Na Fatuma Kitima,Dar es Salaam
RAIS Mstaafu wa awamu ya pili,Ali Hassan Mwinyi, amejumuika pamoja na
baadhi ya viongozi kwenye futari iliyoandaliwa na Mwenyekiti Taifa wa
JUWAQUTA,Shekh Alhad Mussa Salum.
Akitoa nasaha zake baada ya futari hiyo,
Mwinyi aliwapongeza waandaaji wa futari hiyo
kwa kuwakutanisha pamoja na kuweza kufahamiana na watu mbali mbali.
Alisema jambo la kukutana pamoja ni zuri
na linatijika hivyo alitoa rai kwa
waislamu kuendelea kukutana.
Naye Mwenyekiti wa Taifa wa JUWAKUTA,
Shekh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Musa Salum, alisema futari hiyo imekuwa
na tija kwani watu wengi wamepata fursa ya kufahamiana na kubadilishana mawazo.
Aliwashukuru viongozi waliohudhuria
katika futari hiyo na kuahidi kuendelea kuimarisha udugu wa Tanzania na
wageni.
No comments:
Post a Comment