Habari za Punde

Polisi Z'bar :Tunamshikilia Mansour kwa kukutwa na Silaha

Jeshi la Polisi visiwani Zanzibar linamshikilia aliekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Kiembe Samaki kupitia tiketi ya CCM Bwana Mansour Yussuf Himid.
 
Akieleza sababu za kukamatwa kwake Naibu mkurugenzi wa makosa ya jinai Zanzibar wakati akizungumza na Mazrui media, Bwana Salum Msangi amesema wamemshikilia Mansour baada ya kupata taarifa za raia wema kuwa anamiliki silaha.
 
Alieleza kuwa mara baada ya kupata taarifa hio jeshi hilo liliamua kufanya msako maalumu nyumbani kwa aliekuwa Mheshimiwa huyo mnamo majira ya 2:30 asubuhi huko Chukwani nje kidogo ya mji wa Zanzibar na ndipo walipokuta silaha za aina mbili.
 
Akizitaja miongoni mwa silaha hizo Msangi amesema ni Bunduki moja aina shotgun yenye risasi 112 pamoja na bastola aina ya beretta aliokuwa na risasi 295.

Ameleza kuwa licha ya silaha hizo kumilikiwa kihalali na Mansour lakini kisheria hazikutakiwa ziwe na risasi nyingi kiasi hicho kama zilivokutwa nyumbani kwa Mansour.
 
Aidha ameleza kwa mujibu wa sheria ya Zanzibar silaha aina ya bastola ilitakiwa isizidi risasi 25 na bunduki aina ya shotgun isizidi risasi 20.
Licha hayo Naibu Mkurugenzi huyo amefafanua sheria ya Zanzibar haimruhusu mmiliki yoyote wa silaha kihalali kubaki nayo nyumbani kwake isipokuwa aikabidhi kituo cha polisi na anaweza kuifata wakati akilazimika kuitumia.
Jeshi la Polisi visiwani Zanzibar limetoa wito kwa wamiliki wote wa silaha kuzingatia sheria halali za umiliki wa silaha ili kujiepushia matatizo.

9 comments:

  1. Kwa mujibu wa shtaka atakalofunguliwa ni dhahiri Mansouri atashinda kesi hii ya kubuniwa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mbona hukusingiziwa ww wala wazee wako acha upumbuvu wa kumpendelea mwenye makosa kwa kushabikia mambo ya siasa acha kumpenda mtu fuata sheria bwege ww

      Delete
  2. Yaani mmiliki wa silaha haruhusiwi kubaki nayo nyumbani kwake isipokuwa aikabidhy kituo cha polisi na anaweza kuifata wakati akilazimika kuitumia? Does it make sence? ukivamiwa na majambazi utaifataje silaha yako polis? umevamiwa na wasokutakia mema utaifataje silaha polis? kuwa na silaha na kuikabodhy polisi ni sawa na kutoimiliki wewe na kuwa inamilikiwa na POLISI,ety ukitala kuitumia ukaichukue....Khaaaa ukishafika polisi useme nataka nikam shoot mtu POLISI wakupe silaha yako ama? silaha ni kwa self defence,na emergency inaweza kutokea anytime....kuweni na akili nyie polisi na statement zenu,wabongo wanaruhusiwa kutembea na silaha saa 24,kwanini wazanzibari mtu limit silaha zikabidhiwe polisi? it doesnt make sence hata kidogo.

    ReplyDelete
  3. Huo wanaotaka kufanya ccm ni uhuni sasa utaiwekaje silaha polisi sasa ukivamiwa na majambazi ndio uende polisi kufuata silaha hao majambazi watakusubiri kuweni wakweli musifanye mambo kama muko chooni

    ReplyDelete
  4. Tuweke mapenzi ya vyama pembeni, yeye atashinda vipi wakati kiwango cha risasi ni zaidi ya kile kinachoruhusiwa na sheria? Pia, tumeelezwa kuwa katumia risasi 5, je kazitumia wapi mbona hakutoa report polisi alipozitumia?
    Kajitia mwenyewe mtegoni na Kiembe Samaki keshaikosa, kwani hili ni kosa la jinai. Mwakilishi hatakiwi awe mwenye kosa la jinai!
    Inasikitisha vipi amemiliki nyumbani kwake idadi kubwa ya risasi kama hivi? Hii yoyote mwenye akili itamtia wasiwasi!

    ReplyDelete
    Replies
    1. FYI. Maalim Seif alizushiwa kukamatwa na nyaraka za siri za serikali. Na alikaa jela, akagombea na anashinda chaguzi zote za uraisi. Hili la Mansour halishangaza. Ilikua OK kuzimiliki akiwa waziri ingawa sheria hairuhusu, lkn sio sawa kuzimiliki sasa kwa vile SI waziri wala mwanachama wa ccm. Politiki Zenjibaria. Wacha Tanganyika waendelee sisi tuendekeze ujinga mpaka kiama.

      Delete
  5. Nyie nkodobwe acheni nsiasa zenu mansour n gaidi tiii tena lakutupwa.

    ReplyDelete
  6. Kwa kweli ni aibu - a son of a revolutionary Yussuf Himid as we knew him has turned out to become a reactionary!!!!!
    HATA BABA YAKE ANGELIKUWA HAI BASI ANGELIMNYAKA VIBAO!!!

    ReplyDelete
  7. Bila ya kuangalia sura au jina la aliyekutwa na silaha na risasi hizo, nitaangalia matakwa ya sheria kama yamezingatiwa. kwanza risasi zilizokutwa zinamilikiwa kwa mujibu wa sheria? nitapenda kujua hizo risasi zimetikanaje? zimeingizwa lini zanzibar na zilikuwa ni kiasi gani? nitapenda kujihakikishia kama kuna nyaraka zozote zinazoonesha wapi zimetoka na zilikuwa ni kiasi gani (how many have been declared). Je, risasi 5 ziko wapi na zimetumikaje endapo zilikuwepo kwenye declaration. Pia nitaangalia kwenye records zilizopita za uhalifu, je kulikuwa na maganda ya risasi kama hizo? Usalama wa wananchi wote ni dhamana ya serkali kupitia vyombo vya ulinzi na usalama.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.