuliwa na ujenzi katika Skuli 3 za msingi, Donge Mtambile, Mwanda na Donge Kipange umefanyika
5. Kufanya ujenzi wa kituo 1 na kufanya ukarabati wa kituo kimoja cha afya.
Ujenzi wa kituo cha Afya Bumbwini Kiongwe umekamilika na ukarabati wa kituo cha Afya Fujoni unaendelea kufanywa
5.Kuimarisha uendeshaji wa shughuli za ofisi
1. Kuendeleza ujenzi wa jengo jipya la Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini ‘B’ Kinduni.
Uendelezaji wa ujenzi   wa jengo jipya la Ofisi ya Halmashauri Kinduni umefanyika kwa kufanya fiting ya umeme na upigaji wa plasta.

2. Kuwalipa watendaji stahiki zao
Watendaji  wamelipwa stahiki zao za mishahara, muda wa ziada wa saa za kazi, likizo, mchango  na posho la waheshimiwa madiwani kwa kila mwezi zimelipwa

3. Mafunzo nchini
Watendaji saba (Utawala wa Rasilimali watu - Shahada ya pili 1), (Uchumi  Shahada ya kwanza 1 na Utawala wa Umma 1), ( Uhazili, Utawala wa Umma na Usimamizi wa Biashara- Stashahada 3 na cheti 1), wamesaidiwa  sehemu ya gharama ya mafunzo

4. Misaada ya mazishi na maafa.
Halmashauri imesaidia gharama za mazishi (watu 5) na kutoa msaada wa maafa kwa mfanyakazi mmoja aliyeunguliwa moto nyumba yake.

Malengo ya Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini "B" kwa Mwaka wa Fedha wa 2014/2015

 

1.     Kuimarisha ukusanyaji wa mapato yanayotokana na vianzio vya Halmashauri yatakayofikia TZS 309.7 kwa mwaka 2014/2015;
2.     Kuimarisha vyanzo vya mapato katika Mamlaka ya Halmashauri;
3.     Kufanya mapitio na kuimarisha uelewa wa Sheria za Uendeshaji wa Halmashauri;
4.      Kutekeleza miradi mbali mbali ya jamii na kusaidia vikundi katika kupunguza umaskini;
5.     Kuimarisha uendeshaji wa shughuli za Ofisi; na
6.     Kuimarisha huduma za usafi na utunzaji wa mazingira

Jadweli Namba 5: Utekelezaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kusini kwa Mwaka 2013/2014

 

Malengo ya Mwaka 2013/2014
Shughuli Zilizopangwa Kutekelezwa
Utekelezaji halisi

1. Kukusanya mapato yatakayofikia jumla ya TZS 129,886,000

1. Kukusanya mapato kupitia vyanzo mbalimbali vya Halmashauri.
Jumla ya TZS. 91,278,000/= sawa na asilimia 70 zimekusanywa.
2. Kutoa elimu juu ya umuhimu wa ulipaji ada za Halmashauri kwa wananchi na wafanya biashara
Elimu imetolewa juu ya umuhimu wa ulipaji ada za Halmashauri kwa wananchi na wafanya biashara. 
3(a) Kufanya ufuatiliaji wa ukataji wa leseni za biashara na ada ya vibali vya ujenzi.


Jumla ya lita 2,683  za mafuta ya diseli zimenunuliwa

3(b) kufanya ununuzi wa stakabadhi na ununuzi wa vitabu vya leseni.

Jumla ya vitabu 40 vya mazao, vitabu 10 vya stakbadhi na vitabu 3 vya leseni vimenunuliwa.

2. Kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo vijijini na Halmashauri
1. Uendelezaji wa jengo la ghorofa la Ofisi ya Halmashauri.
Ujenzi wa ghorofa ya kwanza unaendelea kwa kazi ya uwekaji wa   fremu za milango, kobra na uwekaji wa ‘tiles’ vyooni umefanyika
2. Kusambaza maji safi Kizimkazi Mkunguni na kusaidia vifaa vya ujenzi kwa Skuli ya Jambiani
Vifaa vya kusambazia maji safi Kizimkazi Mkunguni vimenunuliwa na mabati 84 (Danida) kwa Skuli ya Jambiani yamenunuliwa

