Habari za Punde

ZIRPP yaandaa Mkutano na waandishi wa habari

Tunapenda kukuarifuni kuwa Mwenyekiti wa Kamati Mahsusi ya watu sita, pamoja na wajumbe wenzake, wanaitisha mkutano na waandishi wa habari kwa madhumuni ya kuelezea juu ya Waraka Mahsusi kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi utakaowasilishwa rasmi Jumatatu tarehe 04 Agosti 2014.
 
Pamoja na mambo mengine, Mwenyekiti wa Kamati Mahsusi ataelezea mapendekezo yaliyofanywa na Kamati yake kuhusiana na haja ya kuunusuru Mchakato wa Katiba na jinsi ambavyo Maslahi ya Zanzibar yatakavyoweza kulindwa na kutetewa katika jitihada za kupata katiba mpya ya Tanzania.
 
Mkutano huo na waandishi wa habari utafanyika siku ya Jumatatu, tarehe 04 Agosti 2014, katika Ukumbi wa Mkutano wa ZIRPP, Vuga kuanzia saa 05 asubuhi. Nakla ya Executive Summary ya Waraka huo itatolewa kwa waandishi wote kwa taarifa yao. Masuala na Majibu yataruhusiwa. Chai, kahawa, soda baridi na vitafunio vitatolewa bure pamoja usafiri.
 
Nyote mnakaribishwa.
 
Muhammad Yussuf
Executive Director
Zanzibar Institute for Research and Public Policy
P.O. Box 4523
Zanzibar
TANZANIA
Tel: 0777 707820 Cellular
Tel: 0242 233526 Office
Email:
yussufm@gmail.com
Weblog: www.zirppo.wordpress.com
Website: www.zirpp.info

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.