Na Khamisuu Abdallah
Serekali ya Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania imetiliana saini na kampuni ya Inventions Technology ya Dar es Salam, kuweka
huduma ya ideo conference katika ofisi za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Utiaji saini huo ulifanyika katika ofisi
za Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Kisauni wilaya ya magharibi Unguja,
ambapo kwa uapnde wa Serkali ya Jamhuri iliwakilishwa na Kaimu Katibu Mkuu
Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia, John Mndogo na kampuni hiyo iliwakilishwa na Mkurugenzi Mtendaji,Samwel Muro.
Akizungumza katika hafla hiyo Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,Prof. Makame Mnyaa Mbarawa, alisema vifaa
hivyo vinatarajiwa kuwekwa katika mikoa yote ya Zanzibar ili kurahisisha huduma
ya mawasiliano kwa viongozi na wananchi.
Alisema uwekaji wa vifaa hivyo
kutawezesha viongozi, watendaji na wataalamu kufanya kazi zao kwa kushirikiana
na kuwasiliana na wadau wengine wakiwa katika sehemu zao za kazi bila ya
kulazimika kusafiri na kutumia fedha.
Alisema huduma hiyo pia itapunguza
gharama na muda mkubwa unaotumika katika mawasiliano na vyombo vya usafiri
sambamba na kuimarisha mawasiliano serikalini.
Aidha alisema maeneo yatakayofungwa
mitambo hiyo ni Ofisi ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Ikulu, Ofisi za Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano, Chuo cha Amali Mkokotoni na Makunduchi Community Center kwa Unguja.
Kwa upande wa kisiwa cha Pemba alisema ni
Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Chake Chake na Ofisi ya Wizara ya Mifugo na
Uvuvi iliyopo Wete.
Alisema katika kuhakikisha matumizi ya
TEHAMA yanakuwa hasa katika ofisi za Serikali tayari wizara yake imeshafunga
mitambo hiyo katika makao makuu ya mikoa 21 ya Tanzania Bara ikiwemo ofisi ya
Waziri Mkuu, Wizara ya Fedha na ofisi ya Rais-Menejiment ya Utumishi wa Umma na
TAMISEMI.
Hata hivyo, alisema uwepo wa mkonga wa taifa
wa mawasiliano utawawezesha kuwepo kwa ufanisi mkubwa kupitia matumizi ya video
conference na serikali kwa kuwa mkonga huo una uwezo mkubwa wa mtandao wa
internet wenye kasi.
Aliongeza ujenzi wa mkonga wa taifa
unaotekelezwa kwa awamu tano ambapo awamu ya kwanza na ya pili umeshakamilika na
umeanza kutumia tokea mwaka 2012 zikiwa na jumla ya kilomita 7,560.
Alisema kwa sasa wizara yake ipo katika
hatua ya utekelezaji wa awamu ya tatu inayohusisha ujenzi wa vituo vitatu vya
kutunza kumbukumbu (internet data centres) vitakavyojengwa Dar es Salaam,
Dodoma na Zanzibar.
Akizungumzia matumizi mabaya ya mitandao,
alisema sheria zinaandaliwa ili
kuwadhibiti watu hao.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa
Miundombinu na Mawasiliano,Issa Haji Ussi aliishukuru Serikali ya Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa kuwaletea huduma hizo.
No comments:
Post a Comment