3.Uimarishaji wa kazi za kiofisi
    
1. Kuimarisha ufanisi wa utendaji kazi kwa kununua vifaa vya kuandikia na vifaa vya matengenezo ya magari
Vifaa vya kuandikia ikiwemo karatasi, kalamu, bahasha, stepla, sola tepu na wino wa printa vimenunuliwa.
Vipuri vimenunuliwa na matengenezo ya gari na vespa yamefanyika. 
2. Kufanya vikao vya Baraza na Kamati za Kudumu.
Jumla ya vikao kumi na mbili vimefanyika, vikao 3 vya Baraza la Madiwa na vikao 9 vya Kamati zote za kudumu.
3. Kuwapatia Waheshimiwa Madiwani na wafanyakazi stahiki zao.
Waheshimiwa Madiwani   na wafanyakazi saba wa mkataba wa muda wamepatiwa stahiki zao.
4. Kuwajengea uwezo watendaji
1. Kuwapatia mafunzo ya muda mfupi na muda mrefu watendaji wawili wa Halmashauri
Wafanyakazi wawili wamelipiwa gharama za masomo katika fani ya utunzaji wa kumbukumbu na Huduma za Jamii


Malengo ya Halmashauri ya Wilaya ya Kusini kwa Mwaka wa Fedha wa 2014/2015


1.     Kukusanya Mapato yatakayofikia TZS.. Milioni 131.
2.     Uimarishaji wa kazi za kiofisi.
3.     Kuwajengea uwezo watendaji pamoja na Madiwani
4.     Kusaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi vijijini6.  HALMASHAURI YA WILAYA YA KATI

Jadweli Namba 6: Utekelezaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kati kwa Mwaka 2013/2014

Malengo ya Mwaka 2013/2014
Shughuli Zilizopangwa Kutekelezwa
Utekelezaji Halisi
1. Kufuatilia vyanzo vya mapato ili kufikia lengo kuu la kukusanya TZS.. 200,000,000/= kwa mwaka wa fedha 2013/14.
1. Ukusanya Mapato yatakayofikia Tsh.200,000,000/=
Hadi kufikia Machi 2014 Halmashauri imeweza kukusanya TZS. 137,871,502 sawa na asilimia  68 ya lengo la mwaka

2. Kusimamia na kutekeleza miradi minane ya wananchi katika wadi tofauti.1. Kusaidia utiaji nguzo za umeme katika kijiji cha Cheju pamoja na kusaidia Ushirika wa akina mama Cheju.
Nguzo 12 za umeme zimelipiwa na generator 1 na pump 1 imenunuliwa, mpira wa maji roll 1, kanga 110, kwa  ajili ya kusaidia ushiririka wa akina mama Cheju,
2. Kusaidia vikundi vya maendeleo vya akina mama kupiia viti maalum
Viti vitatu na meza 1, mabati 32, ‘hardboard’ 5, mifuko 32  ya saruji, shehena 1 ya mawe imenunuliwa kwa ajili ya kusaidiwa vikundi vya maendeleo vya akina mama.
3. Kusaidia kutia umeme katika skuli ya maandalizi ya Unguja Ukuu Kae bona
 Halmashauri imenunua vifaa vya umeme (Wire 2.5 roll 5,wa 1.5 roll 5, switch 10 pcs plug 10, main switch 1 pcs wire earth 15 pcs,earth rod 1pc socket breaker 1, cement pkt 1 nakionjut pipe) kwa kusaidia kutia umeme katika Skuli ya Maandalizi ya Unguja Ukuu Kaebona.

4. Kusaidia ujenzi wa vyoo katika skuli ya Michamvi na Ukongoroni pamoja na kituo cha afya Michamvi.

 Matofali 150, saruji mifuko 50, mchanga shehena 4, mawe shehena 4, mbao 60 vidirisha 24, mabati 24, nondo 20, kokoto shehena 2 na milango 10.
5. Usambazaji maji Bambi.
Halmashauri imesaidia vifaa vya usambazaji maji, saruji mifuko 50, nondo 4, mipira ya maji roll 6 kwa kusaidia ujenzi wa nyumba ya walimu ya Bambi.

6. Utiaji kifusi njia za ndani katika shehia ya Bungi na Kikungwi
Dizel lita 1500 na oil zimenunuliwa pamoja na malipo ya mafundi kwa utiaji kifusi njia za ndani katika Shehia ya  Bungi na Kikungwi.
3. Kusimamia na kutekeleza miradi endelevu ya kuongeza pato la Halmashauri
1. Kuanzisha kilimo cha mbogamboga (Green House)
Halmashauri  imefanya semina moja, iliyowajumuisha watendaji na madiwani iliyoendeshwa na mtaalamu wa kilimo cha mbogamboga
4. Kufanikisha utekelezaji wa shughuli za kiofisi
1. Kuwapatia stahiki zao wafanyakazi 12 wa mikataba ya muda
 Wafanyakazi 12 wamelipwa stahiki zao
2. Kugharimia safari za kikazi, gharama za petrol na matengenezo ya gari
Safari  6 za kikazi zimefanyika, lita 900 za petrol na lita 2700 za diesel zimenunuliwa kwa ufuatiliaji wa shughuli za Ofisi, pamoja na matengenezo ya gari.
3. Kugharimia matumizi ya ofisi na kuendesha kazi, malipo baada ya saa za kazi, mawasiliano, umeme, vifaa vya kuandikia, matengenezo ya zana na ujira wa benki
Posho la madiwani kwa kila mwezi limelipwa, ununuzi wa vitabu vya stakbadhi, vifaa vya kuandikia, malipo ya matumizi ya kuendesha kazi na matumizi ya ofisi yamefanyika

