Habari za Punde

Dk Shein ampongeza Rais mpya wa Malawi

STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
 Zanzibar                                                         02 Juni, 2014
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amemtumia Salamu za Pongezi Rais Mpya wa Malawi Mheshimiwa Peter Mutharika kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Malawi kufuatia ushindi wake katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliofanyika hivi karibuni.
 
“Wananchi wa Zanzibar wanayo furaha kueleza kuridhishwa kwao kuona wananchi wa Malawi wamedhihirisha imani yao kwako na kukuchagua kuwa Rais wa nchi ya Malawi”Dk. Shein amesema.
 
Katika salamu hizo Dk. Shein alieleza matumaini ya wananchi wa Zanzibar kuwa chini ya uongozi wa Mheshimiwa Mutharika, ndugu zao wa Malawi wataendeleza umoja wao na kuimarisha maendeleo ya nchi yao.
 
“Tunatarajia kuona uhusiano kati ya Zanzibar na Malawi unaimarika kwa faida ya nchi na watu wa nchi mbili hizi na kuendeleza jitihada zaidi katika kuimarisha ushirikiano wetu wa kikanda” Salamu hizo zimeongeza.
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amemtakia Rais Mutharika afya njema, heri na fanaka katika kuiongoza nchi yake.           
Postal Address: 2422 Tel.+255 776 613 015, Fax: 024 2231822 
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.