Na Khamis
Mohammed
UELEWA mdogo
wa wanajamii pamoja na imani potofu walionayo baadhi ya watu kuhusu dhana nzima
ya uzazi wa mpango, imeelezwa kuwa ni changamoto kubwa inayopelekea wanawake
wengi kutojitokeza kutumia uzazi wa mapango.
Hayo
yameelezwa na Dk.Sebastian Macrice, wakati wa mdahalo juu ya uzazi wa mpango kwa maendeleo,
uliofanyika ofisi za Kitengo Shirikishi cha Afya ya Uzazi na Mtoto,
Kidongochekundu mjini hapa.
Dk.Macrice,
alisema, baadhi ya wanawake wamekuwa wakitaka kushiriki uzazi wa mpango,
lakini, kutokana na kuwahofia waume zao, wamejikuta wakipata huduma hiyo kwa
kujificha kinyume na malengo yanayokusudiwa.
Alisema,
wanaume wengi si washiriki wazuri katika suala la afya ya uzazi, hatua
inayosababisha wanawake wanaoamini uzazi wa mpango kuamua kutumia njia za usiri
na hivyo kukosekana maridhiano baina ya pande hizo.
Alisema,
suala hilo
limefanya baadhi ya ndoa kuvunjika au kukumbwa na migogoro isiyotarajiwa
ikiwemo tuhuma za kutembea nje ya ndoa.
Dk.Macrice,
alisema, hivi sasa ni asilimia 27% ndiyo inayotumia uzazi wa mpango na kwamba
lengo linalokusudiwa ni kufikia angalau asilimia 60 ifikapo mwaka 2020.
"Safari
bado ni ndefu, vifo vinavyotokana na uzazi ni vingi, lazima jamii ibadilike,"
alisema.
Alisema,
lengo hilo
linaweza kufikiwa kwa kushirikiana na
wanajamii katika kupata elimu sahihi juu ya uzazi wa mpango sambamba na kuepuka
uzazi wa papo kwa papo.
"Uzazi
wa papo kwa papo unapelekea kuregea kwa
fuko la uzazi au wakati mwengine kupelekea kutoka damu nyingi kwa mama
mjamzito, ni hatari", alieleza.
Aidha,
alieleza, hata ulemavu wanaopata wamama ambao hawajajiandaa kubeba ujauzito nao
unaweza kuepukika kwa kutumia uzazi wa mpangilio na hivyo kupunguza vifo vya mama na watoto.
Dk.Macrice,
alisema, uzazi wa mpangilio unatoa uhueni
kwa familia katika kuwatunza watoto hao pamoja na kuwapatia huduma nzuri,
kwa vile panakuwepo na maandalizi ya kiuchumi kabla ya kupokelewa mtoto mpya.
Naye Sheikh
Ismail Asaakher kutoka Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana Zanzibar, alisema,
uislamu haukatazi uzazi wa mpango, lakini, inachosisitiza ni njia ambazo hazitaleta athari baina ya
wazazi.
"Bwana
Mtume ametuhimiza tuoane ili tuwe wengi,
lakini, kwa kuwatimizia watoto mahitaji yao
ya lazima," alisema.
Hivyo,
alisema, ni juu ya wazazi kuridhiana
bila ya kupoteza haki ya mwengine na kwamba mtoto ni zawadi ambayo
inatakiwa kupatiwa huduma.
Mapema,
Mwakilishi kutoka UMATI, Mwanajuma Salum Othman, alisema, moja ya tatizo kwa
nchi zinazoendelea ni kuongezeka kwa
idadi ya watu, hivyo uzazi wa mpango unatoa nafasi kudhiti hali hiyo.
Hata hivyo,
alisema, jamii bado haijaelewa umuhimu wa uzazi wa mpango kulingana na
rasilimali ndogo wanayowajibika nayo katika maisha ya kila siku.
No comments:
Post a Comment