4. Kuendesha vikao vya Baraza la Madiwani na Kamati zake
 Vikao 7 vya Kamati na vikao 5 vya Baraza vimefanyika.
5. Kutoa Misaada kwa wananchi na kugharimia shughuli za sherehe na mapambo
Wananchi 11 wamesaid wa kwa matatizo mbali mbali yakiwemo kuunguliwa nyumba na kusafirisha mgonjwa.
5. Kuongeza taaluma kwa wafanyakazi na kuongeza vitendea kazi.
1. kununua vespa 1 kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa kazi za ofisi
Vespa 1 imenunuliwa.

2. Ununuzi wa photocopy machine 1, laptop 1, printa 1, Scaner 1 na mabao mawili ya taarifa.
Fotokopi 1 na printa 1 zimenunuliwa

Malengo ya Halmashauri ya Wilaya ya Kati kwa Mwaka wa Fedha wa 2014/2015

1.     Kukusanya Mapato yatakayofikia jumla ya TZS.. Milioni 204.
2.     Ufanikishaji wa kazi za kiofisi.
3.     Kuongeza taaluma kwa wafanyakazi, kuwajengea uwezo Madiwani na kuongeza vitendea kazi
4.     Kusaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi katika wadi tofauti


BARAZA LA MJI MKOANI

Jadweli Namba 7: Utekelezaji wa Baraza la Mji Mkoani kwa Mwaka 2013/2014

Malengo ya Mwaka 2013/2014
Shughuli Zilizopangwa Kutekelezwa
Utekelezaji Halisi
1.Kuongeza kiwango cha  ukusanyaji wa mapato kutoka TZS,35,000,000/= hadi kufikia TZS 40,000,000/= kutokana na vyanzo mbali mbali vya mapato.
1. Kuandaa ziara ya ufuatiliaji wa ukusanyaji wa mapato hadi kufikia TZS  40,000,000
Jumla ya TZS 52,965,700/= sawa na asilimia 132  zimekusanywa.
2. Kuendesha mikutano miwili ya  mikakati kwa wakusanyaji mapato.
Mikutano imefanyika.
3. Kuandaa vipeperushi vinavyohimiza umuhimu wa kulipa kodi.
Vipeperushi vimetayarishwa na kusambazwa kwa jamii.
2. Uendelezaji wa ukarabati wa soko la samaki na matunda la Mbuyuni
1.Kufanya ukarabati wa sehemu ya ndani ya soko la samaki na matunda Mbuyuni
Ukarabati umefanyika katika hatua za awali.
3. Kuimarisha vyanzo vya mapato vya baraza kwa kujenga milango minne yakufanyia biashara katika eneo la Jamhuri Garden.
Kujenga milango minne ya biashara katika eneo la Ng’ombeni.
Milango mitatu imejengwa na kufikia hatua ya uwezekaji.
4. Kuimarisha usafi wa mazingira katika eneo la Baraza la Mji kwa kujenga silabi mbili za kutunza taka katika eneo la Mbuguani.
1. Kufanya mikutano 5 ya Baraza la Madiwani na vikao 20 vya Kamati
Vikao vine vya Baraza na 16 vya kamati vimefanyika.
1.Kuipatia Ofisi vifaa vya kufanyia usafi wa mazingira katika eneo la Baraza
Vifaa vya usafi vimenunuliwa na kazi imefanyika kwa ufanisi
2. Kujenga silabi mbili katika eneo la Mbuguani.
Ujenzi wa silabi mbili umefanyika na jamii imeweza kuzitumia sehemu hizo kwa kuhifadhia taka.
5. Kusaidia miradi ya jamii katika wadi mbili za Uweleni na Mbuyuni.
1. Kusaidia ujenzi wa vidaraja eneo la Mbuyuni na kufanya ununuzi wa vifaa vya ujenzi wa Skuli ya Uweleni.
Ujenzi wa vidaraja eneo la Mbuyuni na ununuzi wa vifaa vya ujenzi kwa Skuli ya Uweleni umefanyika.


Malengo ya Baraza la Mji Mkoani kwa Mwaka wa Fedha wa 2014/2015

(i) Kuongeza kiwango cha ukusanyaji wa mapato kutoka TZS. 40 milioni hadi kufikia TZS. 70 milioni kutokana na vyanzo vyake mbali mbali vya mapato;
(ii) Kuendelea kulifanyia ukarabati soko la samaki na matunda la Mbuyuni;

(iii) Kuimarisha vyanzo vya mapato vya Baraza.

