Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal akihutubia katika Kongamano hilo wakati wa Ufunguzi wake
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa Tanzania Ndg. Nehemia Mchechu akizungumza wakati wa Kongamano hilo Nchini Dubai.
Wageni Waalikwa katika Kongamano la Nyumba lililofanyika Nchini Dubai wakifuatilia Kongamano hilo.
Dubai, United Arab
Emirates-Katika
kile kinachoonekana ni hatua kubwa katika kuelekea kutengeneza fursa kwenye
sekta ya uendelezaji wa makazi, Shirika la Nyumba la Taifa limeweka historia
kwenye soko la kimataifa na kufanikiwa kwa mara ya kwanza kufanya kongamano la
uwekezaji hapa Dubai ambalo limefanikiwa kufikia lengo lake la kuonyesha fursa
zilizopo kwenye sekta ya ujenzi kwa makampuni makubwa ya ujenzi yaliyopo
Mashariki ya Kati na kwingineko.
Tukio hili la kipekee na kihistoria kwa Tanzania lilizinduliwa
na Makamu wa Rais Mheshimiwa Gharib Bilal na lilihudhuriwa na makampuni makubwa
ya ujenzi Dubai kama Damac, Nahkeel, Jumeirah na Emaar, ambayo yamehusika na
ujenzi wa majengo makubwa na maarufu Dubai kama Burj Khalifa, Hoteli za Jumeira
na Dubai Mall.
Makampuni mengine yaliyohudhuria kutoka ukanda wa Guba kama Qatar na Bahrain
pamoja na nchi nyingine kama Korea ,
Sweden na Romania yameonyesha kuwepo kwa nia ya makampuni
makubwa kuwekeza kwenye sekta ya makazi Tanzania .
Malengo ya Mkurugenzi
wa Shirika la Nyumba la Taifa;
Kongamano la Wawekezaji Wa Sekta ya Makazi Tanzania ni sehemu ya
lengo kuu la Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Mchechu,
ambaye kwa sasa analiongoza shirika hilo kubwa Afrika Mashariki. Kipindi cha
Msechu kwenye uongozi kimeonyesha mabadiliko na ubunifu mkubwa kwenye
uendelezaji wa sekta ya makazi nchini.
Mchechu anasema lengo kuu la kongamano hili ni hatua kubwa kuelekea
mkakati wa kuionyesha dunia kuwa Tanzania ni sehemu pekee likija swala la
uwekezaji na urudishaji wa faida kwenye sekta ya makazi.
‘Tanzania inatoa fursa ya pekee linapokuja swala la uwekezaji
kwenye sekta ya makazi barani Afrika na hii ni kutokana na uwazi pamoja na
utulivu wa kisiasa na amani inayopatikana nchini, uchumi unaokua pamoja na
ushirikiano mkubwa unaotolewa na serikali’ anasema Mchechu.
‘Tukio hili la kihistoria ni sehemu tu ya mpango kamili wa
kuifahamisha dunia kuhusu fursa za uwekezaji kwenye sekta ya makazi zinazopatikana
nchini’ alisema Mchechu.
Mchechu anaamini kuwa huu ni muda mwafaka kwa wawekezaji
kuitazama Tanzania na Afrika kwa ujumla. ‘Zamani ilikuwa ni hatari kwa
wawekezaji kuwekeza Afrika na Tanzania, lakini kwa uchumi wa leo, ni hatari
kutokuwekeza Tanzania’ alisema Mchechu.
Kati ya miradi iliyoonyeshwa kwa wawekezaji ni pamoja na miradi
mitatu ambayo itaendelezwa kwa kwa kipindi cha miaka 5. Hii inajumuisha miradi
miwili ya kuendeleza Arusha inayoitwa Safari City na USA River ambayo kwa
pamoja itakuwa na jumla ya nyumba 8000, pamoja na mradi mwingine wa kuendeleza
makazi Dar es Salaam utakaofahamika kama Salama Creek Satellite City ambao
utakuwa na jumla ya nyumba 9,500.
Miradi hii yote iko tayari kwa maana ya kuwa vibali vyote vya
mradi vimepatikana na kinachotakiwa ni kuwekeza tu, na ndio maana kongamano
hili lilikuwa muhimu kwa ajili ya kupata uwekezaji unaotakiwa.
