Na
Hafsa Golo
SERIKALI
imeitetea Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka, kuhusu begi za dawa za kulevya
zilizotelekezwa sehemu ya kuondokea
abiria katika uwanja wa ndege wa
Zanzibar,ikisema taasisi hiyo haipaswi kubebeshwa lawama.
Waziri
wa Sheria na Katiba, Aboubakar Khamis Bakary, alisema hayo jana wakati
akihitimisha bajeti yake na kujibu hoja mbali mbali za Wawakilishi katika
mkutano wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2014/2015.
Alisema
wanaopaswa kulaumiwa ni maofisa wa uwanja huo kwa kuruhusu mtu kuingia na
mabegi hayo hadi sehemu ya kuondokea abiria bila kujulikana.
Alisema
taarifa alizonazo ni kwamba kamera za usalama zilizopo uwanjani hapo (CCTV) hazikuweza
kuwabaini walioingiza dawa hizo, hivyo hakuna sababu ya kuitupia lawama ofisi
ya DPP kwa kuwa kazi yake ni kushitaki pekee na wala si kufanya uchunguzi.
Kuhusu
mauaji ya askari polisi yaliyotokea Bububu, pia alisema DPP hapaswi kulaumiwa
kwa sababu jalada la kesi lililopelekwa na polisi kwa Mwendesha mashtaka,
halikuwa na vielelezo vinavyothibitisha kwamba wahusika ndio waliotekeleza
mauaji ya askari huyo, badala yake jalada lilianisha kosa la kuchoma matairi na
kuharibu barabara.
Hata
hivyo, alisema kuna haja ya polisi kufanya uchunguzi wa kina kuhusu matukio
mbali mbali ya kihalifu ili kuondoa lawama zinazojitokeza sambamba na maofisa
wa jeshi hilo
kujengewa uwezo wa kufanya kazi kitaalamu.
Alisema
DPP amekuwa akifanya kazi na kusimamia majukumu yake kwa mujibu wa sheria.
"Kesi
zinapokosa ushahidi wa kutosha Mkurugenzi
wa Mashtaka hawezi kuzifikisha mahakamani,” alisema.
Kuhusu
kesi kuchelewa kupata hukumu, alisema ni pamoja mashahidi kutofika mahakamani
na ukosefu wa uchunguzi wa kesi kitaalamu.
Alisema
baadhi ya wakati uchunguzi unaofanywa na polisi huwa haujitoshelezi hali
inayosababisha mahakama kuzitupilia mbali kesi hizo.
Aidha
alisema anachofahamu Katibu wa Tume ya Kurekebisha sheria, anafanya kazi zake
kwa weledi mkubwa akishirikiana na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mshibe Ali
Bakar na katika kipindi kifupi wamezifanya marekebisho sheria nyingi
zisizokwenda na wakati.
Wizara
hiyo imeomba kuidhinishiwa jumla ya shilingi 11,002,870,000 na tayari bajeti ya
wizara hiyo imepitishwa.
Hizo ni camera feki na hazifai kuwepo.
ReplyDeleteSio feki,zimefutwa ile sehemu myeti kwa manufaa ya muhusika na wadauwkae!
ReplyDelete