(iv) Kuimarisha usafi wa mazingira katika eneo la Baraza la Mji pamoja na kuwajengea uwezo wafanyakazi..
7.  BARAZA LA MJI CHAKE CHAKE

Jadweli Namba 8: Utekelezaji wa Baraza la Mji Chake Chake kwa Mwaka 2013/2014

Malengo ya Mwaka 2013/2014
Shughuli Zilizopangwa Kutekelezwa
Utekelezaji Halisi
1. Kuongeza kiwango cha ukusanyaji wa mapato kutoka TZS 83,000,000 mpaka TZS 100,000,000
1. Kukusanya mapato ya TZS 100,000,000
Jumla ya TZS 107,931,300/= sawa na asilimia 107 zimekusanywa.
2. Kufanya vikao 4 vya Baraza na 16 vya kamati pamoja na vikao vya watendaji
Vikao 4 vya Baraza vilifanyika na 19 vya kamati kujadili mambo tofauti ya Baraza
3. Kufanya ziara kwa Madiwani ndani ya Kisiwa cha Unguja na Pemba.
Ziara mbili za Madiwani zilifanyika ndani ya Kisiwa cha Unguja na Pemba kujadili maslahi ya Madiwani na kazi za Baraza.
4. Malipo baada ya saa za kazi kwa wafanyakazi wa Baraza la Mji
Malipo baada ya saa za kazi yalilipwa kwa watumishi waliofanya kazi katika muda wa ziada
5. Kufanya vikao na jamii hasa wafanyabiashara
Vikao vya wafanyabiashara wenye maduka, biashara ndogo ndogo na  wachuuzi vilifanyika
6. Kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa Baraza juu ya kutoa huduma bora za kuwajali wateja.
Wafanyakazi wa Baraza walipewa mafunzo ndani ya eneo la kazi ili kuweza kuwahudumia wateja
2. Kuimarisha miundo mbinu ndani ya eneo la Baraza la Mji Chake chake
1. Kutengeneza njia ya Msingini ili iweze kupitika
Kazi ya utengenezaji misingi imemalizika kwa kiwango cha zege
2.Utiaji wa kifusi njia ya Machomanne, Michakaeni na Katar
Ununuzi wa kifusi na utengenezaji wa njia umefanyika
3. Ujenzi wa vituo viwili vya kusubiria gari
Vibanda viwili vilijengwa vya kusubiria gari eneo la Madungu na Machomanne

4. Kuweka alama za Barabarani ndani ya eneo la Mji wa Chake Chake
Alama zimetengenezwa na kuwekwa mnamo husika
5. Kusaidia miradi ya maendeleo iliyoanzishwa na wananchi
Misaada tofauti ya kijamii ilitolewa kama vile kujenga daraja, kutoa mabati, matofali na fedha taslim
6. Kuhifadhi maporomoko ya ardhi katika eneo la Katar
Kazi ya kufukia na kuchawanya dongo imefanyika
7 Ujenzi wa Msingi wa Kichungwani
Msingi wenye urefu wa mita 150  ulijengwa na kukamilika kwa hatua ya awali.
8.Ujenzi wa choo cha soko la samaki Machomanne
Choo kimekamilika

9. Ujenzi wa msingi wa Mkungu malofa
Msingi umeendelezwa kwa hatua ya kuwekwa mawe na saruji
10.Kufanya matengenezo ya jengo la machinjio lililoko eneo la Tinga tinga
Kazi ya kujenga kuta, kutia milango,kutia zege katika uwanja wa machinjio ulifanyika
11.Malipo ya uchoraji wa ramani na utafiti wa mapendekezo ya ufukiaji wa sehemu ya jangwa
Kazi ya utafiti na mapendekezo ya utumiaji wa eneo la jangwa ulifanyika
12.Uwekaji wa taa za barabarani
Vifaa vya taa za barabarani vimenunuliwa na kazi kufanyika katika kiwango cha kuridhisha

13.Malipo ya upimaji wa maeneo ya Baraza la Mji ili kupata hati miliki
Baadhi ya meneo yaliyopimwa na hati miliki ya eneo moja (Katar) imepatikana
3. Kuendelea kuimarisha huduma za usafi katika eneo la Baraza la Mji kwa kuongeza vibarua na wafanyakazi
1. Ukaguzi wa masoko 4 ya Baraza la Mji
Masoko yalikaguliwa na kufanyiwa marekebisho kwa kila penye hitilafu

2.Ukaguzi wa mahoteli na nyumba za kulala wageni
Hoteli 5 na nyumba 6 za kulala wageni zimekaguliwa

3. Uzoaji wa taka na usafishaji wa maeneo tofauti ya Mji
Jumla ya tani 3,980 zilizotolewa na kupelekwa jaa kuu la VitongojiMalengo ya Baraza la Mji Chake Chake kwa Mwaka wa Fedha wa 2014/2015

(i)                 Kuongeza kiwango cha ukusanyaji wa mapato  kutoka TZS. 100 milioni na kufikia TZS. 150 milioni kutokana na vyanzo vyake mbali mbali vya mapato;
(ii)              Kuweka mazingira mazuri ya kazi na kujenga uwezo wa wafanyakazi
(iii) Kuendelea kuimarisha huduma za usafi katika eneo la Baraza la Mji kwa kuongeza vibarua na vitendea kazi; na
(iv) Kuimarisha miundombinu ya njia za ndani za Baraza la Mji zikiwemo njia za Msingini na Mkungu Malofa.


