Habari za Punde

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, Aweka Jiwe la Msingi Maskani ya Komandoo Makangale Pemba.

Mwenyekiti wa Vijana Wilaya ya Micheweni Ndg. Mselem Kombo Khatib, akisoma Quran kabla ya kuaza kwa hafla hiyo ya kukabidhi Vifaa Kikundi cha Vijana cha Tudumishe Amani na kuweka jiwe la msingi la Maskani ya Komandoo Dkt Salmini Amour Juma Makangale. 
Wananchi wa Kijiji cha Makangale Wilaya ya Micheweni Kaskazini Pemba wakimshangilia  Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, alipowasili katika kijiji cha Makangale Wilaya ya Micheweni Pemba, akiwa katika ziara yake kutembelea Mskani za Vijana wa UVCCM.   
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akiweka jiwe la Msingi la Maskani ya Komando  Dkt Salmin, katika Kijiji cha Makangale Wilaya ya Micheweni Pemba
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akiwapongeza Vijana wa Makangale kwa ujenzi wa Maskani yao baada ya kuweka jiwe la Msingi la Mskani hiyo, kulia Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi na Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM  Mhe. Shaka Hamdu Shaka
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akiwahutubia Wananchi wa Kijiji cha Makangale Wilaya ya Micheweni Pemba, akiwa katika ziara kutembelea Vikundi vya V ijana wa UVCCM Pemba.  
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif, akitowa nasaha zake kwa Wananchi wa Makangale Wilaya ya Micheweni Pemba, wakati wa kuwatambulisha Wajumbe wa Umoja wa Wake wa Wawakilishi na Wabunge wa CCM, walipofika katika Kijiji cha Makangale kutowa Msaada wa Vifaa vya Ushoni kwa Vijana wa UVCCM wa Kikundi cha Tudumishe Amani.  
Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Mhe. Shaka Hamdu Shaka, akizungumza katika hafla ya kuweka jiwe la msingi la Maskani ya Vijana ya Komandoo Dkt. Salmin Amour. Makangale

Vijana wa Maskani ya Vijana Makangale Pemba wakishangilia wakati wa hafla ya kuweka jiwe la Msingi la Maskani yao na Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein.

Mwenyekiti wa UVCCM Kaskazini Pemba Ndg. Fadhila Nassor Abdi, akitowa Salamu za Vijana wa UVCCM wa Mkoa wa Kaskazini Pemba wakati wa Hafla hiyo ya uwekaji jiwe la msingi la Maskani ya Komandoo Dkt. Salmini Amour Juma.
Vijana wa Kimasai wakicheza Ngoma ya Kimasai wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi la Maskani ya Vijana wa Makangale Pemba.
Mbunge wa Viti Maalum CCM Pemba Faida Mohammed Bakari,akitowa Salamu zake kwa Vijana wa UVCCM makangale wakati wa hafla ya kuweka jiwe la msingi la maskani yao. ya Komandoo Dkt Salmini Amour.  

Kijana wa Kikundi cha Tudumishe Amani Ndg.Maganga Mrisho akisoma risala ya Wanakikundi cha Vijana, wakati wa hafla ya kuweka jiwe la msingi la Maskani yao ya Komandoo Dkt. Salmini Amour. 
Wananchi wa Kijiji cha Makangale wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, alipofika kijiji hapo kuwawekea jiwe la Msingi la Maskani ya Komando Dkt. Salmini Amour.
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akimkabidhi Kiongozi wa Kikundi cha Tudumishe Amani Bi Mariya Juma, Vyerehani vitatu kwa ajili ya Mradi wa Vijana wa Kikundi hicho kilichoko Makangale Wilaya ya Micheweni Pemba. jumla ya Vyarahani Vitatu Majora ya Vitambaa na Pembejeo za Kilimo Wamekabidhi wanakikundi hicho cha Vijana Makangale.Pemba
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akimkabidhi Kiongozi wa Kikundi cha Tudumishe Amani Bi Mariya Juma Jora la Kitambaa kwa ajili ya Mradi wa Vijana wa Kikundi hicho kilichoko Makangale Wilaya ya Micheweni Pemba. jumla ya Vyarahani Vitatu Majora ya Vitambaa na Pembejeo za Kilimo Wamekabidhi wanakikundi hicho cha Vijana Makangale.Pemba
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akimkabidhi Fedha Katibu wa Kikundi hicho cha Tudumishe Amani Bi Mariya Juma,hafla hiyo  imefanyika katika viwanja vya Maskani hiyo Makangale Pemba. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.