Na Zainab Anuwar
WASTANI ya watu 64,000 huugua kifua kikuu kila mwaka nchini Tanzania, sawa
na wagonjwa 176 kwa kila siku.
Hayo yalielewa na Daktari Damana wa hospitali ya Kuu ya Mnazi Mmoja katika
kitengo cha maradhi ya kifua kikuu na ukoma,Ali Ahmad, wakati akizungumza na
mwandishi wa habari hizi ofisini kwake Mnazi Mmoja .
Alisema watu wengi wanapata maambukizo ya maradhi ya kifua kikuu na ukoma
kwa sababu ya kutogundua mapema dalili zake na jinsi ya kujikinga.
Alisema hadi sasa kuna jumla ya wagonjwa 685 wanaoendelea na matibu katika
hospitali za Unguja na Pemba.
Hivyo, aliwataka wananchi wanapoona wana dalili za kifua kikuu wafike
hospitalini mapema kwa sababu ugonjwa huo unatibika.
Alisema watu walio kwenye hatari ya kuambukizwa ugonjwa huo ni watu
wanaoishi na VVU na watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.
Kundi jengine ni la wazee walio na umri wa kuanzia miaka 65, watu wenye
magonjwa wa muda mrefu kama vile kisukari, saratani pamoja na watoto wenye
utapiamlo.
Daktari huyo alisema wanakabiliana na changamoto mbali mbali katika
kupunguza ugonjwa huo ikiwemo jamii kuuhusisha ugonjwa huo na imani za
kishirikina.
No comments:
Post a Comment