Habari za Punde

Mke wa Rais Mama Mwanamwema Akabidhi Madawati na Fedha Vikundi vya Wanawake Jimbo la Uzini Unguja.

Mwanafunzi wa Darasa la Sita wa Skuli ya Mgenihaji Ndg.Maimuna Iddi, ambae ana ulemavu wa kutokuona akisoma Quran kabla ya kuazakwa hafla hiyo.
Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mhe. Mohammed Raza akimkabidhi madawati mia na viti vyake Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, hafla hiyo imefanyika katika skuli ya Mgenihaji Jimbo la Uzini Unguja.
MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akimkabidhi  Madeski Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Mgenihaji Ndg.Ali Mohammed Nassor, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya skuli ya Mgenihaji kulia Mwakilishi wa Uzini Mhe. Mohammed Raza madawati hayo yametolewa na Ndg Abdulhamid Mohammed Ali Mhoma, kupitia kwa Mwakilishi wa Uzini Mhe Mohammed Raza
MWAKILISHI wa Jimbo la Uzini Unguja Mhe. Mahammed Raza, akitowa maelezo kwa Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, wakatin wa kukuabidhi madawati kwa Skuli ya Msingi Mgenihaji Wilaya ya Kati Unguja.jumla ya madawati 100 na viti 100 vimekabidhiwa skuli hiyo jana.
Hayo ndiyo madeski ya madarasa mawili yaliojengwa na Mhe. Momahmmed Raza Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Zanzibar yakiwa katika moja ya madarasa hayo yakisubiri wanafunzi kusomea.

MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akiwahutubia Wananchi wa Jimbo la Uzini Unguja wakati wa hafla ya kukubidhi Vifaa kwa ajili ya Vikundi vya Ushirika na Madawati ya Skuli ya Msingi Mgenihaji, kulia Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dkt Idris Muslim Hija na kushoto Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif
MKE wa Balozi wa Mdogo wa China Zanzibar Bi Wu Yan, akiwasalimia Wananchi na Wanafunzi wa Mgenihaji wakati wa hafla ya kukubidhi madawati na Vifaa mbalimbali kwa Wanawake wa Mgenihaji
WANAFUNZI wa Skuli ya Msingi ya Mgeni haji Wilaya ya Kati Unguja wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akiwahutubia katika hafla ya kukabidhi madawati kwa ajili ya skuli hiyo
 Wazee wa Wanafunzi wa Skuli ya Mgenihaji wakiwa katika viwanja vya sherehe skuli ya Mgenihaji wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar akiwahutubia.

Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Zanzibar Mhe. Mohammed Raza akiwahutubia Wananchi wa Jimbo lake la Uzini wakati wa sherehe za kukabidhi madawati mio moja alioyoyakabidhi kwa Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, na kumkabidhi Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Mgenihaji.
MWALIMU Fatma Suleiman, akisoma risala ya Wananchi wa Mgenihaji wakati wa hafla wa kukabidhi madawati yaliotolewa na Mhe Mohammed Raza kwa ajili ya Skuli ya Msingi ya Mgeni haji Wilaya ya Kati Unguja
Katinu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Bi Mwanaidi Saleh , akizungumza katika hafla hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja ,Dkt.Idris Muslim Hija, akizungumza katika hafla hiyo ya kukabidhi vifaa na Madeski kwa Skuli ya Msingi Mgenihaji Unguja.  
MWAKILISHI wa Jimbo la Uzini Mhe Mohammed Raza, akimkabidhi zawadi Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, wakati wa hafla ya kukabidhi madawati ya Skuli ya Msingi Mgenihaji Wilaya ya Kati Unguja
MWAKILISHI wa Jimbo la Uzini Mhe Mohammed Raza, akimkabidhi zawadi Mke wa Makamu wa Pili wa  Rais wa Zanzibar,Mama Asha Balozi,wakati wa hafla ya kukabidhi madawati ya Skuli ya Msingi Mgenihaji Wilaya ya Kati Unguja
MKE wa Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akimkabidhi msaada wa fedha Kiongozi wa Kikundi cha Wanawake cha Hatukati Tamaa.Bi Siwa Khamis, shilingi laki tatu kwa ajili ya kukiendeleza kikundi chao

MKE wa Raisc wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akimkabidhi Vyarahani Viwili, Nyuzi na Vitambaa. Kiongozi wa  Kikundi cha Kasi Mpya.Ndg. Mwanaisha Mtumwa
MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akimkabidhi Nahodha wa timu ya Hatuna Yawa ya Bambi ilichukuwa nafasi ya Pili ya michuano ya Kombe la Muungano lililofanyika viwanja vya bambi Wilaya ya Kati Unguja. Anayeshuhudia Mke wa Balozi Mdogo wa China Zanzibar Bi Wu Yan
Wanafunzi wa Skuli ya Mgenihaji wakiimbi wimbo maalumu wa kuwataka Wazazi kuchukua jitihadi kuwahimiza Watoto kwenda Skuli kupata Elimu, wakiimba wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika viwanja vya skuli hiyo Jimbo la Uzini Zanzibar.  

1 comment:

  1. @ Mh Raza Hizi Shuhuli za Kichama au za Kiserikali?.. Maana naona kila kwenye Kusimamia au kufungua Miradi ya Maendeleo Utawaona CCM hao wako mbele.. Na haya madawati yametolewa na Balozi wa Uchina nahisi ni shuhuli za Kiserikali ambazo zilitakiwa zishuhulikiwe na Waziri wa Elimu au wasaaidizi wake na sio Mke wa raisi na mke wa Balozi wa Tanganyika Nchini Zanzibar..?...... Hata hivo CCM wanajitahidi kugawa fedha na misaada ili waonekane kama vile wanawapenda sanaa Wazanzibari...

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.