8.  HALMASHAURI YA WILAYA YA CHAKE CHAKE

Jadweli Namba 9: Utekelezaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkoani kwa Mwaka 2013/2014

Malengo ya Mwaka 2013/2014
Shughuli Zilizopangwa Kutekelezwa
Utekelezaji Halisi
1.Kuongeza ukusanyaji wa mapato kutoka TZS 36 milioni  hadi kufikia TZS 48,728,000/=.
1. Kufanya tathmini ya biashara zilziomo ndani ya Hlamashauri pamoja na ufuatiliaji wa mapato kwa ujumla ili kukusanya TZS 48,728,000/=.
Tathmini ya biashara na ufuatiliaji wa mapato katika vianzio vya mapato imefanyika ambapo jumla ya TZS 47,711,510 /=  sawa na asilimia 98 zimekusanywa.
2. Kuimarisha mazingira bora ya kufanyia kazi kwa kununua vitendea kazi
1.Kufanya matengenezo madogo madogo ya ofisi
Matengenezo madogo madogo ya ofisi yamefanyika.
2.Kufanya malipo ya mishahara kwa waajiri 2 wa muda
Malipo yamefanyika
3. Kufanya malipo ya posho la safari kwa watendaji walioshiriki kwenye vikao vya Wizara.
Malipo ya safari yamefanyika
4.Kufanya vikao 13 vya kamati na 4 vya Baraza la Madiwani
Jumla ya mikutano 13 ya Kamati na 3 ya Baraza la Madiwani wa Halmashauri imefanyika
3. Kuendelea kusaidia utekelezaji wa miradi ya  wananchi katika Halmashauri.
1. Kuimarisha ujenzi wa soko la mnada la Kichuwani
Ujenzi umefanyika na umefikia hatua ya linta.

2. Kulipa gharama za kituo cha kufanyia mtihani Skuli ya Ndagoni Chake Chake.
Malipo ya kituo yamefanyika na wanafunzi wameendelea kufanya mtihani.

3.Uwekaji wa kifusi katika njia ya Gombani Kati
Kazi ya kutia kifusi imekamilika.
4. Kumpatia mafunzo ya muda mrefu mfanyakazi mmoja katika fani ya utawala ngazi ya shahada ya uzamili.
1. Kumpatia mafunzo ya muda mrefu mfanyakazi mmoja wa Halmashauri..
Mfanyakazi mmoja amelipiwa ada na anaendelea na masomo.

Malengo ya Halmashauri ya Wilaya ya Chake Chake kwa Mwaka wa Fedha wa 2014/2015
(i) Kuongeza ukusanyaji mapato kutoka TZS. 48,728,000/= hadi kufikia 82,036,000/= kutokana na vyanzo vyake mbali mbali vya mapato;
(ii) Kuimarisha mazingira bora ya wafanyakazi, vitendea kazi na kuimarisha ofisi;
(iii) Kuendelea kusaidia utekelezaji wa miradi ya wananchi katika Halmashauri;


9.     HALMASHAURI YA WILAYA YA MKOANI

Jadweli Namba 10: Utekelezaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkoani  kwa Mwaka 2012/2013

