Asya Hassan na
Khamis Amani
Mahakama ya Mkoa
Mwera, imemuachia huru mshitakiwa,Nasu Kassim Chande (30) mkaazi wa Muyuni ‘C’ wilaya
ya kusini Unguja, alieshitakiwa kwa kosa la kumuingilia mtoto wa mkewe, kutokana
na ushahidi kutopatikana.
Hakimu wa mahakama
hiyo, Hamisa Suleiman Hemed, alimwachia huru mshitakiwa huyo kutokana na
ushahidi uliotolewa na mashahidi kutobainisha ukweli wa kosa lililokuwa
likimkabili.
Akitoa hukumu,
hakimu huyo alisema anamuachia huru
mshitakiwa chini ya kifungu cha 219 cha sheria namba 7 ya mwaka 2004.
“Kutokana na
kutokuwepo ushahidi wa kutosha ambao ungeweza kuishawishi mahakama kukubali shitaka
dhidi yake, mahakama hii inamuachia huru mshitakiwa,” alisema.
Mshitakiwa huyo alishitakiwa
kwa kosa la kumuingilia kimwili mtoto wa mkewe na kumsababishia ujauzito, ingawa ushahidi wa
daktari haukueleza kwamba ujauzito umepatikana
lini na kama ni wa mshitakiwa.
Sababu nyengine
iliyosababisha mshitakiwa aachiwe huru ni makosa ya mashtaka, ambapo mshitakiwa
alishtakiwa kwa kumuingilia maharimu wake wakati kifungu 160 namba 7 ya mwakja
2014, kinaeleza kwamba maharimu ni mju
kuu wa kike, dada na mama na wala sio mtoto wa kambo.
“Mazingira ya kosa hili yapo yana utata kwa
kuwa kesi hii ni kubwa ushidi wake pia ulipaswa uwe mzito na wa kuridhisha,”
alisema.
Awali kwa mujibu wa
hati ya mashitaka iliyowasilishwa mahakamani hapo ilildaiwa kuwa mshitakiwa
huyo alifikishwa mahakamani hapo Oktoba 29 mwaka 2012 kujibu shutuma hizo.
Ilidaiwa tukio hilo lilitokea mwezi
usiofahamika ambapo mshitakiwa alimuingilia mtoto wa mkewe wa ndoa na
kumsababishia ujauzito kitendo ambacho ni kosa kisheria.
No comments:
Post a Comment