Habari za Punde

Balozi Seif Azungumza na Bolosi wa Israel na Muwekezaji wa Kampuni ya Aksh Opit Fibre ya Dubai.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Mkongo wa Mawasiliano { Aksh Opti Fibre } yenye makao makuu yake Dubai Bwana Chetan Choudhari  akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Chetan Choudhari  wa kampuni ya Aksh Opti Fibre ya Dubai akibadilishana mawazo na Balozi Seif katika azma ya Kampuni hiyo kutaka kuwekeza  vitege uchumi Zanzibar.

  Balozi wa Israel Nchini Tanzania Bwana Gil Haskel akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif wakati alipokwenda kuaga akikaribia kumaliza muda wake wa utumishi wa kidiplomasia hapa Tanzania.

Balozi Haskel akimuhakikishia Balozi Seif nia ya Serikali ya Irael kuendelea kugawa Taaluma yake iliyonayo hasa ile ya sekya ya kilimo  kwa nchi washirika.
Pembezoni kushoto ni Mke wa Balozi huyo wa Israel Nchini Tanzania Bibi Haskel.
 Balozi wa Israel Nchini Tanzania anayemalioza muda wake akipokea zawadi ya mlango kutoka kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kama ishara ya kumbu kumbu ya uwepo wake nchini Tanzania.
Mke wa Balozi wa Israel Nchini Tanzania Bibi Haskel akipokea zawadi ya viungo { Spice } kutoka kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.(Picha na Hassan Issa wa – OMPR )

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.