Malengo ya Mwaka 2013/2014
Shughuli Zilizopangwa Kutekelezwa
Utekelezaji Halisi
1. Kukusanya mapato  TZS 51,265,000/=
1. Kukusanya mapato TZS 51,265,000/=
Jumla ya TZS 74,869,822/= sawa na asilimia 146 zimekusanywa.
2. Kufanya ziara mbali mbali kwa ajili ya kuboresha vyanzo vya mapato
Ziara zimefanyika katika maeneo ya Shehia za Mwambe, Mizingani, Chambani na Kiwani
2. Kuendeleza ujenzi wa soko na kuongeza sehemu za maduka katika soko la Mkanyageni.
1. Kujenga milango na kutia plasta, kutengeneza vibaraza vya kuuzia matunda na samaki.
Ujenzi wa milango, kutia plasta na vibaraza vya kuuzia matunda umefanyika.
3 Kusaidia miradi ya maendeleo ilioanzishwa na wananchi.
1. kusaidia vifaa vya ujenzi kwa wadi 5 za Mizingani, Kengeja, Wambaa, Mwambe na Chambani
Ununuzi wa vifaa umefanyika kwa wadi 5 za Halmashauri.
4 Kuimarisha ufanisi kazini na kuipatia Ofisi vitendea kazi vya kisasa.
1. Kuwapatia wafanyakazi mafunzo ya muda mrefu na mfupi kulingana na kada zao na misaada kwa ujumla
Mfanyakazi mmoja amesomeshwa mafunzo ya  Diploma katika fani ya uchapaji .
2. Kufanikisha usimamizi na kufuatilia shughuli  za Halmashauri
Ufuatiliaji wa ukusanyaji wa mapato shughuli za kazi Wizarani na safari za ufuatiliaji zimefanyika.
3. Kufanya vikao 4 vya Baraza na 10 vya kamati
Vikao vimefanyika
4. Kuendeleza ujenzi wa jengo la Halmashauri
Ujenzi wa ukanda na ukuta wa jengo la Halmashauri umefanyika.


Malengo ya Halmashauri ya Wilaya ya Mkoani kwa Mwaka wa Fedha wa 2014/2015

(i) Kukusanya jumla ya TZS. 85 milioni kutokana na vyanzo vyake mbali mbali vya mapato;
(ii) Kuendelea na ujenzi wa soko la samaki la Kangani na kujenga mabanda matatu ya madiko ya kudumu ndani ya Halmashauri;
(iii) Kusaidia miradi ya maendeleo ilioanzishwa na wananchi katika Wadi zote kumi na moja za Halmashauri.
(iv) Kuimarisha ufanisi kazini kwa kuipatia Ofisi vitendea kazi vya kisasa.


10.            BARAZA LA MJI WETE

Jadweli Namba 11: Utekelezaji wa Baraza la Mji Wete kwa Mwaka 2013/2014

Malengo ya Mwaka 2013/2014
Shughuli Zilizopangwa Kutekelezwa
Utekelezaji Halisi
1. Kuimarisha ukusanyaji wa mapato yatakayofikia TZS. 65,000,000
1. Kukusanya mapato ya TZS. 65,000,000/= kupitia vyanzo mbalimbali ndani ya Mamlaka ya Baraza la Mji la Wete
Jumla ya TZS. 42,467,890/= sawa na asilimia 65 zimekusanywa
2. Kuendesha mkutano minne kwa wakusanyaji wa mapato ili kufanya tathmini na kuibua vyanzo vipya vya mapato
Mikutano 3 imefanyika.
3. Kufanya vikao 4 vyenye lengo la kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kulipa ada za usafi.
Vikao 3 vya taaluma juu ya kulipa ada  vimefanyika na jamii imeshajihika katika kulipa ada hizo.
4. Kuandaa vipeperushi 200 vinavyohimiza umuhimu wa kulipa ada na kuvisambaza katika maeneo yote ya Baraza la Mji Wete
Vipeperushi 200 vyenye ujumbe wa  kuwahimiza wafanyabiashara juu ya umuhimu ulipaji ada vimeandaliwa na kusambazwa katika maeneo tofauti ya Mji wa Wete.
5. Kufanya ziara 6 katika vyanzo vya mapato vya Baraza la Mji Wete kwa lengo la kutathmini na kufuatilia mwenendo mzima wa ukusanyaji wa mapato.
Ziara 6 zimefanyika.
2. Kuimarisha usafi wa Baraza la Mji
1. Kufanya ukaguzi wa Hoteli 3, nyumba 2 za kulala wageni na mikahawa 10

Hoteli 3, nyumba 2 za kulaza  wageni na mikahawa  10 imekaguliwa.
3. Kukarabati jengo lililokuwa likitumika kama Soko la samaki la Kitutia (Selemu) na kulifanya kuwa ni kwa matumizi ya biashara kwa kujenga milango ya maduka 15
1. Kuandaa mchoro wa soko
Mchoro wa soko la Kitutia (Selem) umeandaliwa
4. Kuimarisha mazingira bora ya kafanyia kazi na maslahi ya wafanyakazi
1. Kufanya vikao 3 vya Baraza  pamoja na kamati zake.
Vikao vitatu vya Baraza vimefanyika pamoja na kamati zake.
2. Kuwapatia wafanyakazi stahiki zao
Wafanyakazi 94 wa kudumu na 7 wa mkataba wa muda wamepatiwa stahiki zao
5.Kuendesha shughuli za kawaida za Ofisi
1.Kugharamia safari za kikazi Unguja na Tanzania Bara kwa Waheshimiwa Madiwani na maafisa wengine wa Baraza
Malipo ya safari za Unguja na Tanzania Bara yamefanyika.
6. Kusaidia miradi ya jamii katika eneo la Baraza la Mji Wete na kuweka kifusi kituo cha magari Wete
1. Kusaidia miradi ya maendeleo katika eneo la Baraza la ji Wete
Vifaa vya ujenzi na vifaa vya kusambazia maji vimetolewa katika wadi 7 za Baraza la Mji Wete.
2. Uwekaji wa kifusi kituo cha magari Wete Mjini Shehena
Uwekaji wa kifusi kituo cha magari Wete umefanyika.1. Kuimarisha ukusanya mapato yatakayofikia 110 Milioni
2. Kuimarisha usafi katika eneo la Baraza la Mji Wete.
3. Kuendelea na ukarabati wa jengo lililokua likitumika kama Soko la samaki la Kitutia na kulifanya kuwa ni kwa matumizi ya biashara kwa kujenga milango 15 ya  maduka.
4. Kuimarisha mazingira bora ya kufanyia kazi na maslahi ya wafanyakazi
5. Kuendesha shughuli za kawaida za Ofisi.
6. Kusaidia miradi 7 ya jamii katika eneo la Baraza la Mji wa Wete na kuweka kifusi kituo cha magari Wete