Serikali inatimiza
wajibu wake;
Makamu wa Rais, Mheshimiwa Dr Mohamed Gharib Bilal akizungumza
na wageni waalikwa alielezea namna serikali yake imefanya kazi kubwa kwa miaka
michache iliyopita kuhakikisha inatengeneza fursa katika sekta ya makazi,
ambapo mabadiliko makubwa yalikuwa katika maeneo matatu makuu ambayo sasa
yamekuwa sheria. Maeneo hayo ni pamoja na mikopo ya nyumba, uanzishwaji wa kampuni
ya kusaidia kuwezesha mikopo ya nyumba (TMRC),pamoja na upitishaji wa sheria ya
Condominium ambazo kwa hakika zimechangia mabadiliko makubwa kwenye sekta ya
makazi.
‘Tanzania kwa sasa inashuhudia mafanikio makubwa kwenye sekta ya
makazi, huku kukiwa kuna upungufu wa jumla ya nyumba milioni 3.8 na upungufu
huo unakua kwa kiasi cha makazi 200,000 kwa mwaka, ambayo kwa hakika inatoa
changamoto kubwa kwa Tanzania lakini ni fursa kubwa kwa wawekezaji’ alisema
Bilal.
Naye Balozi wa Tanzania kwenye nchi za Falme za Kiarabu,
Mheshimiwa Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akizungumza na wageni waalikwa
alisisitiza namna sekta ya makazi ilivyoimarika nchini Tanzania.
‘Sekta ya makazi ndio sekta inayokua kwa kasi zaidi nchini
Tanzania na tunakaraibisha wawekezaji kutoka nchi za falme za Kiarabu’ alisema
Mbarouk.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa
George B. Simbachawene, anasema msingi mkuu wa kukua kwa sekta ya makazi ni
ushirikiano baina ya serikali na sekta binafsi ambao unaruhusu uwekezaji na
ukuaji mzima wa sekta.
‘Ushirikiano baina ya sekta binafsi na serikali ni muhimu kwa
ukuaji wa sekta ya makazi. Tukio kama hili linaruhusu wawekezaji kutoka nchi za
falme za Kiarabu kuona fursa zilizopo Tanzania na kuzitumia’ anasema Simbachawene.
Kiwango cha Uwekezaji
ni kipi?
Mchechu anasema kongamano la hili linalenga kufikia wawekezaji
wenye uwezo wa kuanzia dola milioni 20 hadi dola nusu bilioni.
‘Tunajua uwezo wa uwekezaji unaotakiwa hauwezi kufikiwa kwa
usiku mmoja na ndio maana miradi yetu mingi ni zaidi ya miaka 5 hadi 7, lakini
tuna miradi ambayo inaanzia dola milioni kumi hadi dola milioni mia, kwahiyo
kiasi chochote ambacho mwekezaji atakuwa nacho kati ya kiwango hicho tuna fursa
za kuwekeza’ anasema Mchechu.
Watanzania Wanaowekeza
Tanzania:
Mchechu anasema kutafuta wawekezaji hakuishii tu kwa wale walio
nje ya Tanzania bali hata kwa Watanzania, na kwa kuanza kutakuwa na kongamano
mwisho wa mwezi huu litakalofanyika Dar es Salaam ambalo litajumuisha
wawekezaji walio nchini wanaotaka kuendeleza nchi yao.
‘Hatujasawahau dada na kaka zetu nyumbani Tanzania, wengi wao wana
nafasi kubwa ya kuwekeza katika miradi ya uendelezaji wa sekta ya makazi nchi,
na tunataka kuhakikisha wanapata fursa hiyo pia’ anasisitza Mchechu.
Ushirikiano na Wadau:
Kongamano hili limefanyika kwa ushirikiano kati ya Balozi wa
Tanzania Dubai, Mheshimiwa Omary Mjenga pamoja na Balozi Maalumu wa Mambo ya
Kiuchumi, Bwana Cleophas Ruhumbika, ambao walishughulikia taratibu za kongamano
pamoja na kualika makampuni ya uwekezaji ya Dubai.
"Tuna furaha kubwa kufanya kazi bega kwa bega na Shirika la
Nyumba la Taifa kwenye tukio hili la kihistoria’ anasema Mjenga. ‘ Sehemu kubwa
ya kazi yetu hapa Dubai ni kuwezesha fursa kwa Tanzania ambayo inaendana na
wajibu wetu hapa. Pia tuna furaha kubwa kuwa tukio limekuwa la mafanikio
makubwa na nina hakika kuwa fursa zaidi za wawekezaji kuja Tanzania zitazidi
kufunguka’ anamalizia Mjenga.
No comments:
Post a Comment