Na Haji Nassor, Pemba
Mfanyabiashara wa kuku katika soko kuu
mjini Chake Chake Pemba, Amour Mohamed Salim (40) (Cheupe), amevamiwa na
majambazi kumpiga kwa vitu vizito usiku wa kuamjia jana.
Alisema majambazi hayo yalikuwa yamevalia
sare zinazofanana na za JKU.
Tukio hilo lilitokea nyumbani kwake
Chambani wilaya ya Mkoani Pemba, baina ya saa 7:00 na saa 8:00 usiku, wakati akiwa
amelala na familia yake.
Mashuhuda wa tukio hilo, walisema awali
walisikia kishindo kikubwa na mlio kama wa risasi, na kufuatiwa na sauti za
watu waliomtaka Cheupe atoe fedha.
Hata hivyo, walisema wakati
wakijitayarisha kutoka kwenda kumsaidia, waligundua kuwa nyumba zao zimefungwa
kwa nje na kushindwa kutoka nje hadi alipotokea jirani mwenzao kuwafungulia na
walipofika kwa mfanyabiashara huyo majambazi hayo yalikwishatokomea.
“Sisi tulisikia toa pesa, nakuua, toa
pesa, kisha tukasikia jamani nauliwa, nauliwa lakini tulipotaka kwenda kutoa
msaada, tuligundua nyumba zetu zimefungwa kwa nje,” alisema Mohamed Said Msiu mmoja wa mashuhuda hao.
Alisema majambazo hayo yalipora nguo
zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye mabegi matatu,simu ya mkononi, ufunguo wa
skuta, fedha taslimu shilingi 120,000 na vitu nyengine vya thamani.
Mke wa mfanyabiashara huyo,Mariyam Salim
Suleiman, alisema baada ya mume wake
kuvamiwa na watu, walimtaka awape shilingi milioni 10 vyenginevyo wengemua.
“Tupatie shilingi 10 milioni, ili
tukuachie uhai wako, au sisi tunakua,” alisema Mariyam akiwanukuu majambazai hayo.
Nae mfanyabiashara huyo, alisema watu hao
walivunja mlango kwa kutumia mawe na vifaa vya ujenzi.
“Mimi najisikia nafuu sana na kwa kweli
hawakuniathiri sana, lakini nguo za mke wangu na fedha taslimu wameondoka nazo,”
alisema.
Cheupe alifikishwa hospitali ya Chambani
na kupatiwa huduma ya kwanza, ambapo baadae alikwenda kituo cha polisi Mtambile
na kupatiwa fomu ya matibabu (PF3) na kwenda hospitali ya Chake Chake kutibiwa.
He mpaka pemba kuna majambazi hatari hii
ReplyDeleteHe mpaka pemba kuna majambazi hatari hii
ReplyDeletekwani pemba ni Makka?
ReplyDeleteHeeee unashangaa pemba kua na majambazi mbona hushangai kua na wachawi which is good majambazi na wachawi?
ReplyDeleteInashangaza sana sana kusikia Pemba kuna majambazi.Ujambazi katika kisiwa hichi ni sawa na mmasai kumuona anapika kaimati.Utamanudi wa WaPemba hauwendi sambamba na ujambazi.Mimi binafsi siamini kuwa Mpemba anaeishi Pemba atamfanyia Mpemba mwenzake vituko vya aina ujambazi.Kuhusu uchawi,hii ni kasumba ya wageni wanaosikiliza hadithi za kuwahusisha wa Pemba na uchawi.Kama kweli wa Pemba ni wachawi,mbona uchawi huo haukowonekana walipokuwa wakitandikwa bakora,bila sababu, mbele ya macho ya wananchi katika mazingira kama kwamba wao si binaadamu.
ReplyDelete