12. HALMASHAURI YA WILAYA YA WETE

Jadweli Namba 12: Utekelezaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Wete kwa Mwaka 2013/2014

Malengo ya Mwaka 2013/2014
Shughuli Zilizopangwa Kutekelezwa
Utekelezaji Halisi
1. Kukusanya jumla ya TZS.. 66,424,000/= kutokana na vyanzo mbali mbali vya mapato.
1. Kukusanya mapato TZS  66,424,000/=
 Jumla ya TZS 67,419,000/= sawa na asilimia 101  zimekusanywa
2. Kufanya mikutano 9 ya wafanyakazi juu ya umuhimu wa  udhibiti wa fedha.
Mikutano imefanyika.
2. Kuimarisha  usafi wa mazingira  katika eneo la Halmashauri.
1.Kununua vifaa vya kufanyia usafi wa mazingira.
Vifaa vya usafi wa Mazingira  vimenunuliwa
3. Kufanya usafi wa mazingira maeneo ya Ole na Madenjani
Usafi katika maeneo ya Madenjani na Ole umefanyika.
3. Kuanzisha ujenzi wa soko la Gando kwa hatua ya msingi.
Kujenga soko katika hatua ya msingi.
Ujenzi umekamilika.
4.Kuimarisha mazingira  bora ya kufanyia kazi pamoja na kuipatia ofisi vitendea kazi.
1.Kuwaendeleza wafanyakazi ngazi ya Diploma.
Wafanyakazi wawili wamepatiwa mafunzo ya  uhasibu ngazi ya Diploma


2. Kuandaa mikutano 4 ya Baraza na mikutano 20 ya Kamati za Kudumu.
Mikutano 12 ya Kamati  na mikutano 3 ya Baraza  imefanyika.
3. Ununuzi wa mafuta na vilainishi
Ununuzi wa mafuta na vilainishi vimenunuliwa kwa ajili ya ufuatiliaji wa kazi za Halmashauri.
4. Kufuatilia vikao na shughuli nyengine za Halmashauri.
Madiwani na maofisa mbali mbali wameshiriki vikao na kufuatilia kazi mbalimbali za Halmashauri pia baadhi ya madeni ya safari yamelipwa
5. Ununuzi wa vifaa vya kufanyia kazi.
Risiti mbali mbali zimenunuliwa pamoja na mabuku ya vyeti vya mazao na vitabu vya leseni za biashara

7. Kugharamia uendeshaji wa Ofisi ikiwemo gharama za simu, umeme, matengenezo ya magari, viburudishaji wa Benki, msaada wa mazishi, sherehe na mapambo na matengenezo ya Kompyuta.
Shughuli mbali mbali za za kuendesha Ofisi zimetekelezwa.
5.Kuendeleza ujenzi wa ofisi ya Halmashauri kwa hatua za uwezekaji.
1.Kumalizia ujenzi wa ofisi.
Ujenzi umefikia hatua ya kuezeka.

Malengo ya Halmashauri ya Wilaya ya Wete kwa Mwaka wa Fedha wa 2014/2015


2. Kusaidia huduma za jamii na usafi wa mazingira.
3. Kuweka mazingira mazuri ya ofisi na kuwaendeleza wafanyakazi.

HALMASHAURI YA WILAYA YA MICHEWENI

Jadweli Namba 13: Utekelezaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni kwa Mwaka 2013/2014

