Na Nafisa Madai
HATIMAE ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa
wa Zanzibar uliokua umekwama kwa muda mrefu, umeanza kwa kasi huku ujenzi huo
ukitarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini
kwake Kisauni nje kidogo wa mji wa Zanzibar, Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu
na Mawasiliano, Dk. Juma Malik Akil, alisema hitilafu zilizotokea hapo awali
tayari zimeshafanyiwa kazi na ujenzi unaendelea .
Alisema mradi huo uliosita miaka miwili
iliyopita kwa sababu mbali mbali unaendelea tena chini ya kampuni ya Kichina ya
BCEG ikisimamiwa na Mshauri Elekezi Kampuni ya ADPI kutoka Ufaransa.
Alisema juhudi za serikali katika
kuwaletea maendeleo wananchi wake ikiwa na pamoja na kuwajengea miundombinu
muhimu ambayo itakuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi
wa Zanzibar
itaendelea.
Alisema lengo la serikali kujenga uwanja
huo ni kufikia hadhi ya kimataifa ambayo itaweza kuitangaza Zanzibar na kuongeza idadi ya watalii.
Uwanja huo hadi kumalizika kwake
utagharimu dola za Marekani milioni128 ambazo ni mkopo wakutoka benki ya Exim
ya China
na unategemewa kuchukuwa abiria milioni 1.6 kwa mwaka na kutua ndege kubwa
ikiwemo Airbus A340 na Boeing 777.
Mratibu wa mradi huo,Yassir Dicosta, aliwaomba
Wazanzibari kutoa hofu kuhusu jengo hilo .
Mshauri elekezi kutoka kampuni ya ADPI ya
Ufaransa, Jean Mare, alisema kazi yake kubwa ni kuangalia ujenzi huo unavyokwenda.
No comments:
Post a Comment