Na ShemsiaKhamis, Pemba
UJENZI wa mradi mkubwa wa kiwanda cha
sukari katika kijiji cha Kiuyu Mbuyuni wilaya ya Micheweni kisiwani Pemba,
utatumia shilingi bilioni 30.
Mkurugenzi wa kampuni ya Talon Sugar
Group kutoka India, Dk. Hamza Hussein Sabri,
alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya
kukagua eneo ambalo mradi huo utajengwa.
Alisema kiwanda hicho cha kisasa
kitawanufaisha wananchi wote wa Pemba, ambapo kampuni itawapatia miche ya miwa
na pembejeo zote kwa ajili ya kilimo hicho na baadae miwa yao wataiuza kwa kampuni hiyo.
Aidha alisema ujenzi wa mradi huo utaanza
Oktoba na na utaanza uzalishaji wa sukari mwaka ujao.
Aidha alisema kiwanda kitatoa fursa za
ajira kwa vijana wa Pemba na kusaidia
kupunguza pengo la ajira linalowaandamana vijana.
“Kiwanda
chetu hakitalima mua,kitakachofanya ni kuwapa
wakulima fursa ya kulima miwa na baadae kiwanda kitanunua miwa kwa ajili ya kuzalisha
sukari,” alisema.
Kwaupande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda
hicho,Satish Purandare, alisema kiwanda hicho hakina uhusiano wowote na kiwanda
cha sukari Mahonda kilichopo wilaya ya kaskazini B Unguja.
Nae, Ofisa kutoka Mamlaka ya Uwekezaji Vitega
Uchumi Zanzibar (ZIPA),Ali Shaaban Suleiman, alisema ujio wa wawekezaji hao
wataleta faraja kwa wananchi wa Pemba .
Hicho kitakuwa kiwanda cha pili cha
sukari Zanzibar
kikitanguliwa na kile cha Mahonda na kitakapoanza uzalishaji kitaondoa uagizaji
wa sukari kutoka nje.
No comments:
Post a Comment