Malengo ya Mwaka 2013/2014
Shughuli Zilizopangwa Kutekelezwa
Utekelezaji Halisi
1.Kuongeza kiwango cha ukusanyaji wa mapato kutoka 77 milioni hadi 80.4 milioni kutokana na vianzio vyake vya mapato
1. Kukusanya TZS 80.4 milioni kutoka vyanzo mbalimbali vya Halmashauri.
Jumla ya TZS. 99,236,650/= sawa na asilimia 123 zimekusanywa
2. Kufanya semina ya siku 2 kwa madiwani na watendaji, juu ya umuhimu wa kuelewa majukumu yao ikiwemo kuwahamasisha wananchi kulipa kodi za Halmashauri kwa hiari
 Semina ya siku mbili kuhamasisha  wadau  umuhimu  wa kulipa kodi  kwa hiari imefanyika. 
2. Kufanya mikutano na wadau mbali mbali wakiwemo wafanyabiashara wenye mahoteli, wachuuzi na madalali
Mikutano 5 ya wadau mbali imefanyika ambapo  wafanyabiashara wameweza kulipa  ada
3. Kuendeleza mfumo wa uwekaji wa taarifa ( Data base) za vianzio vya mapato ya Halmashauri
Mfumo wa uwekaji wa taarifa za vianzio vya mapato umeendelezwa kwenye wadi zote za Wilaya ya Micheweni.4.Kufanya ufuatiliaji na tathmini juu ya ukusanyaji wa mapato
 Ufuatiliaji na tathmini umefanyika ambapo kiwango cha ukusanyaji wa mapato kimeongezeka
2. Kuendelea na hatua ya pili ya ujenzi wa ukumbi wa mikutano
1. Kuendeleza ujenzi wa ukumbi wa mikutano Micheweni
Ujenzi unaendelea na umefikia hatua ya    linta.
3. Kuimarisha mazingira bora ya kufanyia kazi pamoja na kuipatia ofisi vitendea kazi.
1.  Kuweka mabango kwenye mipaka ya Wilaya ya Micheweni pamoja na kufanyia matengenezo bango la Ofisi na jiwe la msingi la Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya.
Mabango 2 ya mipakani yamewekwa pamoja na kuyafanyia matengenezo bango na Jiwe la msingi la Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni.
2. Kuipatia Ofisi kompyuta moja aina ya laptop
 Kompyuta moja aina ya laptop imenunuliwa
3. Kuweka samani za ofisi
Meza tatu za ofisi zimenunuliwa.
4. Kuipatia ofisi huduma za uendeshaji
Vifaa vya kuandikia vimenunuliwa pamoja na kulipia gharama za umeme, maji na mawasiliano

5. Kuvifanyia matengenezo vipando vya ofisi
Vespa mbili za Ofisi zimefanyiwa matengenezo.
6. Kuwapatia maslahi Waheshimiwa Madiwani na wafanyakazi wa muda
Madiwani 13 na wafanyakazi 8 wa muda wamepatiwa maslahi yao.
7. Kufanya vikao 15 vya Kamati za Kudumu na mikutano mitatu ya Baraza
Vikao 18 vya Kamati na mikutano 5 ya Baraza imefanyika

8. Kuwapatia mafunzo ya muda mrefu na mfupi, wafanyakazi 3, ngazi ya shahada ya pili 1, stashahada 1 na mfanyakazi 1 mafunzo ya muda mfupi.
Wafanyakazi 2 wamelipiwa ada za masomo mmoja ngazi ya shahada ya pili ya uchumi na stashahada ya Uhasibu.
3.     Kukamilisha ujenzi wa Chinjio la Mziwanda
1. Kutia, madirisha, milango na sakafu pamoja na kuchimba karo
Ujenzi umekamilika 
5. Kusaidia juhudi za wananchi katika kuimarisha huduma za afya,elimu na barabara.
1. Kusaidia ujenzi wa Skuli ya Makangale
Msaada wa vifaa ikiwemo bati, ndono na saruji vimetolewa.
2. Kusaidia ujenzi wa skuli ya Msuka
Vifaa vya ujenzi ikiwemo mabati, nondo n saruji vimetolewa

3. Kusaidia ujenzi wa choo cha jamii Micheweni
Ujenzi wa choo cha jamii unaendelea.
4. Kuweka kifusi njia ya Limani Kipange-Konde
Kazi ya uwekaji wa kifusi imefanyika.
5. Kusaidia wananchi walioathirika na majanga ya moto, Shehia ya Shumba Mjini na Maziwa n’gombe.
Jumla ya kaya 53 zilizoathirika na majanga ya moto zimesaidiwa fedha za kusaidia mahita muhimu.

Malengo ya Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni kwa Mwaka wa Fedha wa 2014/2015.


2. Kuimarisha mazingira bora ya kufanyia kazi.
3. Kuwajengea uwezo wafanyakazi na madiwani wa Halmashauri.
4. Kuimarisha miradi ya Maendeleo ya Halmashauri.
5. Kusaidia juhudi za wananchi katika kuimarisha huduma za jamii na kiuchumi.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.