Na
Fatuma Kitima,Dar es Salaam
WAZIRI
wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe, amekipongeza kiwanda cha mabomba cha Pipe
Industry Ltd, kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam kwa kutengeneza mabomba
mapya kwa teknolojia ya kisasa ambapo
kiwanda hicho kitasaidia kupunguza gharama za miradi ya maji.
Aliyasema
hayo jana jijini Dar es Salaama katika ufunguzi wa warsha ya kiwanda cha
mabomba iliyoendeshwa na kampuni ya Burouge ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE)
juu kutambulisha mabomba yanayozalishwa na kiwanda hicho.
Prof.Maghembe
alisema ni faraja kubwa kwa Tanzania
kwa kujengwa kiwanda hicho chenye ubora wa kimataifa na ni jambo zuri kwa kuwa
teknolojia hiyo mpya ipo nchini.
“Tumekuwa tukitumia pesa nyingi kuagiza
mabomba kutoka nje hivyo ni matumaini yangu kwa sasa gharama zitapungua kwa
kuwa tutakuwa tunayapa hapa nchini,” alisema.
Naye
Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda hicho, Seif Seif alisema, kiwanda hicho ni cha aina
yake na cha pekee si Tanzania
tu bali Afrika Mashariki ya Kati.
Alisema
kiwanda hicho kinazalisha mabomba imara ya kisasa kwa kutumia teknolojia ya
hali ya juu inayokidhi viwango vya kimataifa.
No comments:
Post a Comment