Na Joseph Ngilisho,Arusha
MUUZA nyama ,Lucas Lomayany Molel (37) mkazi
wa Ilboru,jijini hapa,anatafutwa na polisi kwa kosa la kumuua mkewe wa
ndoa,Agness Lucas (24) kwa kumkata mapanga, kwa kile kinachoelezwa kuwa ni wivu
wa mapenzi.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia
jana nyumbani kwa mtuhumiwa,ambapo huyo baada ya kutekeleza mauaji hayo
aliufunika mwili wa marehemu mkewe na kisha kuendelea kulala nao kitandani hadi
alfajiri alipofanikiwa kutoroka.
Mdogo wa mtuhumiwa,William Lomayany, alisema kabla ya mauaji hayo, kaka yake
alikuwa na tabia ya kumpiga mkewe na aliwahi
kumjeruhi mara kadhaa kwa kumkatakata kwa sime.
Akisimulia mauaji hayo,Williamu alisema usiku wa kuamkia jana majira ya saa 4:00,mdogo
wake alirejea nyumbani kwake na kukuta mkewe hayupo.
Alisema aliamua kumsubiri bila kulala
hadi majira ya saa 6:00 usiku ndipo mkewe aliporejea.
Alisema marehemu baada ya kufunguliwa na
kuingia ndani ,alivua nguo zote na kubakiza nguo ya ndani ambapo alijifunga
kanga na kutaka kulala,hata hivyo mtuhumiwa alimfuata chumbani na kuanza
kumhoji kujua anakotokea.
Alisema wawili hao walianza kugombana kwa
maneno ,lakini baada ya muda hali ya utulivu ilirejea ndani ya chumba hicho,
lakini majira ya saa moja asubuhi jana walipata taarifa za mauaji hayo.
Alisema mtoto wa kwanza wa mtuhumiwa,
alitwaye Jesca Lucas (11) ndiye aliyekuwa wa kwanza kufungua mlango na kutoa
taarifa kwa majirani kuwa mama yake amelala huku damu zikiwa zimetapakaa juu ya
godoro.
Alisema baada ya taarifa hiyo ndugu wa
karibu wakiwemo majirani waliingia ndani ya chumba hicho na kukuta mwili wa
marehemu ukiwa umelala chini ya dimbwi la damu ukiwa utupu.
Akizungumza mbele ya askari polisi
waliofika kushuhudia mwili wa marehemu, mtoto wa mtuhumiwa,alisema baba yake
alimwamsha usiku na kumwambia aje kufunga mlango baada ya
kutoka ndani akijua huendea alikuwa anaenda kazini.
“Baba aliniamsha usiku karibia kunakucha
akaniambia nifunge mlango aliondoka bila kusema chochote ila jana usiku baba
alikuwa akimpiga mama na alinipiga na mimi wakati namwambia amsamehe,aliniambia nilale,”
alisema.
Mauaji hayo yamesababisha mzozo mkubwa
kutoka kwa ndugu wa marehemu ambao
walivamia msiba na kuwataka ndugu wa mtuhumiwa wawapatie mwili wa marehemu
ndugu yao wakauzike ,hata hivyo upande wa pili ulizuia.
Kamanda wa polisi mkoani hapa,Liberatus
Sabas, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo
na kueleza kuwa bado uchunguzi unaendelea.
No comments:
Post a Comment