Na Mwanajuma Mmanga
MWENYEKITI wa CCM
jimbo la Kwamtipura, Kombo Said Ally, amasema maendeleo ya jimbo hilo yatafikiwa endapo kutakuwa na
mashirikiano baina ya viongozi wao.
Alisema yeye yuko tayari kushirikiana na wananchi katika
kukabiliana na changamoto zinazorudisha nyuma maendeleo ya jimbo hilo .
Aliyasema hayo
wakati akizungumza na wazee wa jimbo hilo
Mkele wilaya ya mjini Unguja.
Alisema endapo
watashirikiana na kuunganisha nuvu zao watafikia malengo waliyojiwekea na
kukipatia chama ushindi katika uchaguzi mkuu ujao.
Aliwasisitiza wazee
hao kuzidisha mashirikiano na kusimamia maendeo ndani ya jimbo lao bila kujali
itikadi za kisiasa.
Nae Sheha wa shehia
ya Mkele, Khamis Khamis Mkadamu, alisema maendeleo ya jimbo hilo yatafikiwa endapo kutakuwa na
mashirikiano mazuri baina ya viongozi na
wananchi.
No comments:
Post a Comment