Na Rose Masaka, Maelezo
BALOZI wa amani nchini Tanzania, Risasi
Mwaulanga, ameiomba iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, kuwashawishi
wajumbe wa bunge la katiba kutoka Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kurudi
bungeni, kwa sababu tume hiyo ina ushawishi mkubwa.
Akizungumza na waandishi wa habari ukumbi
wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam, Balozi huyo pia aliwanasihi viongozi
wa dini na asasi za kiraia kutochoka kuwashawishi UKAWA kurudi bungeni
kuhakikisha Watanzania wanapata katiba waitakayo na sio katiba ya kisiasa.
Aidha alisema kauli za vitisho na
uvunjifu wa amani vinapaswa kupigiwa kelele na kulaniwa na kila mwanademokrasia
duniani katika kipindi hiki cha kuandaa katiba mpya ili wajumbe waweze kuwa
huru wakati wa kutoa maoni.
Aliwaomba UKAWA kukubali maoni ya Watanzania
walio wengi ya kuheshimu fedha za walipa kodi kwa kurudi bungeni na kupingana
kwa hoja kwani hoja zao zikiwa za nguvu hazitapingwa.
“Nawaomba
UKAWA warudi bungeni ili tuweze kupata katiba mpya itayoyomnaliza changamoto za Watanzania wote na sio masuala
ya vyama vya kisiasa na maslahi binafsi kwani vyama hiyvo vinaweza kutoweka
wakati wowote na nchi ikabaki palepale,” alisema.
Alisema ni nchi ya amani,umoja, upendo na maelewano na
siyo nchi ya vita,chuki na mafarakano hivyo Watanzania tunapaswa kutambua ni katiba
gani wanayoitaka na kuwa na mtazamo
sahihi na maamuzi bora.
Wakati huo huo, Fatina Mathias kutoka
Dodoma, anaripoti kwamba vyombo vya ulinzi na usalama vimeombwa kufuatilia nyendo za wajumbe wa Bunge Maalum
la Katiba kutoka UKAWA ili kujua nani yupo nyuma yao .
Kauli hiyo ilitolewa na Msemaji wa UVCCM,
Paul Makonda, ambaye pia ni mjumbe wa bunge hilo
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma .
Alisema vyombo hivyo vinapaswa
kulichunguza kundi hilo ili kujua nani yuko nyuma yao kutokana na wajumbe hao
kuwa na kiburi kilichopindukia.Alitoa wito kwa Watanzania na vyombo vya ulinzi
na usalama kuwa amani, umoja na uhai wa wananchi upo mikononi mwao na nia ya UKAWA sio nzuri kwa mustakabali wa taifa.
“Rais hawezi kutekeleza madai ya UKAWA ya
kulivunja bunge maalum la katiba kwa kuwa hawezi kuwa sehemu ya kuvunja sheria,kwa
nini UKAWA wanataka kumlazimisha Rais avunje sheria wakati hana mamlaka hayo kisheria zaidi ya
mamlaka ya kuteua wajumbe wa kundi la 201,” alisema.
Alisema mchakato wa kisheria lazima uende
kisheria na kuwataka wananchi kutowaunga mkono kwa uamuzi wao wa kulisusia bunge
hilo kwa kuwa
kufanyqa hivyo ni kushiriki kuvunja sheria.
Alisema kinachoshangaza kutoka kwa UKAWA
ni kubadilisha madai yao
kila kukicha.
No comments:
Post a Comment