Na Rajab Mkasaba, Ikulu
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, amewaapisha Mawaziri na
Naibu Waziri walioteuliwa juzi.
Waliopishwa ni Waziri wa Kilimo
na Maliasili, Mhe. Dk. Sira Ubwa Mamboya, Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano, Mhe.
Juma Duni Haji na Mhe. Rashid Seif Suleiman anaekuwa
Waziri wa Afya.
Wengine walioapishwa katika
hafla hiyo ni Mhe. Mahmoud Thabit Kombo kuwa Naibu Waziri wa Afya, Meja Mstaafu
Juma Kassim Tindwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja na Mhe. Omar Khamis Othman kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Wengine ni Mhe. Mwanajuma Majid Abdulla kuwa Mkuu wa Mkoa
wa Kusini Pemba, Mhe. Ayub Mohamed Mahmoud kuwa Mkuu wa Wilaya ya Magharibi na
Mhe.Hanuna Masoud Ibrahim kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Pemba.
Hafla hiyo, ilifanyika Ikulu
mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamu wa Kwanza
wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdalla Mwinyi
Khamis, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih, Kadhi Mkuu wa Zanzibar,
Sheikh Khamis Haji, Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Khatib Abrahman
Khatib,Washauri wa Rais wa Zanzibar na viongozi wengine wa Serikali.
Kabla ya uteuzi huo, Dk. Sira
Ubwa Mamboya alikuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya ambaye hivi sasa anajaza
nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Suleiman Othman
Nyanga. Mhe. Juma Duni Haji alikuwa Waziri wa Afya ambaye hivi sasa anajaza
nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa
Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Rashid Seif
Suleiman.
Mhe. Rashid Seif Suleiman
alikuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano na sasa anajaza nafasi iliyowacha wazi na Waziri wa
Wizara hiyo Mhe. Juma Duni Haji.
Meja Mstaafu Kassim Tindwa
alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba ambaye kwa hivi sasa anajaza nafasi iliyoachwa
wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Pembe Juma Khamis, Mhe.Mwajuma Majid
Abdulla alikuwa Mkuu wa Wilaya ya
Chake Chake Pemba ambaye kwa
hivi sasa anajaza nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Meja Mstaafu Juma Kassim
Tindwa.
Mhe. Omar Khamis Othman alikuwa Mkuu wa Wilaya
ya Wete ambaye hivi sasa anajaza nafasi iliyowachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa
Mkoa huo Mhe. Dadi Faki Dadi, Mhe. Ayoub Mohamed Mahmoud alikuwa Afisa Tawala
Mkoa wa Mjini Magharibi ambaye hivi sasa
anajaza nafasi iliyowachwa na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe. Hassan Mussa
Takrima.
Mhe.Hanuna Masoud Ibrahim
alikuwa Afisa Tawala Mkoa wa Kusini
Pemba ambaye hivi sasa anajaza nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.
Mwanajuma Majid Abdulla.
No comments:
Post a Comment